Zima moto za Magufuli na uhalisia

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,410
9,182
Ushabiki unaoendelea kufanywa na wengi wetu kwa makeke yaliyoonyeshwa siku za karibuni na Rais mpya wa Tanzania Pombe Magufuli ni wa kuangalia upande mmoja tu wa sarafu. Lakini kwa maoni yangu upande wa pili wa sarafu hiyo unathibitisha maneno ya JK alompa Magufuli jina la TINGATINGA yaani utumiaji nguvu tu wa kusomba chochote kilichoko mbele, kiwe kibaya au kizuri na chenye faida au madhara.

Magufuli karithi serikali iliyooza ya JK. Na hayo anayofanya anayafanya kutaka kuthibitisha hilo. Lakini yeye alitarajia nini katika ziara zake za kushtukiza kwenye Wizara ya Fedha na Hospitali ya Muhimbili zaidi ya aliyoyakuta? Hayo si mapya, ni mambo ya kawaida katika Tanzania yetu na anayajua hata Mmachinga wa Kariakoo.

Kama kiongozi, inatakiwa kwanza aunde serikali yake, tuone hizo sura za baraza lake la mawaziri akiwemo waziri mkuu (maana uteuzi aliofanya wa Mwanasheria Mkuu umeonesha hana mpya) kisha atoe changamoto kwa mawaziri wake wote waunde wizara makini kiutendaji na kuwapa muda wa siku 100 wa kuonesha utendaji wao, kisha ndipo aanze kufanya hizo ziara zake za kushtukiza ili ajipime yeye mwenyewe na serikali aliyounda kuona ina ufanisi wa kiwango gani. Lakini anachokifanya sasa ni aina mpya ya USANII tu na kuwafanya mhanga na mbuzi wa kafara baadhi ya watu.

Kama kweli Magufuli ni kiongozi anoelewa vipaumbele vya majukumu yake alipaswa alishughulikie kwanza suala la uchaguzi wa Zanzibar ambako chama chake kimeshindwa lakini kimeamua hata kuvunja katiba ya nchi kwa kuzuia kukamilishwa mchakato wa uchaguzi.

Kabla ya kumrudia Magufuli niliseme hili kwanza, kwamba aliyeifikisha Zanzibar hapa ilipo ni JK si mtu mwengine yeyote. Maana kama alivyosema Fatma Karume, aliyewanyima Wazanzibari haki yao ya kikatiba ya kuchagua Rais wamtakaye ni yule aliyetuma jeshi la Muungano TPDF au JWTZ likazingire bwawani na kumzuia makamu mwenyekiti wa ZEC asikamilishe kutangaza matokeo ya uchaguzi. Si Jecha, Kificho wala Ali Muhammed Sheni .Tukio lile la kiharamia halikufanywa na vikosi vya SMZ ni vikosi vya ulinzi vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo Amiri Jeshi wake Mkuu ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wakati ule.

Ifahamike pia kwamba iliyopinga matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar ni CCM ambayo hadi wakati huu tunaozungumza kabla ya kukabidhiwa hatamu JPM kama anavyoitwa, inaongozwa na Mwenyekiti Taifa Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa hiyo ni yeye aliye na kauli ya mwisho ya kuamua kama chama chake kikubali au kikatae kuwa kimeshindwa katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar. Tukumbuke pia kuwa baada ya amri aliyotoa JK ya Mapinduzi dhidi ya uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika Zanzibar na ambao umepongezwa na dunia nzima wakiwemo hata wasimamizi wa ndani, JK hakutoa tamko lolote wala kuchukua hatua yoyote mpaka siku moja kabla ya kuondoka madarakani ndipo alipokubali kuonana na Maalim Seif Sharif Hamad ili eti akabidhiwe nyaraka za kuthibitisha ushindi wa cuf. Na yeye akasema, kwa kuwa kabakiwa na saa 24 tu akiwa Rais atamkabidhi suala hilo mrithi wake yaani Magufuli. Upeo wa usanii!
Ni kubwaga manyanga, kama alivyonambia ndugu yangu mmoja.

Nimalizie kusema kwamba JK ameifikisha Zanzibar mahala pabaya zaidi ya pale alipoikuta 2005 alipoingia madarakani, mahala ambapo endapo hazitofanyika jitihada za Watanzania wote na wa vyama na asasi zote huenda isipatikane njia ya kutoka kwenye mkwamo huu ila baada ya kutokea maafa makubwa ya roho za watu; namuomba Mungu ajaalie tusifike huko.

Kwa hiyo namueleza Rais mpya wa Tanzania kwamba jukumu la kwanza ambalo alipaswa kulitekeleza mara baada ya kuapishwa TU lilikuwa ni kukutana na Maalim Seif Sharif Hamad na kushauriana naye jinsi ya kuiongoza Tanzania katika mfumo mpya wa uongozi, wa kuwa na vyama viwili tofauti vinavyotawala katika pande mbili za Muungano, na si kuwadharau Wazanzibari kiasi hiki kwa kuendelea kufanya usanii wa utingatinga tunaoushuhudia hivi sasa.

Rais Magufuli anajua, kama anavyojua JK, kuwa CCM imeshindwa Zanzibar katika uchaguzi halali zaidi ya ule uliompa yeye Magufuli uhalali wa kuwa rais wa Tanzania lakini imeamua kutumia vyombo vya dola kuzuia ushindi wa CUF.

Nimalizie kwa kukumbusha tu kwamba hata Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amemhutubu moja kwa moja Magufuli katika barua yake ya kuipongeza Tanzania kwa kumaliza uchaguzi salama kuwa achukue hatua ya kuhakikisha matakwa ya Wazanzibari walio wengi yanaheshimiwa. Kwa hivyo na mimi namwomba tena JPM, kuwa badala ya kuvamia wizara au taasisi nyengine ya umma alishughulikie kwanza jukumu hilo muhimu zaidi alilonalo kama Rais wa Tanzania.

Makala ya Abdulfattah Mussa

Chanzo: Mzalendo net
 
Uzi mreefu lakin umejaa chuki. Hyo ni mipango yake ambayo amejipangia ni wapi pakuanzia. Afya ndio muhim zaidi halafu bila fedha afya itaendeshwaje?

Kama nyie mnajifanya wajuaji wa haki na mambo muhimu mbona mmeshindwa kushaur mbowe juu ya ubabe anaoufanya ndan ya cdm? Acha kuizima nyota ya magufuli ndugu
 
huenda kapitiwa nduguyo sasa unatafuta kiki usaidiwe mawazo. funguka na fanya kazi si uvivu.
 
Hawa wameshapanga CCM ichukue Zanzibar kwa nguvu kama walivyofanya huku Bara ndio maana hashughuliki na suala hili. Kama Magufuli ame hajashina kihalali unategemea atasimamia sula hili kihalali. Tunadanganyana tu hapa.
 
Uzi mreefu lakin umejaa chuki. Hyo ni mipango yake ambayo amejipangia ni wapi pakuanzia. Afya ndio muhim zaidi halafu bila fedha afya itaendeshwaje?

Kama nyie mnajifanya wajuaji wa haki na mambo muhimu mbona mmeshindwa kushaur mbowe juu ya ubabe anaoufanya ndan ya cdm? Acha kuizima nyota ya magufuli ndugu

unapinga hata hili:what:
 
Saa nyingine tujaribu kutendea haki akili zetu, hivi kama Rais anavyo vipaumbele vingi na akaona kimoja ni rahisi kutekelezeka kwa muda huu tatizo liko wapi? Unapata wapi ujasiri wa kukosoa ziara ya Rais kwenye maeneo hayo wakati Watanzania waliomchagua ndo wanahangaika kwenye hayo maeneo? wasomi wetu wamechangia kuanguka kwa taifa hili kwani wao wanachojua ni kukosoa tu.
 
Mnachosha kila mtu ana lake analotaka Rais afanye sijui kama itawezekana.

Mwacheni Rais afanye kulingana na mipango ya serikali yake.
 
Leo mtu kama simplemind anajifanya kutoa wazo eti rais afanye nini hivi inakuja kweli?
Wakat hata uwezo tu wa mawazo ya kuendesha maisha yake hana amekalia tu kubwabwaja jf leo hii anatoa nini rais afanye pumbavu
 
Last edited by a moderator:
Uzi mreefu lakin umejaa chuki. Hyo ni mipango yake ambayo amejipangia ni wapi pakuanzia. Afya ndio muhim zaidi halafu bila fedha afya itaendeshwaje?

Kama nyie mnajifanya wajuaji wa haki na mambo muhimu mbona mmeshindwa kushaur mbowe juu ya ubabe anaoufanya ndan ya cdm? Acha kuizima nyota ya magufuli ndugu

Wakati mwenzako anajadili u-taifa, wewe anajadili u-vyama!kaaaz kwelikweli.
 
Ushabiki unaoendelea kufanywa na wengi wetu kwa makeke yaliyoonyeshwa siku za karibuni na Rais mpya wa Tanzania Pombe Magufuli ni wa kuangalia upande mmoja tu wa sarafu. Lakini kwa maoni yangu upande wa pili wa sarafu hiyo unathibitisha maneno ya JK alompa Magufuli jina la TINGATINGA yaani utumiaji nguvu tu wa kusomba chochote kilichoko mbele, kiwe kibaya au kizuri na chenye faida au madhara.

Magufuli karithi serikali iliyooza ya JK. Na hayo anayofanya anayafanya kutaka kuthibitisha hilo. Lakini yeye alitarajia nini katika ziara zake za kushtukiza kwenye Wizara ya Fedha na Hospitali ya Muhimbili zaidi ya aliyoyakuta? Hayo si mapya, ni mambo ya kawaida katika Tanzania yetu na anayajua hata Mmachinga wa Kariakoo.

Kama kiongozi, inatakiwa kwanza aunde serikali yake, tuone hizo sura za baraza lake la mawaziri akiwemo waziri mkuu (maana uteuzi aliofanya wa Mwanasheria Mkuu umeonesha hana mpya) kisha atoe changamoto kwa mawaziri wake wote waunde wizara makini kiutendaji na kuwapa muda wa siku 100 wa kuonesha utendaji wao, kisha ndipo aanze kufanya hizo ziara zake za kushtukiza ili ajipime yeye mwenyewe na serikali aliyounda kuona ina ufanisi wa kiwango gani. Lakini anachokifanya sasa ni aina mpya ya USANII tu na kuwafanya mhanga na mbuzi wa kafara baadhi ya watu.

Kama kweli Magufuli ni kiongozi anoelewa vipaumbele vya majukumu yake alipaswa alishughulikie kwanza suala la uchaguzi wa Zanzibar ambako chama chake kimeshindwa lakini kimeamua hata kuvunja katiba ya nchi kwa kuzuia kukamilishwa mchakato wa uchaguzi.

Kabla ya kumrudia Magufuli niliseme hili kwanza, kwamba aliyeifikisha Zanzibar hapa ilipo ni JK si mtu mwengine yeyote. Maana kama alivyosema Fatma Karume, aliyewanyima Wazanzibari haki yao ya kikatiba ya kuchagua Rais wamtakaye ni yule aliyetuma jeshi la Muungano TPDF au JWTZ likazingire bwawani na kumzuia makamu mwenyekiti wa ZEC asikamilishe kutangaza matokeo ya uchaguzi. Si Jecha, Kificho wala Ali Muhammed Sheni .Tukio lile la kiharamia halikufanywa na vikosi vya SMZ ni vikosi vya ulinzi vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo Amiri Jeshi wake Mkuu ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wakati ule.

Ifahamike pia kwamba iliyopinga matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar ni CCM ambayo hadi wakati huu tunaozungumza kabla ya kukabidhiwa hatamu JPM kama anavyoitwa, inaongozwa na Mwenyekiti Taifa Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa hiyo ni yeye aliye na kauli ya mwisho ya kuamua kama chama chake kikubali au kikatae kuwa kimeshindwa katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar. Tukumbuke pia kuwa baada ya amri aliyotoa JK ya Mapinduzi dhidi ya uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika Zanzibar na ambao umepongezwa na dunia nzima wakiwemo hata wasimamizi wa ndani, JK hakutoa tamko lolote wala kuchukua hatua yoyote mpaka siku moja kabla ya kuondoka madarakani ndipo alipokubali kuonana na Maalim Seif Sharif Hamad ili eti akabidhiwe nyaraka za kuthibitisha ushindi wa cuf. Na yeye akasema, kwa kuwa kabakiwa na saa 24 tu akiwa Rais atamkabidhi suala hilo mrithi wake yaani Magufuli. Upeo wa usanii!
Ni kubwaga manyanga, kama alivyonambia ndugu yangu mmoja.

Nimalizie kusema kwamba JK ameifikisha Zanzibar mahala pabaya zaidi ya pale alipoikuta 2005 alipoingia madarakani, mahala ambapo endapo hazitofanyika jitihada za Watanzania wote na wa vyama na asasi zote huenda isipatikane njia ya kutoka kwenye mkwamo huu ila baada ya kutokea maafa makubwa ya roho za watu; namuomba Mungu ajaalie tusifike huko.

Kwa hiyo namueleza Rais mpya wa Tanzania kwamba jukumu la kwanza ambalo alipaswa kulitekeleza mara baada ya kuapishwa TU lilikuwa ni kukutana na Maalim Seif Sharif Hamad na kushauriana naye jinsi ya kuiongoza Tanzania katika mfumo mpya wa uongozi, wa kuwa na vyama viwili tofauti vinavyotawala katika pande mbili za Muungano, na si kuwadharau Wazanzibari kiasi hiki kwa kuendelea kufanya usanii wa utingatinga tunaoushuhudia hivi sasa.

Rais Magufuli anajua, kama anavyojua JK, kuwa CCM imeshindwa Zanzibar katika uchaguzi halali zaidi ya ule uliompa yeye Magufuli uhalali wa kuwa rais wa Tanzania lakini imeamua kutumia vyombo vya dola kuzuia ushindi wa CUF.

Nimalizie kwa kukumbusha tu kwamba hata Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amemhutubu moja kwa moja Magufuli katika barua yake ya kuipongeza Tanzania kwa kumaliza uchaguzi salama kuwa achukue hatua ya kuhakikisha matakwa ya Wazanzibari walio wengi yanaheshimiwa. Kwa hivyo na mimi namwomba tena JPM, kuwa badala ya kuvamia wizara au taasisi nyengine ya umma alishughulikie kwanza jukumu hilo muhimu zaidi alilonalo kama Rais wa Tanzania.

Makala ya Abdulfattah Mussa
Source mzalendo net

nchi inaendeshwa na miongozo na taratibu sahihi mlizojiwekea na si kukurupuka kwa watu wachache, kwa kukosa miongozo sahihi ndio maana nchi imeyumba sana baada ya kutoka nyerere; kwani miongozo ilikua kichwani mwake.
 
Mkubwa.watu kama nyie huwa hamkosekani kwenye jamii.Leo unasema kufuta safari za nje ni zima moto.!!Angekaa bila kutembelea Muhimbili kuna watu tunandugu zetu wagogwa wangeendelea kuteseka.usipende kuandika eti kwa sababu ni gharama ndogo sana kuanzisha uzi JF.Tafadhali uwe unafikili unachoandika.
Itachukua mda kumuelewa Mh.Rais JPM kwa watanzania wesio kuwa na tabia ya kusumbua akili.
 
Anatafuta cheo njoo ujiandokishe kugombea nafasi ya MSHAURI MKUU WA WALIOKUWA WAGOMBEA URAISI TZ. Kwa uwezo wako wa kuchanganya mambo kutakufaa.
Ngoja tuizindue Akili yako bila Malipo Kuibadili TANZANIA KWA HAPA ILIPOFIKIA kunatakiwa Watu wabadilike kifikra kabla ya vitendo, ndio maana Ameamua kubadili utendaji kifikra ili hata baada ya Uteuzi UNAOULILIA! Kila mteuliwa Atai TUNE akili yake.
 
Jamaa yuko sahihi mnaobisha mnayenu

mkuu kila sehem na utaratibu wake hata nyumban kwenu kuna utaratibu ambao baba yako amejiwekea namna ya kuongoza familia na sio kila mwanafamilia anaweza kutoa jambo atakalo na baba alitekeleze
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom