ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Song : Safari by AY- feat King Kikii Kikumbi Mwanza

Tanzanian singer and actor, Ambwene Yesaya a.k.a AY is back on the grind with a new song titled “Safari” and he collaborated with the amazing singer, King Kikii Kikumbi Mwanza Mpango



Source: AyTanzania
 
Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....

Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.......

Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba,Hekaheka,Heka koka,Watoto wa nyumbani,Air Pambamoto(awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.....

Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa......Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku,Mary Maria,Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto,Adza(Aza),Ngapulila,Ogopa Tapeli,Mwisho wa Mwezi,Penzi haligawanyiki,Wivu,Malaine,Nyongise,Shoga,Theresa,V.I.P,Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu....

Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku',Hamza Kalala 'Komando',Manitu Mussa,Issa Chikupele,Hassan Dalali,Hassan Shaw,Ally Jamwaka,Abuu Semhando,Bakari 'Baker' Semhando,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya zege',Eddy Sheggy,Shaban Yohana 'Wanted',Rashid Pembe 'Profesa',Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo,John Kitime,Abdallah Mgonahazelu,Freddy Benjamin,Mohammed Gotagota,Said Hamis 'Misukosuko',Athumani Momba na wengine kibao...

Habari zaidi, soma=>Mashairi ya Kiswahili ya Nyimbo zote za Maquis du Zaire
 
Japo wametimiza ivyo lakini nakataa ahadi yaooo ya kuninyima ata tone la maji wakati nina kiu.....
 
Sito weza wasahau BIMA LEE hasa kile KIBAO cha BILIONEA WA MAPENZI

KWA WALE WAHENGA WENZANGU TUU
MNA KUMBUKA HIKI KIBAO????

nikwelewejeee,
Nikwite nani weweeeee,

Nikwite bwana mapenzi hilo jina halikufai ,

Nikwite bwana mapenzi hilo jina halikugaiiiiii,

Naona bora Nikwite Bilionea wa mapenziiii. *2

Ume tuweka ndani sisi wanawake watatuuuu,

Khanga na kitenge sisi kwetu ni ndoto,

Michele wa kitumbo sisi kwetu ALMASIIII.

Nusu kilo ya sukari utaigawa vipi mara TATUUU

hahahahahahahahahaaa khaaa Zamani raha Sana aisee

Sisi Wazee bwana Hebu tupambane turudishe mziki wetu
 
Naomba link ya kudownload wimbo wa Zumbukuku (Fikiria Dunia) wa DDC Mlimani

Pia nikipata Gere wa DDC pia itakua vizuri
 
Nimeguswa na hisia za Mzee Pembe,Vijana Jazz ikiwa iko moto kweli kweli,ndo hivyo zimebaki stori!
Ila sikumpata vizuri,mbona miaka ya 1996/97,Vijana Jazz walitoa Album iliyo hit(Tafrija la Kuuaga Umaskini-Umaskini bye bye) ambapo ilifanya vizuri tu. Naona anguko la Dansi lilianza miaka ya 1999 kuja hadi 2000. Baada ya hapo ilikuja Dansi mpya ya Twanga Pepeta miaka hiyo ya 1999-2006!Twanga,Muungano,TOT,Tam Tam na FM Academia,Beta Musica,Extra Bongo na Dar Musica. Hata hivyo nazo zinaelekea kufutika.
Dar musica ya nani ilkuwa
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom