Zile hoja za ufisadi ziko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zile hoja za ufisadi ziko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsayaMwita, Sep 17, 2008.

 1. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nakushukuru Mola kwa kunipa pumzi yako baba, bado ninaendelea kuishi, japo sitakiwi kuishi hapa duniani(Tanzania), najua ni mpango wako kuwa hapa duniani katika nchi njema ya Tanzania, nchi tajiri huku mimi nikiwa maskini wa kutupwa.

  Ndugu zangu wana JF, kuna kipindi nilidhani mtalisaidia Taifa kwa kukemea maovu ya viongozi wetu na kuwaasa ya kufanya lakini mambo yamegeuka, MAFISADI wametuzidi nguvu tumesahau yote, yale ya BOT, EPA, RICHMOND na mengineyo mengi,.

  Naomba sasa tujiulize kweli nini hatima ya watoto wetu kwa siku za usoni?

  Hebu kweli tuna mikakati ya dhati ya kuleta mabadiliko 2010?,

  Niliwahi kusema kuwa mbona huko kwenu mijini hakuna mageuzi ya kweli, na hapo ndipo kwenye vyombo vya habari vya kutosha? kwenye wasomi wa kutosha? waandishi wa kumwaga?
   
 2. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni jambo la kujiuliza hebu hizi kelele tunazopiga tutasikika? ni kwa nini sasa huko mijini msiamke kama sisi huku shamba tulivyoamua, kwamba CCM sasa basi?
   
 3. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kuwatoa ama kusema Basi kwa ccm tu si tiba kabisa Labda useme Basi kwa ccm na ndiyo kwa wepi na wenye sera zipi?

  Juzi nilibaki mdomo wazi baada ya kusikia chama mbadala kinauza sera zake kule kwetu eti sera yake ni MSICHAGUE CHAMA CHA MAFISADI.

  Yani ni vichekesho tu .Homeboy kazi ipo yawezekana leo usiniilewe lakini mwalimu mzuri ni Mda.
   
 4. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Mstahiki Meya Leo bado utaweza Ongea haya?
   
Loading...