Zimbabwe Election: Progress & Results

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,354
1,943
Nimejaribu kusoma hapa na pale kuhusu uchaguzi wa kesho Zimbabwe. Inafurahisha kwamba angalau watu wengi sasa hatimaye wameweza kuona ubaya wa Mugabe na inaonekana kesho wameamua liwe na lisiwe hawatampigia kura Mugabe. Katika somasoma yangu pia nimegundua kuwa bado kuna watu wa kutosha, japokuwa si kwa kiwango cha kumpa ushindi Mugabe, ambao bado wanampenda Mugabe. Sasa mimi najiuliza hivi hawa watu wanataka Mugabe awafanyeje ndio wamchukie maana ameshawatenda kila aina ya ubaya unaoweza kufikiria? Ninaamini kwa haya aliyokwisha kuyafanya Mugabe ingekuwa ni kwa wenzetu wazungu, hata kura za watoto na mke wake asingezipata. Sasa mimi ndio najiuliza sisi waafrika tuna matatizo gani inapokujwa kwenye kuchagua viongozi?

Ok, kwa Tanzania watu wanaoendelea kuipigia kura CCM wanatoa visingizio kwamba wapinzani wapo wachache wenye uwezo na hawana sera. Haya, na huko Zimbabwe? Mbona upinzani wameshusha kila aina ya sera na kila mwanasiasa hodari yupo kwenye upinzani, iweje basi watu waendelee kumpigia kura Mugabe na CCM ( or sorry I mean, ZANU-PF) yake?

Kibaya zaidi ni kwamba jeshi eti limesema halitatambua mshindi mwingine zaidi ya Mugabe! Sasa najiuliza tena hawa wanajeshi wa nchi zetu mafunzo yao yakoje kiasi kwamba wanashindwa kuelewa wajibu wao kwa kiwango hiki? Halafu lijamaa (Mugabe) limesema eti ikibidi litatumia style ya Kibaki huko Kenya, na limewaonya MDC ole wao wafuata mtindo aliotumia Odinga, watakiona cha mtema kuni-hii hapa soma: http://www.guardian.co.uk/commentisfree/2008/mar/28/zimbabwe

Sasa mimi ndio najiuliza, sisi wabongo (Waafrika) tuna matatizo gani hasa kwenye mambo haya ya kuchaguana?

Je, tunahitaji nadharia (theories) maalumu kwa ajili ya kuelewa siasa za Afrika?
 
Kitila,

Jeshi limeshasema haliwezi kukubali matokeo yoyote ambayo Mugabe hatashinda. Mugabe atashinda kihalali au kwa kuiba.
 
Kitila,

Jeshi limeshasema haliwezi kukubali matokeo yoyote ambayo Mugabe hatashinda. Mugabe atashinda kihalali au kwa kuiba.

Sasa mimi ndio nimechoka hapo, sasa kwa nini wanafanya uchaguzi kesho in the first place? Kwa nini wanajiangaisha wakati tayari wameshaamua ni Mugabe hadi afe?
 
Cant fault the man

494px-Robert_Mugabe.jpg
 
Sasa mimi ndio nimechoka hapo, sasa kwa nini wanafanya uchaguzi kesho in the first place? Kwa nini wanajiangaisha wakati tayari wameshaamua ni Mugabe hadi afe?

Mimi bado naamini kuwa Mugabe atashindwa na kukubali matokeo hapo kesho. Kinyume cha hapo inabidi Kikwete ajiandae kupeleka majeshi yetu zimbabwe "kulinda amani"

BTW itakuwa the same standard na ile iliyotumika kupeleka majeshi Comoro!
 
MWK,

Mugabe hawezi kukubali. Wakitaka kumshinda inabidi wafanye kama Kenya.

Mugabe aondoke maana kaiua nchi.
 
Taizo la issue ya Zimbabwe mara nyingi watu huwa hawataki kudususs form both sides of the issue.

Zimbabwe haiongozi Africa kwa HUman rights violations lakini cha ajabu husikii nchi kama Egypt au Eitrea zikilalamikiwa

let alone DRC ambako zaidi ya watu milioni 4 washauwawa

this is where you see the British hypocrisy at its best

One minute Mugabe mbaya next minute wataongeza close relationship na China. Next minute Mugabe ni mbaya jioni wanamkaribisha King Abdulla ambaye Britain and Saudi Arabia wanashared values

Wakimbizi wengi wa Zimbwabwe na hasa ambao wapo ulaya pamoja na kumchukia Mugabe, wanapenda ashinde ili waweze kuendelea kuwa wakimbizi...
 
Sasa Mugabe akishinda si itakuwa kithibitisho kingine kuwa ndivyo tulivyo au? Maana hata hilo jeshi na lenyewe choka mbaya tu sasa sijui kwa nini wanataka Mugabe ashinde...mijitu mingine bana...aaaaggghhh
 
Nyani,

watakaompigia Mugabe kura ndivyo walivyo na sio sote.
Huyu bwana to say the least ameharibu ile nchi without
avail.Yaani hata iweje atarudi mamlakani hadi kufa kwake.
There is no need for election in the first place.Na kwa
kuiba mali, anashindana na kina Mobutu na Mugabe...hio picha
hapo juu inaeza kukuhadaa eti jamaa is humble and such!
 
..Mugabe amesema akishindwa atakubali matokeo. pia amewaasa wapinzani wake wakishindwa wakubali matokeo. sijui kwanini taarifa kama hizo huwa zinafichwa.

..unajua kuna watu walizima bongo zao on the possibility kwamba Mugabe anaweza kushinda. nadhani hilo ndilo tatizo kubwa lililopo.

..baada ya Mugabe kushindwa ktk constitutional referendum ambayo haikuipigia kampeni wako waliofikiri kuwa ndiyo mwisho wake kisiasa. walionywa kwamba Mugabe akiingia vijijini na kutema sera zake basi itakuwa habari nyingine hawakusikia.

..MIMI NAOMBA MUGABE ASHINDWE NA UPINZANI UCHUKUE ZIMBABWE. WANANCHI WANATESEKA BURE KWA KUADHIBIWA NA NCHI ZA MAGHARIBI KWASABABU WAMEMPIGIA KURA MUGABE.

NB:

..Hivi si ilikubalika kwamba Mwai Kibaki ameiba uchaguzi? Sasa kwanini bado yuko madarakani tena kwa mkataba wenye baraka za wakubwa?

..Vipi kuhusu Nigeria? Hivi ule unaweza kuita ni uchaguzi kweli?
 
Wasivyo Walivyo ndio wanatakiwa kuwa wengi na kwa jinsi hali ilivyo Zimbabwe asilimia 100 ya Wazimbabwe wote walitakiwa wasiwe walivyo...hii ina maana hata uteuzi wa chama chake hakustahili kupata lakini jinsi ilivyo mijinga ikampitisha na sina hata chembe ya shaka kwamba atashinda kesho!! Ndivyo Walivyo hadi nione kinyume chake!!!
 
Mkuu unashangaa ya Zimbabwe wakati Ndo yaliyopo Tanzania. Zimbambwe kuna kituo cha kupigia kura kimeorodheshwa porini kuna kibanda KIMOJA TU lakini wapiga kura wake ni zaidi 1000. Zaidi ya hicho kibanda hakuna mtu wala mbwa katika maeneo hayo.Maana ingine hicho ni kituo feki.Mama wa upinzani analamimika nasema atalala hapo aone nani atakuja kupiga kura na anatokea wapi
 
Pamoja na ubaya wa Mugabe bado katika wale wote wanaogombea tofauti yao ni moja tu kwamba wapinzani wanayo full support ya Uingereza wakati Mugabe hana.Naungana na GT kwamba hawa watu si wakweli.Utaona wanakumbatia madikteta kibao sehemu mablimbali duniani pale ambapo maslahi yao yanalindwa,kinyume chake huyo kiongozi anakuwa hafai.

Tuchukulie mfano kwetu Tz nani asiyejua jinsi Viongozi wetu wanavyosifiwa kila siku,wananchi wanafaidika na nini? kila siku skendo za ufisadi.Angalia Ethiopia yule Meles inakadiriwa ameua watu zaidiya 10,000 wakati wa uchaguzi na kuwasweka ndani lakini ni rafiki mzuri tu wa hawa jamaa wa west,angalia ilivyokuwa kwa Musharafu.

Umefika wakati sisi waafrika tusiwe tunacheza twist kwa tune yoyote toka kwenye western media hasa uingereza.Ukifuatilia sasa hivi media za uingereza Zimbabwe kwao ni kipaumbele kuona kwamba wanamg'oa Mugabe lakini sio kwa sababu wanawatetea wananchi wa huko,ni kwa maslahi binafsi.

Tumezid mno kuamini kila wanachosema bila kufanya analysis ya kutosha ndo maana wataendelea kukwapua rasilimali zetu na kutuletea kijisehem tu kwa njia za misaada na sisi tunapiga makofi.

Iwapo Wazimbabwe wataamua kumchagua Mugabe hiyo ni juu yao,lakini sipendi kuona kiongozi hachaguliwi kwa sababu hapendwi na uingereza na australia,kisa? Wazungu wamenyang'anywa ardhi.
"ILI UKOMBOZI WA NCHI UFANIKIWE NI LAZIMA UANZE NA UKOMBOZI WA FIKRA ZA WATU WAKE" - Babu yangu (1982)
 
..Mugabe amesema akishindwa atakubali matokeo. pia amewaasa wapinzani wake wakishindwa wakubali matokeo. sijui kwanini taarifa kama hizo huwa zinafichwa.

..unajua kuna watu walizima bongo zao on the possibility kwamba Mugabe anaweza kushinda. nadhani hilo ndilo tatizo kubwa lililopo.

..baada ya Mugabe kushindwa ktk constitutional referendum ambayo haikuipigia kampeni wako waliofikiri kuwa ndiyo mwisho wake kisiasa. walionywa kwamba Mugabe akiingia vijijini na kutema sera zake basi itakuwa habari nyingine hawakusikia.

..MIMI NAOMBA MUGABE ASHINDWE NA UPINZANI UCHUKUE ZIMBABWE. WANANCHI WANATESEKA BURE KWA KUADHIBIWA NA NCHI ZA MAGHARIBI KWASABABU WAMEMPIGIA KURA MUGABE.

NB:

..Hivi si ilikubalika kwamba Mwai Kibaki ameiba uchaguzi? Sasa kwanini bado yuko madarakani tena kwa mkataba wenye baraka za wakubwa?

..Vipi kuhusu Nigeria? Hivi ule unaweza kuita ni uchaguzi kweli?

JokaKuu:

Nakubaliana kabisa na hoja yako hii. Baadhi wetu tukishasikia sababu za wakubwa (UK, USA) kumkataa kiongozi hatuchukui muda kudadisi na kuzihoji sababu hizo. Kwa bahati mbaya, watu hao hao ndio wanaozidi kuwa 'megaphone' za hao wakubwa katika kuendelea kueneza uongo wa hao wakubwa.

Kitila katoa taarifa hapo chini kuhusu wanajeshi walivyotamka, na yeye Mugabe alivyosema - sijui kama ndugu yetu amesita kidogo na kujiuliza kama hayo yaliyosemwa ni ya ukweli.

Tusitumie njia za kukidhi mahitaji yetu hata kama njia hizo siyo halali.

Sisemi kuwa Mugabe alipoifikisha Zimbabwe ni pazuri, ningetamani sana safari hii asingegombea tena. Lakini sioni hii iwe ndio sababu na mfano wa kuendelea kuwalaumu wananchi wanaofanya uchaguzi wao wenyewe. Lazima pana sababu wanazoziona wananchi wenyewe katika kufanya hivyo, tusiwe wavivu wa kujaribu kuzitafuta sababu hizo na kuzielewa. Tusiwe watu wa kulaumu tu wananchi.
 
binafsi sijaona tofauti ya yalivyo zimbabwe na tanzania,nimeangalia sky news kuhusu zimbabwe nilitamani niwaambie kuwa hayo ndio maisha ya kiafrica.
 
Kitila

Mabillionare waliotengenezwa na Mugabe watampa kura lakini waliokosa kutengeneza hayo mabillioni hawawezi kumpa. Uchaguzi utakuwa wa haki na Mugabe atashinda kwa kama asilimia 5 plus minus.

Halafu SADCC wakiongozwa na JK, Mbeki na malaya wa kutisha anayejiandaa kuongoza SA mzee Zuma watasema BRAVO BRAVO BRAVO mwendo mdundo, na walalahoi wanaolipa kodi ndio wataendelea kusaga kulia na kusaga meno.
 
Taizo la issue ya Zimbabwe mara nyingi watu huwa hawataki kudususs form both sides of the issue.

Zimbabwe haiongozi Africa kwa HUman rights violations lakini cha ajabu husikii nchi kama Egypt au Eitrea zikilalamikiwa

let alone DRC ambako zaidi ya watu milioni 4 washauwawa

this is where you see the British hypocrisy at its best

One minute Mugabe mbaya next minute wataongeza close relationship na China. Next minute Mugabe ni mbaya jioni wanamkaribisha King Abdulla ambaye Britain and Saudi Arabia wanashared values

Unfortunately, Your post raises more questions than answers: who said nowadays multiple wrongs make a right? When are we going to stop blaming others on our blunders? Certainly, to anything bad and good, there will always be external and internal factors attributable to it, but at the end of the day, you can't blame your neighbour for the poor management of your family. Mugabe and his cronies are sole responsible for, and accountable to, the ongoing woes in Zimbabwe. Again, why on earth some people seem to believe that it is only Mugabe who can stand on the way of the supposedly Zimbabwe's neo-colonialist? Aren’t there other ZANU-PF zealots who are as zealous as Mugabe to continue his struggle? Why should one person be allowed to destroy the whole nation as Mugabe has done?
 
JokaKuu:

Kitila katoa taarifa hapo chini kuhusu wanajeshi walivyotamka, na yeye Mugabe alivyosema - sijui kama ndugu yetu amesita kidogo na kujiuliza kama hayo yaliyosemwa ni ya ukweli.

Sasa mkuu, kama nimesikia mwenyewe kwenye TV na wamerudia tena jioni hii hao wanajeshi wakisema hivyo, hivi mimi tena nitafute ushahidi na ukweli gani? au wale waliokuwa wanaongea kwenye TV ni kanyaboya, tena TV ya serikali ya ZANU PF?! Hebu nisaidie hapa mkuu wangu ili tuwe pamoja!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom