Sumbi Sanchez
Member
- Apr 16, 2017
- 45
- 172
Miezi miwili iliyopita Melinda Gates, mke wa Bilionea Bill Gates, alisema kuwa muda si mrefu Afrika ingetawaliwa na miili ya wafu mitaani kutokana na vifo vya Covid19.
Dada yetu Mange Kimambi nae muda mrefu sana amekuwa akitabiri baada ya wiki mbili au wiki kadhaa Corona itakuwa si siri tena hapa Tanzania kwa kuwa tumekataa lockdown.
Wajuaji wengine nao huku maofisini, mitandaoni na mitaani walitabiri kuwa kwa kuwa hatukuchukua hatua kama za huko Ulaya na nchi nyingine za Afrika zilizoamua kukopi upuuzi wa 'lockdown' hivyo tungekosa hata sehemu za kuzikana.
Eti jamani? Hiyo hali itatokea lini? Binafsi Uswahilini ninapoishi hakuna mtu anajali kuhusu barakoa, social distancing, sanitizer, kunawa mikono wala kitu chochote kinachohusiana na hivyo. Safari za kwenda Ilala sokoni, Kariakoo na sehemu nyingine za mikusanyiko zinafanywa bila tone la woga. Lakini sijawahi kusikia kifo wala kesi ya Corona inayomuhusu mtu ninayemfahamu hapa mtaani.
Sasa jamani hebu tuambieni hivyo vifo visivyo na idadi vitaanza lini? Maana mnatuambia serikali inaficha takwimu. Ni lini sasa tutarajie maiti mitaani?
Nina mashaka makubwa kuwa Marekani wanachapisha takwimu za uongo za vifo na kesi za Covid19 kwa malengo fulani. Nchi kama Belarus hazijawahi kufunga mpaka wala kuwa na lockdown lakini hawafikii hata 1/10 ya maambukizi ya Marekani. Hapa kwetu pia tumeshaambiwa hakuna lockdown wala baba yake lockdown. Lakini hali ni shwari mno ukilinganisha na takwimu za kuogofya za Bwana Trump.
Corona ipo lakini haitishi kama mataifa fulani na jumuiya za kimataifa wanavyojaribu kutuaminisha kwa malengo wanayoyajua wenyewe. Lockdown ni upuuzi wa ajabu sana. Unafanya mpaka lini hiyo lockdown? Mpaka watu watakapoanza kufa na njaa?
Tumeshaanza kuona nchi za Ulaya zikiondoa vizuizi walivyoweka kuhusiana na Covid19. Wamegundua ni upumbavu usio na maana yoyote. Asante serikali ya Tanzania kwa kukataa kuiga upuuzi. Covid19 itaendelea kuwepo kama magonjwa mengine yanayoua watu kila siku. Maisha lazima yaendelee.