ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,752
Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....

Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.

Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba, Hekaheka, Heka koka, Watoto wa nyumbani, Air Pambamoto (awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.

Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa. Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku, Mary Maria, Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto, Adza(Aza), Ngapulila, Ogopa Tapeli, Mwisho wa Mwezi, Penzi haligawanyiki,Wivu, Malaine, Nyongise, Shoga,Theresa, V.I.P, Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu.

Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku', Hamza Kalala 'Komando', Manitu Mussa, Issa Chikupele, Hassan Dalali, Hassan Shaw, Ally Jamwaka, Abuu Semhando, Bakari 'Baker' Semhando, Mhina Panduka 'Toto Tundu', Adam Bakari 'Sauti ya zege', Eddy Sheggy, Shaban Yohana 'Wanted', Rashid Pembe 'Profesa', Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo, John Kitime, Abdallah Mgonahazelu, Freddy Benjamin, Mohammed Gotagota, Said Hamis 'Misukosuko', Athumani Momba na wengine kibao.

Habari zaidi, soma=>Mashairi ya Kiswahili ya Nyimbo zote za Maquis du Zaire
 
Pia kuna Washirika Tanzania Stars Band.....

Bendi hii ilikuwa ikimilikiwa na Jumuiya ya Washirika Tanzania na iliundwa na wanamuziki wengi waliojiengua kutoka Orchestra Vijana Jazz,iliundwa mwaka 1989 na ilikuwa ikitumia mtindo wa Watunjatanjata(Watanzania tuondoe njaa Tanzania) na baadae wakajiita Njata one....

Bendi hii ilikuwa ikifanya maonesho yake katika ukumbi wa 92 Hotel pale Sinza Shekilango...Ilikuwa ni bendi kali hasa na ilikuwa ni tishio kwa bendi zilizotamba enzi zake hasa Vijana Jazz...

Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Yaliyopita si ndwele(Nimekusamehe lakini sitokusahau),Washirika,Nelson Mandela,Julie,Penzi la ulaghai,Nimebaki nashangaa,Spare tyre,Maeliza,Gubu la wifi zako,Zuhura,Umbea,Watoto wamekuja juu,Masumanda,Kissa,Kayumba na nyingine kali....

Bendi hii iliundwa na wanamuziki wengi waliojiondo Vijana Jazz kama Hamza Kalala 'Komando',Eddy Sheggy,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya Zege' bila kuwasahau Abdul Salvador 'Father Kidevu',Emma Mkelo 'Lady Champion',Robert Mabrish,Zahir Ally Zorro,Madaraka Morris 'Kiwembe' ,

Baadae mwaka 1991 baadhi ya wanamuziki wakiongozwa na Hamza Kalala na Eddy Sheggy na kwenda kuunda bendi mbili tofauti za Bantu Group Band(wana Kasimbagu Kahabuka) na MCA International(wana Munisandesa) na wengine(Eddy Sheggy na wenzake) walihamia Bima Lee Orch. wana Magnet Tingisha.....Hiii iliifanya Watunjatanjata itetereke kidogo hadi mwaka 1992 ilipompata mtaalam Zahir Ally Zorry ambaye aliifanya ikabaki imara na mtindo wa Watunjatanjata waliouboresha na kuwa Njata One wakiwa na nyimbo kama Gubu la Wifi zako,Maeliza,Zuhura na Umbea
 
Haaa Bala umeturudisha kwenye mambo yetu yaleeeee,
Vijana walikuwa machachari na ndio walikuwa bendi neutral ya wapinzani wa Jadi DDC na Msondo
Umenikumbusha Dudumizi mtaalamu wa nyimbo za mapenzi

Jamaa(Jerry Nashon Dudumizi) alikuwa mtunzi kwelikweli wa nyimbo za mapenzi hasa akiwa na Bima Lee na Vijana Jazz...

Angalia kama kitu hiki kitamu hapa chini ambacho ni utunzi wake..

V.I.P-Jerry Nashon 'Dudumizi"


(Wote): Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo,

(Dudumizi): Si maji wala Soda vitakavyozima kiu yangu,ila ni wewe VIP,
Si maji wala Soda vitakavyozima kiu yanguuu,iila ni weweeeee,VIP
Baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa,na kisirani cha kufokewa na boss,
Nahitaji VIP wa kunibembeleza,nakutaka wewe mama,unibembeleze,
Si kwa maneno ila kunitomasatomasa,kwa mikono yako laini yenye bangili,
Unipe busu mwanana la kunipumbaza wee (VIP).

Baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa,na kisirani cha kufokewa na boss,
Nahitaji VIP wa kunibembeleza,nakutaka wewe mama,unibembeleze,
Si kwa maneno ila kunitomasatomasa,kwa mikono yako laini yenye bangili,
Unipe busu mwanana la kunipumbaza wee (VIP)

(Wote): Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo,
Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo.

Dudumizi: VIP sogea karibu,ubipe busu mwanana mama

(Wote): Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo,

Bridge

(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.
Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka


Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP,
Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP
Natamani penzi live sio penzi la ndotoni,nakuomba uwe wangu VIP,
Tafadhali nakusihi, ili niondokane na ndoto za mapenzi.

(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.
Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka


Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP,
Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP
Natamani penzi live sio penzi la ndotoni,nakuomba uwe wangu VIP,
Tafadhali nakusihi, maaa mamaa,maaa....maaa yoooo,maa mamamaaaaaaaaaaaaaaa,
Tafadhali nakusihi, ili niondokane na ndoto za mapenzi.


Dudumizi: Ukinikubali VIP,mimi niko tayari,kubadili dini,
Ukinikubaliii VIP mimi niko tayari,kubadili dini,
Hata kama wazazi wangu hawapendi,nitafanyafanya mipango niwe na wewe sambamba(sambamba)
nitafanyafanya mipango niwe nawee sambambaaa

(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.


Ukinikubalii VIP,mimi niko tayari kubadili dini,
Ukinikubalii VIP,nitatoa mahaliii ya mbuzi saba,
Hata kama sina VIP,nitafanyafanya mipango niwe na wewe sambamba(sambamba) nitafanyafanya mipango niwe na wewe
sambamba.

(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.
 
Halafu walikuwepo MK Groups watoto wa Maghorofani(New Afica hotel) wana Ngulupa tupatupa Dansi chini ya uongozi wake Kasongo Mpinda 'Clayton',hawa jamaa walikuwa wanatisha sana sikiliza nyimbo zao kama Nishike mkono,Mariam Mary,ama ule 'Kibela acha chuki,chuki yaleta ugomvi,Kibela acha chuki,chuki yaleta migonganoo,ooh ooh Kibela' na nyingine.

Bila kuwasahau MK Beats wana Tukunyema(mpaka chini mpaka chini) chini ya uongozi wake mzee Shem ibrahim Kalenga akiwa na vijana wake akina Malick Star na Sisco Lunanga (waliondoka MK Beats hawa wakaenda kuanzisha Lulu Band ya Kanda Bongo Man iliyokuwa na makazi yake pale La Prima Victoria chini ya uongozi wake Connie Karanja)..Enzi hizo ilikuwa ni mambo ya Tukunyema tu,wowowo.


Tucheze wote ooh tuche wote tukunyema aah tukunyema wa Tabora ooh tucheze wote Tukunyema aah...Au Tukunyema tukunyema mpaka chini mpaka choniii, wowowoooo Mambo ya Belaombwe..dah,si mchezo yaani.

Mnayakumbuka mambo ya Mzee Kistuli na wowowo?
 
Balantanda!
Naona umemtaja sana Eddie Sheggy, lakini hujagusia alipokuwa SUPER RAINBOW. Hebu lete shule zaidi.

Nanreen......Eddy(mtoto wa Tambaza almaarufu kama msomi wa Tambaza huyu) kwa kweli alikuwa anavutia hasa,alikuwa ana sauti ya kipekee kabisa,sikiliza nyimbo alizoimba kama Wivu,Mwisho wa mwezi,Ngapulila(Vijana Jazz), Julie,Nelson Mandela,Yaliyopita si ndwele(Washirika Tanzania Stars), Shakaza(Bima Lee Orch), Milima ya kwetu(Super Rainbow), Ngondoigwe,Baba Jane(Bantu Group) utagundua ni kwa nini nasema Eddy Sheggy 'Mzee Shakaza'(R.I.P) alikuwa na sauti ya kipekee........Japo wadogo zake Francis na Christian Sheggy walijaribu kumuiga,hawakuweza.....Jamaa alikuwa sayari nyingine kabisa.......

Hebu angalia kitu hiki ulichokiomba ambacho Eddy alikitunga na kukiimba akiwa na Super Rainbow,aliimba kwa kushirikiana na Nanah Njige.....Kitu Milima ya kwetu...

Milima ya Kwetu

Nikitazama milima ya kwetu ee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo,
tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
baba na mama wataniuliza bibi yako yuko wapi ee,
Ndugu jamaa wataniuliza bibi yako yuko wapi eee,

japokuwa ninakaribia kufika nyumbani ee,
Ninatamani gari isifikie upeesi,
kwa ile aibu nitakayopata mbele ya wazazi ii,
kwa vile ni miezi michache imepita nilitoka na bibi yangu,

(Eddy)
Nitasema nini kwa baba mimi najuta aa,
kwa pesa zake nyiingi alizopotezaa,
harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana,
watu walikula na kunywa na kusaza mamaa,

Nikaenda kuishi na bibi yule mjini,
kazi yake ilikuwa ni vituko,
nikaenda kuishi na bibi yule mjini kazi yake ilikuwa ni vitiimbwi,

Alianza kuweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa,

kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai,
nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,

kafuatia kuchelewa akienda sokoni,
nikimuuliza anitukana hadharani aibu,

kuna gari imekuja hadi mlangoni,
kujitetea akasema mjomba wake kaja,

hivi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani,

hatimaye kunibeza na kunidharau,
shikamoo ikaisha ikabaki
Vipi babu, mambo zakoo ee x2

Nilishindwa kumuuliza ee sikutaka kumuudhi,
sababu nilikuwa nampenda nampenda saana x 2

chorus:

walisemaa dalili ya mvua ni mawingu,
niliyempenda kanitoroka mama,

(Eddy Sheggy)
Nilinyang'anywa tonge mdomoni,
nilinyang'anywa tonge kinywani,
niliyempenda kanikimbia mama yoyo,
niliempenda kanikimbia masikini nifanye nini mama,

(chorus)

Vituko ee, vituko vya bibi huyoo,
sitaweza kusahau mimi oo mama ee,
sitaweza kusahau mimi oo sheggy ee,
alikuwa kama helikopta, ndege isiyochagua mahali pa kutua ee,
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oo,
ana bwana mmoja ama wawili mama mama oo,
nifanye nini mama oo,
 
Mama - Tancut Almasi Orchestra

Hii Band ya Tancut Almsi kwa kweli................ Bado naitafuta Album nzima yenye wimbo huu wa mama.

Balantanda bado naisubiri maana uliniahidi kunitafutia nyimbo ORIGINAL za hawa mapacha wa Kikongo.

Ukitaka kusikiliza, basi pitia hapa: Wanamuziki wa Tanzania :: Music - ReverbNation
 
Tukunyema walikuwa wananikuna sana

Hao nao walikuwa wanatisha aisee......

'Kinababa amkeni,kina mama amkeni(kwa nini), tucheze tukunyema tukunyema,tukunyema,mpaka chini mpaka chini,wowowoooooooooo'

Ilikuwa raha sana yaani,mzee Shem Ibrahim Kalenga na vijana wake Malick Star na Sisco Lunanga...

Btw......Unamkumbuka mzee Kistuli?(andunje anapanda kwenye stuli ndo analifikia wowowo)
 
Mama - Tancut Almasi Orchestra

Hii Band ya Tancut Almsi kwa kweli................ Bado naitafuta Album nzima yenye wimbo huu wa mama.

Balantanda bado naisubiri maana uliniahidi kunitafutia nyimbo ORIGINAL za hawa mapacha wa Kikongo.

Ukitaka kusikiliza, basi pitia hapa: Wanamuziki wa Tanzania :: Music - ReverbNation

Hahaaaaaaaaa,nimekusoma Home boy,nitafanya utaratibu wa kukutumia,shaka ondoa Nkwingwa...
 
Pia ilikuwepo bendi ya Tancut Almasi,bendi hii ilikuwa inamilikiwa na kiwanda cha kukata almasi kilichokuwa mkoani Iringa na ilikuwa ni mojawapo ya bendi za mikoani zilizokuwa na makali kweli(kama jirani zao wa JKT Mafinga wana Kimulimuli chini ya Zahir Ally Zorro na Kurugenzi ya Arusha).....Tancut Almasi walikuwa wakitumia mtindo wa Fimbo Lugoda na Kinye kinye Kisonzo,tisa kumi Mangala.......

Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Samahani ya uongo,Pili wangu,Butinini,Ngoma za Afrika,Helena mtoto wa Arusha,Masikitiko,Lutandila,Safari siyo kifo na nyingine nyingi tu tamu...

Bendi hii iliundwa na wanamuziki kama Kalala Mbwembwe,Nanah Njige,Nuru Mhina,Kawalee Mutimwana,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Mafumu Bilali 'Bombenga',Shaban Yohana 'Wanted',John Kitime,Akuliake Saleh 'King Maluu',Ray Mlangwa,Mohammed Shaweji,Kibambe Ramadhan,Bakari Buhero,Bdul Mngatwa,Hashim Kassanga na wengine wengi......Bendi hii ilikuwa na hazina ya vipaji kwa kweli.......

Bendi hii ilitamba sana kabla ya kuanza kusambaratika baada ya wanamuziki wake tegemeo akiwemo Kalala Mbwembwe,Kyanga Songa na Kasaloo Kyanga kuanzisha bendi nyingine hapohapo Iringa ya Ruaha International ambayo ilitamba sana na wimbo wa Lutandila namba 2 Safari (Safari safari safari kweli tabu,naomba kwa Mungu baba nifike salama,safari yangu mieee,safari ya Zimbabweee............ulikuwa wimbo mtamu kweli jamani).....
 
Pia ilikuwepo bendi ya Tancut Almasi,bendi hii ilikuwa inamilikiwa na kiwanda cha kukata almasi kilichokuwa mkoani Iringa na ilikuwa ni mojawapo ya bendi za mikoani zilizokuwa na makali kweli(kama jirani zao wa JKT Mafinga wana Kimulimuli chini ya Zahir Ally Zorro na Kurugenzi ya Arusha).....Tancut Almasi walikuwa wakitumia mtindo wa Fimbo Lugoda na Kinye kinye Kisonzo,tisa kumi Mangala.......

Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Samahani ya uongo,Pili wangu,Butinini,Ngoma za Afrika,Helena mtoto wa Arusha,Masikitiko,Lutandila,Safari siyo kifo na nyingine nyingi tu tamu...

Bendi hii iliundwa na wanamuziki kama Kalala Mbwembwe,Nanah Njige,Nuru Mhina,Kawalee Mutimwana,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Mafumu Bilali 'Bombenga',Shaban Yohana 'Wanted',John Kitime,Akuliake Saleh 'King Maluu',Ray Mlangwa,Mohammed Shaweji,Kibambe Ramadhan,Bakari Buhero,Bdul Mngatwa,Hashim Kassanga na wengine wengi......Bendi hii ilikuwa na hazina ya vipaji kwa kweli.......

Bendi hii ilitamba sana kabla ya kuanza kusambaratika baada ya wanamuziki wake tegemeo akiwemo Kalala Mbwembwe,Kyanga Songa na Kasaloo Kyanga kuanzisha bendi nyingine hapohapo Iringa ya Ruaha International ambayo ilitamba sana na wimbo wa Lutandila namba 2 Safari (Safari safari safari kweli tabu,naomba kwa Mungu baba nifike salama,safari yangu mieee,safari ya Zimbabweee............ulikuwa wimbo mtamu kweli jamani).....

Angalia kibao kitamu kama hiki cha Tancut Almasi...

Ninakwendaa safari, safari yenyewe safari ya kikazi,

Ninajuaa mama utabakiii, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mamaa watafurahii x 2

Ninakwendaa safari, safari yenyewe safari ya kikazi,

Ninajuaa mama utabakiii, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mamaa watafurahii x 2

Ninakwendaa safari, safari yenyewe ya masafa marefu,

Ninajuaa mama utabakiii, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mamaa watafurahii x 2

Ninakwendaa safari, safari yenyewe ya masafa marefu,

Ninajuaa mama utabakiii, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mamaa watafurahii x 2

Lakini usisikie yaoo mama watoto oo,……………..,

Nakwenda kutafuta maisha ya watoto wetu…………….,

Chunga watoto wetu mamaa nitarudi, tutaonana kwa mapenzi ya Mungu,
Chunga watoto wetu mamaa nitarudi, tutaonana kwa mapenzi ya Mungu,

Safari sio kifoo o mama iyeye,
Subiri nitarudii o mama watoto,
Safari sio kifoo o mama iyeye,
Subiri nitarudii o mama watoto,

Nikirudi mamaa nitakuletea zawadi,
Nikirudi mama nipokee kwa mikono miwili

Iyeye, oo mama iyee,

Nikirudi mamaa nitakuletea zawadi,
Zawadii nono, mama watooto.


(a keba, keba, keba, keba, keba, keba, keba, kebaaa,)
(fimbo, fimbo, fimbo, fimbo, lugoda,lugoda, lugoda, lugoda - Mangalaa..


 
Pia kuna Orch. Marquiz Original,kundi hili liliundwa miaka ya 70 na wanamuziki waliotoka katika jimbo la Shaba nchini Zaire(DRC) waliingia nchini wakiitwa Orchestre Super Gabby,baada ya kuingia nchini walibadilisha jina na kuanza kuitwa Orchestra Maquis du Zaire/Marquis Original.....Mitindo waliyoitumia ni pamoja na Ogelea Piga Mbizi,Zembwela na Sendema.....Ukumbi waliokuwa wakipiga(uwanja wao wa nyumbani) ni Lang'ata Social Hall pale Kinondoni(FM Club ambapo kwa sasa ni kanisa).....Hawa pia walikuwa wanaujua muziki hasa kutokana na aina ya muziki mchanganyiko wa kizaire(kavasha) na vionjo vya kitanzania walivyopiga....

Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana,nyimbo kama Mayanga,Ngalula,Makumbele,Mpenzi Luta,Mpenzi Scola,Karubandika,Seya,Tipwatipwa,Kisabengo,Wakati nilikuwa mdogo,Bi Sofia,Hali ngumu,Ni wewe pekee,Kibulwa,Huba wangu,Mapenzi sio masihara,Wanaume wa leo,Clara,Mayasa,Wema wangu,Double double,Mabruki,Anjelu,Balimwacha,Kazi yangu Baharia,Mapenzi ya pesa na nyingnie nyingi....Hawa jamaa wanaweza kuwa wanaongoza Tanzania kwa kuwa na nyimbo nyingi sana....

Bendi hii imewahi kuwa na wanamuziki kama Tshimanga Kalala Assosa,Issa Nundu,Mukumbule Lulembo 'Parash',Mbuya Makonga 'Adios',Ilunga Banza Mchafu.Dekula Kahanga 'Vumbi',Bobo Sukari,Fredito Butamu,Mbwana Kocks,Kabea Badu,Mutombo Lufungula Audax,Matei Joseph,Kaumba Kalemba,Mukuna Roy,Berry Kankonde,William Maselenge,Seif Said,Nguza Vicking,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Kiniki Kieto na wengine kibao..............

Hakika ya kale ni dhahabu...
 
Mie kulikuwa na bendi nyingi sana ambazo zilikuwa zinanikuna sana baadhi tu ni Msondo, Ngide, Western Jazz, Marquiz, Dar Jazz, Vijana, Jazz na nyingi nyinginezo ambazo kwa kweli muziki wao ulikuwa ni moto wa kuotea mbali kulinganisha na huu muziki wa siku hizi "Bongo Flava" pamoja na kuwa kuna nyimbo chache nzuri lakini mie Mhhhhh! bado haujanigusa kihivyo ukilinganisha na muziki wetu kabla ya Bongo flava.

Sikilizeni hawa jamaa wa kule Tanga walijiita Jamhuri Jazz vibao vyao vilikuwa vitamu sana,
 
Pia kulikuwa na bendi ya Orchestra Safari Sound ambao baadaye walikuja(mwaka 1985) kuitwa International Safari Sound,hawa ni wakali wengine waliotamba sana katika muziki wa Dansi wa Tanzania katika hiyo miaka ya 80 na 90...Bendi hii ilikuwa ikimilikiwa na mfanyabiashara Hugo Kisima.....Bendi hii ilikuwa mara nyingi ikifanya maonesho yake katika ukumbi wa Safari Resort uliopo Kimara.....Bendi hii ilitumia mitinfo ya Dukuduku,Ndekule,Rashikanda wasaa na Power Iranda...

Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana kama ilvyo kwa Orch. Marquiz Original.....Baadhi ya nyimbo zao zilizotamba ni kama Marashi ya Pemba,Mwaipungu,Mwana kwetu,Somboko amba,Siri ya mapenzi,Kipipa Ayubu,Takadiri,Mashaka nakonda,Dunia msongamano,Hasira za chunusi,Christina Moshi,Fordy,Sosy,Homa imenizidia,Majuto,Chatu mkali,Kaka Kinyogoli,Shukrani kwa mjomba,Usicheze na bahari,Marcelina,Mayasa,Matatizo ya ukewenza,Mageuzi na nyingine nyingi.....

Bendi hii iliundwa na wanamuziki kama Freddy Ndala Kasheba(R.I.P),Hassan Rehani Bitchuka,Muhidin Maalim Gurumo,Abel Barthazar,Nguza Vicking,Shaban Dede 'Kamchape,Hassan Shaw,Mhina Panduka,Benno Villa Anthony,Lister Elia,Kassim Rashid,Charles Ngosha,Ally Makunguru na wengine wengi......
 
Bila kuwasahau Bima Lee Orchestra....Bendi hii ilikuwa ikimilikiwa na Shirika la Bima la Taifa.....Iliimarika zaidi mwaka 1984 baada ya kuwapata wanamuziki kutoka bendi tofauti tofauti walipoletwa kwenye bendi hii kwa lengo la kuiimarisha....Wanamuziki hao ni Shaban Dede,Jerry Nashon 'Dudumizi',Joseph Mulenga,Abdalaah Gama na Athuman Momba....Bendi hii ilikuwa ikitumia mtindo wa Magnet 84 na baadae uliboreshwa ukawa Magnet ndele Tingisha.....

Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Neema,Shangwe ya harusi,Makulata,Linalonisibu,Milionea wa mapenzi,Linalonisibu,Siri yako,Visa vya mesenja,Uzuri ni tabia,Dunia ni upepo,Busu pande tatu,Ndoa fungo la hiyari,Penzi dawa ya chuki,Samaki baharini,Baba Shani,Shakaza na nyingine nyingi....

Bendi hii iliundwa na wanamuziki kama Shaban Dede,Athuman Momba,Joseph Mulenga,Abel Barthazar,Abdallah Gama,Belesa Kakere,Maxmilillian Bushoke,Jerry Nashon,Coumson Mkomwa,Eddy Sheggy,Fresh Jumbe na wengine wengine
 
Kwa leo ngoja nimalize na DDC Mlimani Park Orchestra..........Dah....Hata sijui nianzie wapi hapa maana maelezo yatakuwa marefu kweli,ngoja japo niyafupishe kidogo....

Historia ya Bendi hii inaanzia mwaka 1978 ambapo takriban wanamuziki wanane waliihama bendi ya Dar International na
kwenda kuanzisha bendi ya Orchestra Mlimani Park.Baadhi yao ni aliyekuwa mtaalamu wa kupiga ala zote King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jeff,hawa waliungana na Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka na Abel Barthazar(ambaye ndio hasa muanzilishi wa Mlimani Park)..... Ilijulikan hivyo(Mlimani Park Orchestra) kutokana kuwa na maskani yake pale Mlimani Club mitaa ya Mwenge jijini Dar es Salaam chini ya umiliki wa Tanzania Transport and Taxi Services.

Mwaka 1983 waliokuwa wamiliki wa bendi hiyo walifilisika na na hatimaye bendi hiyo ikachukuliwa na Dar es Salaam Development Corporation (DDC) na hapo ndiyo ikaanza kuvuma kwa jina la DDC Mlimani Park Orchestra ikiwa chini ya wanamuziki galacha na waasisi, Muhidin Maalim Gurumo, Abel Baltazar, Hassan Rehani Bitchuka, ambao walitokea JUWATA Jazz Band huku Cosmas Thobias Chidumule, Michael Enoch ‘King Michael' na mpiga gitaa la solo mahiri, Joseph Batholemeo Mulenga, wakiwa wametwaliwa kutoka Dar International. ............Mtindo walioutumia tangu enzi hizo ni ule wa Sikinde Ngoma ya ukae.....

Baadhi ya nyimbo zilizotamba sana za Sikinde ni pamoja na Sauda/MV Mapenzi(namba 1 na 2),Neema,Usitumie Pesa kama fimbo,Mume wangu Jerry,Clara,Hiba,Matatizo ya nyumbani,Majirani huzima redio,Nidhamu ya kazi,Kassim amefilisika,Talaka ya hasira,Hadija,Barua toka kwa mama,Celina,Editha,Fikiri nisamehe,Pole mkuu mwenzangu,Diana,Pesa,Hata kama,Bubu ataka sema,Mnanionesha njia ya kwetu,Tangazia mataifa yote,Mtoto akililia wembe,Nalala kwa tabu,Duniani kuna mambo,Kiu ya jibu,Dua la kuku,Nawashukuru wazazi,Pata potea,Nelson Mandela,Uzuri wa mtu,mdomo huponza kichwa,Taxi Driver,Tucheze Sikinde,Conjesta na nyimbo niyngine nyingi tamu.....

Wanamuziki walioipitia bendi hii ni pamoja na King Michael Enock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum,Habib Jeff,Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka,Abel Barthazar,Henry Mkanyia,Fresh Jumbe,Hussein Jumbe,Benno Villa Anthony,Tino Masinge 'Arawa',Hassan Kunyata,Francis(Nassir) Lubua,Maalim Hassan Kinyasi,Abdallah Gama,Max Bushoke,Muharami Said,Kassim Mponda,Julius Mzeru,Said Chipelembe,Ally Jamwaka,Machaku Salum,Ally Yahaya,Shaban Lendi,Joseph Bernard,Juma Hassan Town na wengine wengi....
 
Mimi bana sikinde tuuu, jamani sikinde watani wangu msondo mtaniwia radhi. Dah kuna vibao nikivisikia mpaka natokwa na jasho kuna kitu km Duniani Kuna mambo, wikiendi nalala kwa taabu, kwa ujumla sikinde you rock my heart!! ningekuwa na pesa ninge invest trillions pale basi tu sina kitu. haya kuna hawa marques du zaire enzi za kamanyola bila jasho kuna kibao kama dola mtoto wa Dodoma( yakaa yaka eeehn mwana mama ndimandimaeee mwana mama ...... mtoto wa dodoma) kuna kinanda flani kinapigwa mle na gitaa yaani ni raha tupu

inanikumbusha sana dada yangu marehemu Mage jamani wakati niko Sumbawanga alikuja toka Dar basi anaziimba hizi nyimbo za makwizzz aaah jamani KAMANYOLA BILA JASHO! ikaja telemuka telemuka chekechaaaaaa
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom