patrick80
JF-Expert Member
- Sep 7, 2017
- 737
- 607
Vizuri sana mkuu.Kalubandika unaujua??
Vizuri sana mkuu.Kalubandika unaujua??
Hawa ni Jamhuri JazzHalafu kuna ule wimbo sijui kaimba nani?mashairi yake;
Aeeee Maria eee bembeleza mwana mamaaaa,msitu mkubwa tutaliwa na simbaaa.....
Huu wimbo nimeusaka kila mahali nimeukosa. Kuna mahali mdau aliniwekea wimbo wa Vijana Jazz uitwao -Kapu la Mjanja- Hizi nyimbo kuna mambo fulani nikizisikia huwa kuna kumbukumbu fulan ambazo hunipa hisia kali sana. Kama mkuu Balantanda au mdau yeyote ataweza kuniwekea nitashukuru sana.Wakati UDA Jazz wanatamba Ally Choki alikuwa mtoto mdogo sana mkuu,sema UDA Jazz imepitiwa na mwalimu(baba wa muziki) wa Ally Choki Komando Hamza Kalala...
Bantu Group Band ndiyo imemtoa Ally Choki japo kuna taarifa kwamba aliwahi pia kupitia bendi ya Lola Afrika ya Profesa Vulata...
Sikiliza kibao cha Baba Jane na 1 cha Bantu Group utamsikia Ally Choki kwenye kiitikio 'Mimi ooooo(mimi oooooh) Baba Jane bye bye, bado nakupenda mume wangu,baba Jane bye bye, narudi nyumbani baba Jane,baba Jane bye bye, narudi kwa baba na mama,baba Jane bye bye"......Hapo Choki ndio kwanza alikuwa anaanza kusikika katika anga za muziki wa kibongo
Daaaaa,ni shida. Siku hizi jaman vipaji viko wapi?Nico Zengekala(R.I.P) pamoja na kilema chake cha upofu alikuwa habari nyingine mkuu,angalia mashairi ya nyimbo hizi utaona maana ya ninachokisema ama ulichokisema wewe hapo juu...
Jackie...
Mtoto Jackiee,mtoto wa Nirobi
Ingawa ni mara ya kwanza mimi nawe Jackiee
Tulipokutana palee Kampala kwenda Nairobi
Tulifurahiana sana kama tuliishi mwaka
Tabia yako njema kweli sitoisahau.
Mtotoo Jackie,mtoto wa mama Jackie wa mapendo
Japokuwa tuliachana stendi ukielekea Nairobi nyumbani eeh
Lakini tutakutana,nitakuja kutembelea,nawe karibu nyumbani eeh
Ooh Jackie yeyeeeh
Mtoto wa mama Jackie wa mapendo
Japokuwa tuliachana stendi,ukielekea Nairobi nyumbani eeh
LAkini tutakutana,nitakuja kutembelea,nawe karibu nyumbani eeh
Ooh Jackie yeyeeeh
Kiitikio:
Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau lakini nashindwa
Hasa ni ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU
Nimejaribu kukusahau lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua eeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU
Sauti yako nyororo inaniua sana na mwendo wako wa maringo unanikondesha mamaaah,ayoleli mwanamama nakuwinda sana Jackie yeyeyeeeh mwanamamaah aeaeeh
Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU
Mvumilivu hula mbivu,Jacki yeyeeeh,mvumilivu hula mbivu Jackie yeyeeeh
Jaribu kuvumilia yeeh tutaonana mamaah kama sio Kampala ni Tanzania mamaa
Jackie yeyeyeeh mwanamama aeaeeh
Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Nitakuja Nairobi eeh nikuone mamaah
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Tutafurahi pamoja mi na wewe mama yeeh
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Jackie yeyeyeeh Maneno sema na yeye
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
ama kitu Solemba
Solemba solemba solemba aaaaaaaaaah
Sitakuwa nikifika nyumbani kwako,aibu nilopata ni kubwa sana,
Ahadi nilopewa ilivunjwa oooh ooooh hata bila kosa,
Ulinipa ahadi tukutane kwenu,nikitumaini nimewahi,
Nilichopata kwako ni matusi oooh ooh na dharau tele,
Ungenieleza ukweli Solemba,kuliko kunidanganya ooh,
Najuta kuitimiza ahadi oooh ambayo si ya kweli,
Ungenieleza ukweli Solemba,kuliko kunidanganya ooh,
Najuta kuitimiza ahadi oooh ambayo si ya kweli,
Bridge

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba
Zengekala: Ulinikana mbele za watu ati hunifahamu,
Ndugu zako na marafiki walianza kutoka nje,
Waliponiona ni mimi,walishangaa sana mama,
Mbona hivyo solemba mama eee
(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba
Zengekala: Nilikuuliza mbona ulinitendea hivyo Solemba,
Ulisema mimi hujipendekeza kwako tena sana,
Na kuwa hunipendi,nakusumbua bure mamaa,
Mola yupo Solemba,Eloi yupo mamaa.
(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba
Zengekala: Nilichomwa na jua toka asubuhi,
mpaka saa nane Solemba,Sababu ya kukungoja wewe
Kumbe ulikuwa ndani,unachungulia dirishani,
Huna huruma Solemba,I shall never forget you mamaa,
(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba
Zengekala: Sikutaki tena,sina haja nawe,
Nimeshapata mwingine anayenipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakayembabaisha kama mimi,
Nimeshituka Solemba,nimeshituka solemba.
(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba
Zengekala: Lalala lalala lalala lalalalala
Nimeshapata mwingine anayenipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakayembabaisha kama mimi,
Nimeshituka Solemba,lololo lolololo mama lo
(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba
Duh, aiseee! Ni hicho kikunio ndio kinanifikirisha. Walitumia nini kuutenda huo ukunaji?Tukunyema walikuwa wananikuna sana
KipapatunduDuh, aiseee! Ni hicho kikunio ndio kinanifikirisha. Walitumia nini kuutenda huo ukunaji?
Hakika huo ukunwaji ulikufikisha kunako!Kipapatundu