ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Wadau wa zilipendwa Naomba msaada wa nyimbo ya vijana jazz mistari yake inaimba (badili mwenendo wako unaweza kukualibia maisha yako hali ya sasa ningumu ungelewa)
 
Huu wimbo unanitesa miaka mingi nahisi muimbaji anaweza kuwa mafumu bilali au baba yake banana. Maneno yanasema

Hata wanifunge jela saizi yangu
Hata wani...... Saizi yangu
Wale wanaogombana, ndiyo wanaopatana


Mwingine
Kula kwake vichochoroni,kulala kwake vichochoroni,usikumbatie vichochoroni, kuna vibaka wengi sana....


Aaahhh.... Kuchoma choma kubaya, utamchoma.mkweo aliyekuzalia mkeo....
 
Nanreen......Eddy(mtoto wa Tambaza almaarufu kama msomi wa Tambaza huyu) kwa kweli alikuwa anavutia hasa,alikuwa ana sauti ya kipekee kabisa,sikiliza nyimbo alizoimba kama Wivu,Mwisho wa mwezi,Ngapulila(Vijana Jazz), Julie,Nelson Mandela,Yaliyopita si ndwele(Washirika Tanzania Stars), Shakaza(Bima Lee Orch), Milima ya kwetu(Super Rainbow), Ngondoigwe,Baba Jane(Bantu Group) utagundua ni kwa nini nasema Eddy Sheggy 'Mzee Shakaza'(R.I.P) alikuwa na sauti ya kipekee........Japo wadogo zake Francis na Christian Sheggy walijaribu kumuiga,hawakuweza.....Jamaa alikuwa sayari nyingine kabisa.......

Hebu angalia kitu hiki ulichokiomba ambacho Eddy alikitunga na kukiimba akiwa na Super Rainbow,aliimba kwa kushirikiana na Nanah Njige.....Kitu Milima ya kwetu...

Milima ya Kwetu

Nikitazama milima ya kwetu ee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo,
tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
baba na mama wataniuliza bibi yako yuko wapi ee,
Ndugu jamaa wataniuliza bibi yako yuko wapi eee,

japokuwa ninakaribia kufika nyumbani ee,
Ninatamani gari isifikie upeesi,
kwa ile aibu nitakayopata mbele ya wazazi ii,
kwa vile ni miezi michache imepita nilitoka na bibi yangu,

(Eddy)
Nitasema nini kwa baba mimi najuta aa,
kwa pesa zake nyiingi alizopotezaa,
harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana,
watu walikula na kunywa na kusaza mamaa,

Nikaenda kuishi na bibi yule mjini,
kazi yake ilikuwa ni vituko,
nikaenda kuishi na bibi yule mjini kazi yake ilikuwa ni vitiimbwi,

Alianza kuweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa,

kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai,
nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,

kafuatia kuchelewa akienda sokoni,
nikimuuliza anitukana hadharani aibu,

kuna gari imekuja hadi mlangoni,
kujitetea akasema mjomba wake kaja,

hivi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani,

hatimaye kunibeza na kunidharau,
shikamoo ikaisha ikabaki
Vipi babu, mambo zakoo ee x2

Nilishindwa kumuuliza ee sikutaka kumuudhi,
sababu nilikuwa nampenda nampenda saana x 2

chorus:

walisemaa dalili ya mvua ni mawingu,
niliyempenda kanitoroka mama,

(Eddy Sheggy)
Nilinyang'anywa tonge mdomoni,
nilinyang'anywa tonge kinywani,
niliyempenda kanikimbia mama yoyo,
niliempenda kanikimbia masikini nifanye nini mama,

(chorus)

Vituko ee, vituko vya bibi huyoo,
sitaweza kusahau mimi oo mama ee,
sitaweza kusahau mimi oo sheggy ee,
alikuwa kama helikopta, ndege isiyochagua mahali pa kutua ee,
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oo,
ana bwana mmoja ama wawili mama mama oo,
nifanye nini mama oo,
 
Huu uzi bendi zetu hizi haupo kweli telegram?Kama vipi ingekuwepo huko telegram ili wenye Nyimbo hizo wazitupie tunufaike wote.
 
Katika hali yoyotee kareni kwa amani na wahusiaa mpaka kifo kijeni watengenishaaa....

Naombeni jina la huu wimbo
 
Back
Top Bottom