Zilizovuma sana

hata mimi

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
1,356
1,437
Kuna kipindi unakuta karibia nchi nzima mnazungumzia kitu kimoja tu (maneno au staili fulani). Ajabu ni kwamba mambo hayo mfano maneno watu huenda mbali zaidi na yanakuwa yanatumika kivingine kabisa tofauti hata na alivyotumia huyo aliyesababisha yavume

Hebu tujikumbushe majambo, maneno na matendo yaliyovuma na kutapakaa sana nchini mwetu katika vipindi tofauti tofauti

Tukumbushane pia na chanzo au mwanzilishi na sababu ya kitu chenyewe

Kushtua kijoti
Joti (Comedian) alianzisha kwenye Ze comedy

Wasira style
Wasira (MP) alikosea kufunga koti kwenye kikao siku moja. Kuna nguo saivi zinashonwa kwa mtindo huo

Malhedwe
Ilitokana na style ya uchezaji kwenye video ya mziki kutoka kwa Mnaijeria. Mpaka saivi mtu akianguka ghafla (mweleka) wanasema ni malelhdwe

Expansion joint
Kutoka bwenini U-DSM baada ya kiongozi mmoja kujitetea kwa kubatiza nyufa jina la 'expansion joints'

Makinikia
Kwenye kesi za Acacia na Barrics. Mpaka leo eti makinikia ya kutosha maana yake hela ya kutosha

Kwani yeye anasemaje
Hii sijui hata ni nani aliileta

Watapata tabu sana!
Afande Muroto akiwatahadharisha wanaopanga kuandamana Dodoma na kwingineko nchini

Ni Yeye
Sijui exactly imeanzia kwa nani lakini nimeanza kuiona humu wakati Lisu akigombea Urais

Anaupiga mwingi
Nimeionea humuhumu kwamba MAMA ANAUPIGA MWINGI na wakafafanua wenye lugha yao kwamba anafanya vizuri (anatekeleza jukumu kwa usahihi)

Mkalimani
Kwenye kifo cha Magufuli (Raisi) mkalimani ali translate ndivyosivyo maneno ya mgeni mmoja hivi basi mpaka leo utasikia ofisini "jamani twendeni tukakalimani chai kwanza ndipo tuje tuendelee"

Wajumbe
Maswala ya uchaguzi. Nakumbuka majina ya watu waliodhaniwa wangekuwa 'wao' yalikatwa kwenye kura za maoni bila huruma na wajumbe wa mikutano husika. Kwa humu hii kitu WAJUMBE ilivuma sana kupitia Paul Makonda, Gwajima na wengineo maarufu

Hamza
Japo imezima haraka sana lakini tayari ilikuwa imeanza lugha ya "Polisi wanaogopa kuhamzuliwa siku hizi"

Demka
Raisat Samia alisema wabunge wanademka bungeni

Mke wa Yesu
Spika Ndugai katika makali yake na hii kitu mpaka leo kumekuwa na memes kibao za mheshimiwa huwa nachekaga sana

Corona, Barakoa, Sanitizer, Karantini, Chanjo, na mfano wa hayo. Misamiati hiyo imekuwa maarufu sana kupitia majanga ya ugonjwa

Tozo
Hapa napo mpaka vibabu wanajua yaani. Tozo tozo tozo, Kuna Tozoland, kuna TZ= TOZO nk
 
Tuendelee tu kusikilizia. Hebu tujikumbushe.
Naughty boy Tundu Lissu anauliza Mbona Sasa ni wiki mbili haonekani?

Mara taarifa zavuma amezimia kupelekwa Nairobi, Nairobi wamesema haponi asifie kwetu, wanampeleka India Sasa, Mara ndege imebadili uelekeo Sasa yaenda Ujerumani.
Mara Nzena limetokea la kutangazwa.
 
Back
Top Bottom