JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,327
- 9,326
Rangi nyekundu iliyoko kwenye hiyo alama inatosha kukuambia kwamba hilo ni tatizo ambalo linahitaji kutatuliwa haraka sana kabla halijaleta madhara makubwa.
Kwa kifupi taa hiyo humaanisha ya kwamba Presha ya oil katika engine ni ndogo.Hivyo kuipuuza kwako inaweza kupelekea engine yako kuharikibika ndani sekunde chache tu kutoka muda ilipowaka (kuzungusha engine).
Endapo taa hiyo itawaka, zima gari yako haraka sana. Kitu cha kwanza angalia kama level ya Oil iko sawa (japo kama taa hii itawaka sababu ya Oil kuwa chini basi jua Oil inakaribia kuisha kwenye engine maana kuna gari zinaweza kutembea na Oil lita moja au mbili bila kuwasha hii taa).
Kama ukikuta oil imepungua basi ongeza oil na washa gari yako, kama taa iliwaka sababu ya Oil kupungua sana basi kwa kuongeza Oil lazima itazima. Kama level ya Oil iko sawa na taa bado inawaka basi ni vema ukatafuta mtu akuvute kwenda garage ambapo unaweza ukapata msaada wa gari yako kuangaliwa, kwa maana gharama ya kuvutwa itakuwa ni ndogo kuliko gharama ya kununua engine nyingine.
Je ni nini kimepelekea taa hiyo kuwaka?
Zipo sababu zingine zinazoweza kupelekea taa hiyo kuwaka ukiachana na taa kuwaka kwa sababu ya level ndogo ya Oil. Sababu hizo ni Pampu mbovu ya Oil, Uchafu kwenye strainer/filter/Kutumia Oil filter ya bei rahisi, Oil pressure sensor kuharibika/nyaya zake kukatika n.k.
Hayo yote hutoyajua moja kwa moja mpaka gari yako ikapimwe kwenye mashine ndio unaweza kujua tatizo ni nini. Mostly kwenye mashine itainesha code kuanzia p0520 mpaka p0524. Na kama haileti code yotote basi inawezekana kujua shida kwa kuangalia Oil pressure kwenye Live Data.
NIPO MAGOMENI, MWEMBECHAI, DAR.