Zilikuwa nyakati za Chico, Nat King Cole, Dean Martin, Sammy Davis Jr, Sidney Poitier..Ukipenda Sal

Sal Davis nilibahatika kumsikia miaka ya 90s hap0 Euro Pub,nafkiri akiwa karejea toka Ulaya,kwakweli alikua na kipaji cha pekee,alifanya ninze kufatilia jazz kwa karibu.kwa akili yangu nikijua ni mmarekani Mweusi anayeishi TZ.
Babukijana,
Sal Davis ni rafiki yangu na nimeandika maisha yake lakini bado ni mswada
kitabu hakijachapwa.

CIMG0225.JPG

Mwandishi na Sal Davis Chef Pride Restaurant Lumumba Avenue Dar es Salaam
2006

Unaweza kupata habari zake hapo chini:
Mohamed Said: FROM THE PAGES OF THE EAST AFRICAN MAGAZINE: SAL DAVIS
Mohamed Said: SAL DAVIS AND CASSIUS CLAY (MUHAMMAD ALI) LONDON 1963
 
Tamim machine nyingine kabisaaa mkuu

Kwanza tazama his prodigious volume of scholarship. Najua haha publish vitabu vine kama akina Njozi et al. Lakini I know he has published hundreds of essay and commentaries kwa bahai mbaya sina hakika kama alifanya film documentaries but he could be a valuable contributor na naamini ana so much secondary and primary resources. Miaka hiyo nilikuwa naenda naye maeneo mbali mbali alipokuwa anaenda kufanya public lectures na and its very difficult not to see the the range, probity as well as impact of his intellectual analyses, interventions, and debates ambazo in my humble opinion were short of nothing but extraordinary. Kwa bahai mbaya hakuna vijana ambao wamefuata nyayo zake kama yeye ninaowafaham zama hizi. Mimi hunikumbusha RK Dau by the way Dr anavyoweza ku move seamlessly between the kwa Klabuni hapo Pan na akina Captain Malik to classroom then to conference circuit, kwenye sports, and corporate boardroom, to the corridors of political power. As for Tamim ni mtu ambaye he often relishes intellectual debate and combat because he believed in the power of ideas na hasa ideas beyond haya mambo yetu ya kawaida. Nakumbuka articles zake Benzi za Africa events alivyokuwa akiwavuruga akina Ahmed Rajab and Co. Binafsi nakumbuka alinipa moja ya first copies za mwanzo za kitabu cha Partnership na vitabu vinginevyo na linguine nilikuwa naazima na soirudishi of course na ninavyo mpaka leo. In my opinion ni mtu aliyeamua ku dedicate his life kuendeleza watu na kwa bahati mbaya sana imekuwa kama case ya Mfalme asiyetambulika kwao. Muhim Allah SW anatambua mchango wake.

The man has a beautiful mind he could have been in the ranks za akina sheikh anta drop, Ivan Van sertima, Molefi Kente Asante, Horace Campbell na wengineo. Itabidi Maalim Mohammed Said tumfungulie Uzi wake
HNIC,
Nimesafiri na Tamim kwingi.

Nimekuwa na Tamim Kenyatta University, University of Johannesburg, University
of Ibadan na kwengine kwingi kama Mzumbe, University of Dar es Salaam na
kwengineko.

Ikiwa Tamim ataamua kunyanyua kalamu kuandika yote ayajuayo kuhusu nchi yetu
hicho kitabu kitakuwa rejea ya maana sana.

Nakuwekea picha hiyo hapo chini ambayo tulipiga nyumbani kwangu 1995 wakati
tunaingia katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.

qY6uYYgb15ME4kFeT-SqH36aR5ieF1AxmwynTvYaVtkWOzTTmvNhURlv_07y2t-5UW4s_vXoZmevN9vRYYu7xPFshrI9XfPLrbIUE7MIFZIImni2s8bMDohQvyL8N_bH3ovCSs_q7mteeixEjzPzbQjbW3n87iw4kCuXuOkTaHH8yH3O5Oe92Vd2r9IrlZI4FwPhW7voroXFLYcAV9XtkQBCc4EuHmeyxx5vMXDpIVhRdBLYdMBm_wZ2uslfVkzjASo9jzx-ujNRenXi1Se9XOxbXJ_6JBt3447cbsvd5n-xECan-muU8nghYnstAVFzFylmRRyCEAIX9einObLbJYhbDxwh0vddfCQXK3sDKIiswy0WX17QHXh0V3Sawd4grU-UtfIe1CcS4ES0FnTH6uG-g-789jFY0l6HQLF75gP2j6yrNHJtbpWz885Q5vhzaaFFCjuqC15L0a3gs3_lA1HxfhIru7HUSEDVUSQsTRqHnRmLSztxbRvA4FYITjQwPdyYl021l9bFQG4uhiDrj8TFUD6gBh-kusgBWFDfAc5xIMYqOPDw2wH9DxmdU4CWTgsnVbwT61kl26o8lntMhWfHW_reAcv6pyBhEPkzLAMpZFjM2v__oQ=w453-h356-no

Waliokaa kushoto: Tamim Faraj, Faraj Mohamed, Prof. Haruna
Lipumba na Dr. Ramadhani Dau. Nyuma kushoto ni Juma Kilaghai
na Mwandishi
 
HNIC,
Nimesafiri na Tamim kwingi.

Nimekuwa na Tamim Kenyatta University, University of Johannesburg, University
of Ibadan na kwengine kwingi kama Mzumbe, University of Dar es Salaam na
kwengineko.

Ikiwa Tamim ataamua kunyanyua kalamu kuandika yote ayajuayo kuhusu nchi yetu
hicho kitabu kitakuwa rejea ya maana sana.

Nakuwekea picha hiyo hapo chini ambayo tulipiga nyumbani kwangu 1995 wakati
tunaingia katika uchaguzi wa kwanza vyama vingi.

qY6uYYgb15ME4kFeT-SqH36aR5ieF1AxmwynTvYaVtkWOzTTmvNhURlv_07y2t-5UW4s_vXoZmevN9vRYYu7xPFshrI9XfPLrbIUE7MIFZIImni2s8bMDohQvyL8N_bH3ovCSs_q7mteeixEjzPzbQjbW3n87iw4kCuXuOkTaHH8yH3O5Oe92Vd2r9IrlZI4FwPhW7voroXFLYcAV9XtkQBCc4EuHmeyxx5vMXDpIVhRdBLYdMBm_wZ2uslfVkzjASo9jzx-ujNRenXi1Se9XOxbXJ_6JBt3447cbsvd5n-xECan-muU8nghYnstAVFzFylmRRyCEAIX9einObLbJYhbDxwh0vddfCQXK3sDKIiswy0WX17QHXh0V3Sawd4grU-UtfIe1CcS4ES0FnTH6uG-g-789jFY0l6HQLF75gP2j6yrNHJtbpWz885Q5vhzaaFFCjuqC15L0a3gs3_lA1HxfhIru7HUSEDVUSQsTRqHnRmLSztxbRvA4FYITjQwPdyYl021l9bFQG4uhiDrj8TFUD6gBh-kusgBWFDfAc5xIMYqOPDw2wH9DxmdU4CWTgsnVbwT61kl26o8lntMhWfHW_reAcv6pyBhEPkzLAMpZFjM2v__oQ=w453-h356-no

Waliokaa kushoto: Tamim Faraj, Faraj Mohamed, Prof. Haruna
Lipumba na Dr. Ramadhani Dau. Nyuma kushoto ni Juma Kilaghai
na Mwandishi

Ma sha Allah, list kali hiyo.
 
Mzee wangu nimeanza kufuatilia historia zako kabla hata sijaijua JF binafsi naheshimu kazi yako na bila ww sidhani km tungeijua Dar ya miaka hiyo ya nyuma maana wazawa wa cku hizi wanajisifia tu nimezaliwa KCMC mara AGHA KHAN ila mwisho wa cku hana lolote kunako Dar.
Nitajitahidi kufuata nyayo zako.
 
Ma sha Allah, list kali hiyo.
Maalim Faiza,
Nilimheshimu Tamim katika mgogoro wa Zanzibar kuingia katika
Organisation of Islamic Conference (OIC) mwaka wa 1993.

Rais Ali Hassan Mwinyi na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Hassan
Diria
walikuwa katika wakati mgumu sana.

Kanisa lilisimama vikali kupinga, magazeti yote yalikuwa yanashambulia
ili muradi Zanzibar ilikuwa mashakani pamoja na Rais Mwinyi na Waziri
Diria.

BAKWATA haikuwa na watu ambao wangeliweza hata kwa mbali kusaidia.
''Enter the Dragon...''

Tamim kila tukikaa kutafakari hali ya nchi yetu anaeleza masikitiko yake
jinsi vyombo vya habari pamoja na magazeti ya CCM na serikali yalivyokosa
adabu kiasi hata cha kumshambulia MwenyeikitI wa CCM Rais Mwinyi.

Kila tukikaa hatuna mazungumzo ila hayo.

Nikikutananae namkuta mwenzangu kesha soma magazeti yote ya siku hadi
''gutter press,'' ananipa ''briefing.''

Ghafla likatokea jambo limezuka vuuu!
Wakati ukifika In Shaa Allah nitalieleza hili la kuzuka.

Ndipo Tamim akaja na kitabu kutoka Nigeria, ''The Two Headed Dragon,''
kitabu kilichokuwa kinaelezea fitna yote ya OIC.

Tamim anakonda panapokuwa hakuna kitu cha kuhangaisha bongo lake
na ananenepa katika, ''crisis.''

''Hawa tunawafungulia front mbili za mapambano tupime ubavu wao.
Tunabisha hodi huko huko kwenye kichaka chao...kisha tunawaleta huku
kwetu wapambane na askari wenda kwa miguu chakula chao biskuti za
chumvi na maji.''

Tamim huyo anakuja na ''strategy,'' ya mapambano.

Bunge lilipigwa na mshangao na barua walizokuwa wanapokea kuhusu
tatizo la Zanzibar kujiunga na OIC kiasi iliulizwa hawa ni akina nani wenye
kalamu kama hii?

Ghafla hali ya hewa Dar es Salaam ikabadilika na Rais Mwinyi akawa kapata
utetezi na watetezi.

Waliokuwa wanamshambulia Rais Mwinyi wakaingiwa na hofu.

Hawakuwa na uwezo wa kufungua, ''front,'' ya pili kuja kulikabili jeshi la,
''infantry.''

Lugha yao ikaanza kubadilika kulikuwa na maneno ya, ''impeachment.''
Msamiati huu ukatoweka ikawa sasa wanasema, ''Baba wa Taifa asaidie.''

''The eagle has landed...''

Ingia hapo chini usome ilikuwaje:
Mohamed Said: Zanzibar Membership to Organisation of Islamic Conference (OIC) and Islam in Africa Organisation (IAO)
 
Mkandu karibu såna.
 
Kuna watu wakisikia OIC matumbo yanajinyongorota na kusukwasukwa na sintofahamu ya ufikiri. Kila neema kwa waislamu kwa ni balaa!!
 
Heshima kwenu wazee wetu....ama kwa hakika umeelezea vizuri na Aina ya uandishi enzi za bandari salama na vijana Wa mjini enzi hizo
 
Asante Mzee mungu azidi kukujalia afya na uzima tuendelee kujifunza mengi kutoka kwako

Japo vijana wa siku hiz umoja huo kama wenu hakuna sana
 
Mohammed Said ninekupata barabara

Maalim Faiza na wewe pia ninekupata

Wasi wasi wangu ni kuwa hii platform.ni ya wagala na wakati huu wenyewe kwa wenyewe wana civil war na kuna siku itafungwa nashauri tuwe na platform mbadala mbadala ambayo tunaweza kukopy na kusafiri hizi nondo
 
16904699_1684605288505254_3395619926298348932_o.jpg

Leo jumapili tar 26/2 tulikuwa kwenye arobaini ya marehem kamanda Chico . Tukiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa marehem . Huyo aliyevaa shati la brown ni Awadhi Chico akifuatiwa na mdogo wake alievaa dark blue. Tunamuomba Mwenyezimungu awape subra na maelewano
 
Sydney simwoni hapo
 
NASHUKURU MZEE SAIDI KWA HISTORIA HII NZURI, NA BILA YA KUMSAHAU KUMTAJA BABA YANGU MDOGO GHALIB HAMZA a. k. a GUY. Allah awarehemu wote Amini
 
Roshnee Ghalib aka Guy alikuwa rafiki yangu toka udogo wetu. Allah amrehemu. Mara ya mwisho tumekutana Magomeni akanambia ndiko anaishi na kununua nyumba sehemu hizo. Mimi nilikuwa njiani naelekea Tanga nilipokuwa nafanya kazi. Nilihudhuria maziko yake. Nilipofika msibani Muharam Mkamba alikuja kunipa pole kwani alikuwa anatambua kuwa mimi ni Ghalib tulikuwa marafiki toka utoto wetu tukicheza mpira pamoja Mnazi Mmoja.
 
MashaAllah, nashukuru sana mzee wetu, nyinyi ndio hazina yetu iliyo bakia. Tafadhali pitia Magomeni Mikumi uone familia yake bado ipo hapo, watoto wake Saidi, Mwanaidi na Almasi. Huyo Balozi Abdul Sisco Mtilo ni mjomba yetu pia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom