Zilivyo balozi mbalimbali za Tanzania huko ng'ambo - Aibu tupu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zilivyo balozi mbalimbali za Tanzania huko ng'ambo - Aibu tupu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tungaraza Jr, Aug 24, 2012.

 1. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  *Baadhi hawajalipwa mishahara miezi sita, zimeajiri Wakenya*Ufaransa pango Sh milioni 720, wanatumia anwani ya Uganda*Ofisi zinaporomoka, Kikwete asema Richmond imeiponza nchi*Membe alia Serikali kukata bajeti yake ikabaki asilimia 44 tu

  Mishahara ya mabalozi

  Taarifa ya Kamati inaonyesha kuwa baadhi ya balozi za Tanzania nje ya nchi, watumishi na mabalozi wanaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu. "Hadi wajumbe wanafanya ziara katika Ubalozi huu [Stockholm, Sweden], watumishi wa Serikali walikuwa wamepata mishahara yao hadi kufikia Machi na hawakuwa wamepata mishahara ya miezi mitatu wakati wajumbe wa Kamati wanaondoka Stockholm tarehe 29 Juni, 2012," inasema sehemu ya taarifa hiyo.

  Tatizo la mishahara lipo katika balozi mbalimbali, na baadhi ya balozi kama Msumbiji wafanyakazi wamefikia uamuzi kuwa walipwe mishahara yao kupitia akaunti za benki zilizopo hapa nchini Tanzania, hali inayowanusuru kwani kwa njia hii wanapata mishahara kwa wakati sawa na watumishi wa Serikali waliopo hapa nchini. Katika eneo hili, vibarua wanaotumikia balozi za Tanzania katika sehemu mbalimbali duniani zilipo ofisi za balozi za Tanzania, wanadai malipo kwa muda mrefu na kupata usumbufu.

  Kamati inapendekeza pia kuwa fedha zinazotengwa kwa ajili ya balozi hizi, badala ya kupelekwa kwanza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kisha ndipo zitumwe kwenye balozi husika, utaratibu ubadilishwe, Hazina itume fedha hizo moja kwa moja kwenye balozi kama ilivyo kwa halmashauri za miji na manispaa hapa nchini.

  Kodi ya pango, anwani ya Uganda

  Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa unakabiliwa na changamoto nyingi ajabu. Tanzania haina jengo pale Ufaransa, hivyo inapangishwa katika jengo linalomilikiwa na Serikali ya Uganda, lakini pia kuna aibu ya ziada.

  "Hakuna jengo la Serikali kwa ajili ya ofisi na nyumba za watumishi, hivyo umepangishwa (ubalozi) na Uganda pamoja na kutumia sanduku la posta la Uganda. Hata mkalimani anayetumika ni Mkenya," inasema taarifa hiyo iliyosainiwa na Makamu Mwenyekiti, Mussa Zungu.

  Baada ya kuona shida wanayopata watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, New Zealand iliamua kuiuzia Tanzania jengo inalolimiliki nchini Ufaransa kwa bei nafuu, lakini Serikali ya Tanzania haijatoa jibu iwapo italinunua jengo hilo au la na ifikapo mwezi ujao wa Septemba, ofa hiyo itafutika. "Ubalozi umekuwa ukiathirika na gharama kubwa unayotumia kwa ajili ya kodi ya kupanga ofisi na nyumba sita za watumishi. Hali hii huugharimu ubalozi kiasi cha euro 31,435.40 (Tshs 59,727,260) kwa mwezi ambazo ni sawa na Th 716,727,120 kwa mwaka na ni asilimia 34 ya bajeti ya ubalozi," inasema sehemu ya taarifa hiyo.

  Tatizo la kupanga na kulipa gharama kubwa ya pango liko katika balozi nyingi za Tanzania, hivyo Kamati imependekeza kuwa Serikali iziruhusu balozi kununua majengo kwa utaratibu wa kuweka mali rehani (mortgage financing), ili kiasi kinachotumika kulipa pango kwa sasa kitumike kulipia nyumba zilizonunuliwa baada ya muda ziwe mali ya Tanzania.

  Majengo yana hali mbaya

  Majengo mengi ya Balozi za Tanzania nje ya nchi yamechakaa kwa kiwango cha kutisha. Mapaa yanavuja, mifumo ya umeme haifanyi kazi, na baadhi ya majirani wanalalamika kuwa uchakavu wa majengo ya Tanzania unapunguza thamani ya nyumba zilizo jirani na majengo hayo katika miji mbalimbali.

  Ottawa, Canada

  Hapa kuna tatizo la uwakilishi mpana, Kamati imependekeza kuwa ufunguliwe ubalozi nchini Cuba badala ya kutegemea Ubalozi wa Canada. Pia kuna tatizo la Watanzania wanaofanya kazi ubalozini kulipishwa kodi, ila hii imetokana na Tanzania kuwalipisha kodi watumishi wa Ubalozi wa Canada waliko Tanzania, hivyo nchi hiyo inasema mabalozi wao nao wakiacha kulipishwa kodi nao wataacha kuwalipisha kodi watumishi wa Ubalozi wa Tanzania.

  Washington, Marekani

  Jengo Na 2139 R Street, NW Washington DC, linalomilikiwa na Serikali jijini Washington, limeendelea kuchakaa kwa Serikali kutotoa ruhusa likarabatiwe. Hadi sasa wamejitokeza wapangaji wenye nia ya kupanga katika jengo hilo ambao wangelipa wastani wa kodi ya dola 400,000 kwa mwaka, karibu Sh milioni 600 za Tanzania, lakini kwa mwaka mzima sasa Serikali imeshindwa kutoa uamuzi wa kuwakubalia wapange jengo hili linaloendelea kuoza. Pia ubalozi huu una kashfa ya kuajiri Watanzania ‘waliojilipua' nchini Marekani kama watumishi wenyeji. "Kuna watumishi wenyeji (local based) ambao ni Watanzania waliozamia nchini humo [Marekani] kitu ambacho ni kinyume cha sheria," inasema taarifa hiyo.

  New York, Marekani

  Kwenye ubalozi huu kuna tatizo la kukosa ruhusa ya kutumia maduhuli wanayokusanya. Nyumba ya Balozi wa Tanzania UN 30 Overhill Road, Mount Venon, ina hali mbaya kiasi kwamba haikaliki. Kamati imeshauri ikarabatiwe haraka. Kamati imeishauri Serikali kununua nyumba ambayo kwa sasa Ubalozi wa Tanzania unapanga inayouzwa Na. 86 Judson Avenue, Dobbs Ferry, New York. Kwa kuwa katika Umoja wa Mataifa kuna masuala mengi, Kamati imependekeza kila wizara hapa nchini iwe na dawati la Umoja wa Mataifa litakalosaidia kuratibu shughuli za umoja huo.

  Beijing, China

  Katika ubalozi huu kuna tatizo sawa na balozi nyingine wakati jengo la ubalozi limechakaa sehemu kubwa inavuja na lina nyufa. Pia sheria ya China inataka gari liendeshwe si zaidi ya miaka 10, lakini ubalozi unatumia gari lililonunuliwa mwaka 2001 hivyo Tanzania inavunja sheria kwa balozi kuendesha gari chakavu. Pamoja na umuhimu wa pekee ilionao China katika uchumi wa dunia ya sasa, hadi leo hakuna Mtanzania mtaalamu wa masuala ya uchumi anayefanya kazi katika ubalozi huu. Kamati inapendekeza mtu huyu ateuliwe haraka. Kamati pia inashauri kutokana na China kuwa na fursa nyingi za kiuchumi, Balozi wa Tanzania nchini China awe na wasaidizi wawili huku ikipendekeza uanzishwe Ubalozi Mdogo katika mji wa viwanda wa Guang-zhou. China pia imeipa Tanzania fursa ya kulipia ada wanafunzi 100 ikiwa Tanzania itaamua kusomesha idadi kama hiyo. Kamati imeishauri Bodi ya Mikopo kutumia fursa hiyo kwa kupeleka Watanzania masomoni China (scholarships).

  Tokyo, Japan

  Ubalozi huu una uhaba wa magari na watumishi. Lakini pia wana tatizo la msingi: "Ubalozi unapoomba taarifa na ufafanuzi wa masuala muhimu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa hukosa taarifa hizo au kupata kwa kuchelewa," inasema taarifa ya kamati. Hili ni tatizo sugu kwa balozi karibu zote. Pia kuna tatizo kuwa asasi za kiraia za Japan zilitoa msaada wa kompyuta 1,000 kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na magari ya wagonjwa kwa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, isipokuwa Serikali hadi sasa haijarudisha ‘export certificate' kuonyesha kuwa msaada huo uliwafikia walengwa, hali inayowatia shaka Wajapani kudhani kuwa labda uliyeyukia njiani. Kamati imeona fursa na inapendekeza Tanzania ianze mara moja mkakati wa biashara na nchi hii.

  Kuala Lumpur, Malaysia

  Ubalozi umeshindwa kulipa ankara za umeme, maji, gesi, simu na matibabu hadi kufikia hatua ya kukatiwa huduma hizo. Maafisa wa ubalozi wameanza kujilipia ankara hizo bila kurejeshewa. Pia katika kile kinachoonyesha kuwa aibu kwa taifa, ubalozi umeshindwa kulipa deni la kampuni ya ulinzi hadi ukaandikiwa barua na wakili wa kampuni hiyo inayotaka kuushitaki ubalozi mahakamani kwa kulimbikiza deni.

  New Delhi, India

  Mbali na hati za utambulisho kwa nchi ambazo Balozi wa Tanzania nchini India analiwakilisha taifa, kuna tatizo la mawasiliano duni kati ya Ubalozi na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Majengo ya kisasa ya ubalozi yaliyoanza kutumika mwaka 2007 hadi sasa hayajatengewa fedha kwa ajili ya kuyafanyia ukarabati kwa miaka mitatu mfulululizo. Kamati imependekeza ubalozi uwezeshwe kifedha.

  London, Uingereza

  Mbali na kucheleweshwa kwa kibali cha kutumia fedha zinazotokana na mauzo ya viza, ubalozi una kiwanja Na. 19 Denewood Road, N64AQ kilichotelekezwa katikati ya Jiji la London. "Sasa hivi Serikali ya Uingereza inaweza kukichukua kiwanja hicho, kwani kinahatarisha usalama wa wananchi wa eneo husika kwa jumla," inasema taarifa hiyo. Pia Serikali imetakiwa kufanyia matengenezo nyumba Na. 6 Colindeep Gardens, NW4 4RU ambayo nayo imetelekezwa kwa sasa haitumiki kabisa.

  Berlin, Ujerumani

  Mwakani meli ya mv Liemba inayofanya kazi katika Ziwa Tanganyika inatimiza miaka 100. Ujerumani imejitolea kuikarabati, lakini haipati mwitikio wowote kutoka Tanzania, hali inayowakatisha tamaa kuwa huenda Tanzania haihitaji msaada huo. La kushangaza hata kiwanda cha saruji cha Wazo Hill kimejitolea kutoa msaada wa euro milioni 2.5 kwa ajili ya ukarabati wa meli hiyo, lakini Serikali imeukataa msaada huu.

  Moscow, Urusi

  Ofisi na nyumba ya Balozi wa Tanzania vipo katika jengo la Serikali ya Urusi lililojengwa mwaka 1886. Tanzania ilianza kutumia jengo hili mwaka 1964 na hadi leo halijawahi kufanyiwa ukarabati. Ubalozi unadaiwa deni kubwa la pango katika jengo hili. "Kwa sababu hiyo hali ya jengo ni mbaya sana kiasi kwamba ilitokea katika Ofisi ya Ubalozi, udongo wa dari (concrete) wenye uzito wa nusu tani ulianguka ofisini kwa balozi na kuacha nondo zote zikiwa wazi," inasema taarifa hii. Pendekezo la ubalozi ni kununua jengo lililopo jirani na ubalozi lenye ghorofa sita kwa wastani wa dola milioni 10 (sh bilioni 16), ambalo wao watatumia ghorofa mbili na nyingine kupangishwa.


  ---
  Nukuu kutoka kwenye gazeti la JAMHURI
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Tungaraza Jr, ulichoandika ni "facts"; baada ya wewe kuzipitia nini maoni yako? Tuache kujenga barabara tuboreshe hadhi za balozi zetu au tuendelee kuwakopa walimu na madaktari ili wafanyakazi wa balozi waishi kifahari? Mimi kwa maone yangu kuna haja ya kupunguza balozi zetu. Badala ya kuwa na balozi kwa kila nchi inayotumia sarafu ya Euro, tunaweza kuwa na ofisi moja katika makao makuu EU; Canada na USA tunaweza kuwa na ofisi moja; Bara la Amerika ya kusini tukawa na ofisi moja. Nchi za Afrika ya Mashariki hakuna haja ya kuwa na ubalozi kwani masuala yote ya Kidiplomasia yanaweza fanyika kupitia East Africa Community.

  Kuhusumu kumiliki majengo, umesema kiasi kinacholipwa lakini hukusema gharama (running costs) za kumiliki majengo + gharama ya kununua jengo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ni aibu sana kwa Tanzania.

  Nilipata pale Ottawa kwenye ubalozi wetu kwa nje yaani utafikiri nyumba ambayo imetelekezwa miaka mingi iliyopita.

  Halafu cha kufadhaisha zaidi ni kwamba sehemu hiyo ina balozi nyingi za Afrika zimekaa sehemu moja ukisogea mbele kidogo kuna ubalozi wa kenya ambao unamiliki jengo kubwa zuri.

  Mimi naona hizi balozi nyingine tuzifunge tu.
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mkuu Maundumula nenda pale wizara ya uchukuzi ukaone jinsi ofisi ilivyominywa na Vi "partition"; kama wanaoteuliwa wanatoka kwenye viofisi vya aina hiyo watapata wapi mawazo ya kuboresha ofisi huko ughaibuni?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We need to understand the concepts of Costs sir! Kwa maoni uliotoa ni haki kabisa kua na ubalozi katika nchi ambazo ni very potential to us kwa kuweka wazi kua Botwana, namibia, Swaz zote ubalozi husika ni ule utakakua na makao makuu SA. Huu ni mfano tu bro.

  Ila wale ndugu na jamaa zao, wanajeshi waliostaafu, marafiki wa shule na wabunge alioshindwa katika chaguzi (James Msekela-Italy). Hii NDIO HOFU KWAO kama kweli cost is on the tips of their fingures.
   
 6. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hebu fananisha na ule wa BANGLADESH ulioko Tanzania, that is the image of Tanzania abroad rit?
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Imagine Mzungu ambaye yupo huko nje anafikiria between kuitembelea Tanzania au Kenya ameambiwa nchi zote mbili ukiwepo unaweza kufika Serengeti au Kilimanjaro. Anaenda kwenye ofisi za ubalozi zote mbili kuomba maelezo ya Visa. Obviously hawezi kuja bongo.
   
 8. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na ndio maana wengi hutua Kenya ili kuupanda Mlima Kilimanjaro. Sasa napata picha na kwa nini budget ni 70% reccurent expenditure. Inaelekea wapi sasa?
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  wanasubiri watoto wao wamalize shule za kuunga unga huku ughaibuni ndio wakashike nafasi hizo........halafu ndio pesa zitumwe kikamilifu....damn!
   
 10. m

  mamajack JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  nani alaumiwe?????
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  wizara ya mambo ya nje iko wapi???
   
 12. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Eti...mishahara yao huko 'balozini' ni kama ya kwetu huku?
   
 13. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Atakua mpuuzi mzungu huyo,maana info zote zipo online na pia kuna mawakala mbali mbali wanao toa recomm.. kwa watalii,So hiyo sio issue, serekali inavitu vya muhimu ambavyo inahitaji kuvikamilisha kwa sasa kabla hata ya kukimbilia huku na kuja kuwapa wala fedha za umma mapango ya kujificha.
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Seeing is believing, mtu anaishi Ottawa down town 10 minutes walk aanze kuhangaika wakati ubalozi upo hapo hapo mjini. Sidhani kama Tanzania inatoa Visa online.
   
 15. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hizo balozi zina kazi gani hasa zaidi ya kuendeleza uwizi wa wakubwa?

  zifungwe tu hazina tofauti na wakuu wa wilaya na mikoa
   
 16. e

  enos Member

  #16
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi kweli kweli jamani,balozi ambazo hazina tija na maslahi kwa taifa hili zifungwe kwani ni hasara kuziendesha ukilinganisha na faida tunayopata kutoka mataifa hayo.
   
Loading...