Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....
Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.......
Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba,Hekaheka,Heka koka,Watoto wa nyumbani,Air Pambamoto(awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.....
Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa......Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku,Mary Maria,Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto,Adza(Aza),Ngapulila,Ogopa Tapeli,Mwisho wa Mwezi,Penzi haligawanyiki,Wivu,Malaine,Nyongise,Shoga,Theresa,V.I.P,Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu....
Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku',Hamza Kalala 'Komando',Manitu Mussa,Issa Chikupele,Hassan Dalali,Hassan Shaw,Ally Jamwaka,Abuu Semhando,Bakari 'Baker' Semhando,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya zege',Eddy Sheggy,Shaban Yohana 'Wanted',Rashid Pembe 'Profesa',Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo,John Kitime,Abdallah Mgonahazelu,Freddy Benjamin,Mohammed Gotagota,Said Hamis 'Misukosuko',Athumani Momba na wengine kibao...
Habari zaidi, soma=>Mashairi ya Kiswahili ya Nyimbo zote za Maquis du Zaire
Vijana wanajua nini kuhusu ZilipendwaWatoto haelewi haya mambo!
Wakuu kwema?
Ebana kuna wimbo wa Sikinde kiitikio chake wanasema “kwa kauli yangu ya ukiwa siwalaumu enyi wakwe”
Mwenye kuujua jina lake au mwenye nao please yamenikuta mkongwe mwenzenu nauomba tafadhali
mwenye nyimbo ya mafumo bilal-mungu aliumba neno mapendo naiyomba nimeitafuta bila mafanikio
Wimbo unaitwa THERESA ulipigwa na kuimbwa na Vijana Jazz Band wana Air Pambamoto Awamu ya Pili..Samahani kuna wimbo wenye maneno...ni penzi gani alilokupa huyoo na kuchanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusiii...unaitwaje na ninaweza kuupata?
Samahani kuna wimbo wenye maneno...ni penzi gani alilokupa huyoo na kuchanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusiii...unaitwaje na ninaweza kuupata?
Wimbo unaitwa THERESA ulipigwa na kuimbwa na Vijana Jazz Band wana Air Pambamoto Awamu ya Pili..
Jamani mimi binafsi naombeni mwenye wimbo wa Edina by Magereza Jazz afanye kuutuma kwa njia yoyote anayoona itafaa, .....