Zijue tofauti za mtu masikini na tajiri

GoPPiii.

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
1,478
2,000
By T. Harv Eker

Book- Secrets of the Millionaire Mind.

1. Tajiri huamini yeye hutengeneza maisha yake,masikini huamini maisha hutokea tu, huamini kuna mtu inabidi afanye kitu ili awe tajiri. Maskini huamini na kulalamika kwamba wao ni maskini sababu uchumi wa nchi mbovu,sababu ya serikali,sababu ya soko bovu, sababu ya biashara zao mbaya, sababu ya muajiri wao, Mungu kawatupa, na wazazi wao.
Ukifuatilia kuna matajiri wanazidi kupiga pesa tu sababu huamini wao ndo wahusika wa maisha yao.

Hakuna mtu atakayetengeneza maisha yako,kila mtu apambane na hali yake tutatusua,kulalamika kila siku hakutupeleki popote.

2. Mtu masikini huwachukia watu matajiri na waliofanikiwa.
Hii ni sababu ya wivu na hasira za ugumu wa maisha. Huamini wao ni masikini sababu ya watu matajiri kwamba matajiri wamechukua pesa zote.

Hakuna haja ya kumchukia tajiri, mpende na ikibidi awe role model wako katika kusaka utajiri.

3. Mtu masikini hupenda kushinda na kuchangamana na masikini wenzake lakini mtu tajiri huchangamana na waliofanikiwa ili apate changamoto na afanikiwe zaidi.
Masikini hufanya hivi ili ili kuhalalisha hali yake ya umasikini,wanasema kifo cha wengi ni harusi.

Tafuta waliofanikiwa,jihusishe nao,hao ndo wana siri za mafanikio,njia za kufanikiwa wanazo hao.

4. Katika watu wasiotumia pesa zao vizuri ni watu masikini.
Hawatunzi pesa wakiamini hawana pesa za kutunza,hawaweki akiba ya pesa,akipata pesa basi asilimia ni kubwa ya kuimaliza hiyo pesa. Huwezi pata milioni na ikafanya mapinduzi kwako ya kimaisha kama elfu kumi tu inakushinda.
Hii ndo sababu hata ukipewa milioni mia leo baada ya mwaka unajikuta huna pesa tena hii ni kwa sababu somo la matumizi na kuweka vipaumbele linatushinda. Mfano mzuri wafuatilie wanaoshida mamilioni kupitia michezo ya kubahatisha baada ya muda hawana kitu.

Tumia ukipatacho vizuri,weka akiba hata kama ni kidogo. Haba na haba hujaza kibaba.

5. Mtu masikini huangalia changamoto kwenye mawazo mapya ya kusaka pesa yanapomjia. Unaweza kuta anawaza kulima badala ya kuwaza faida atakazopata akilima mtu huwaza mvua inaweza isinyeshe au mashamba yako mbali au msimu ulipita watu walipata hasara kwenye kilimo. Tujifunze kujilipua. Upatapo wazo jipya ni vema ukawaza faida utakazo pata ili upate nguvu za kupambana na kutimiza wazo lako. Ukiwaza sana changamoto hauna utakachofanya maana hakuna kitu kisicho na changamoto.

Ukitaka kulima lima,kufungua duka wewe fungua, ukitaka fanya jambo fanya,weka mikakati vizuri.

Mtu anataka kulima anaomba ushauri kwa fundi kujenga khaaaa.

Mtu anataka kununua boda boda anamuuliza na kuomba ushauri kwa muuza duka duuuh.

Ukitaka kulima omba ushauri kwa mkulima.

Ukitaka kufuga mtafute mfugaji akupe shule.

Ukitaka kuwa na duka vile vile tafuta muuza duka akupe ushauri muafaka.

Shukrani.

Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
4,524
2,000
kuna masikini na umasikini, kwangu mimi masikini ni yule mlemavu aliyepungukiwa viungo na hana mbinu yoyote ya kumsaidia kujikomboa kiuchumi,,,,umasikini sasa, ndio kama huu mtu amekaa nyuma ya keyboard au yupo na kisimu chake mdaa huu amelog in JF mfukoni ana buku tu, anasubiri bando liishe ajiunge kifurushi, huku wengine wakiwa hivyo hivyo nyuma ya keyboard wakiingiza 50000 kila baada ya saa...tunatofautiana sana.
 
bullar

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
6,635
2,000
kuna watu hua wana sema ipo cku tu nitatoka alf hana mikakati hua nawa angalia nasubir hio miujiza
 
sundoka

JF-Expert Member
Oct 9, 2011
1,759
2,000
kuna masikini na umasikini, kwangu mimi masikini ni yule mlemavu aliyepungukiwa viungo na hana mbinu yoyote ya kumsaidia kujikomboa kiuchumi,,,,umasikini sasa, ndio kama huu mtu amekaa nyuma ya keyboard au yupo na kisimu chake mdaa huu amelog in JF mfukoni ana buku tu, anasubiri bando liishe ajiunge kifurushi, huku wengine wakiwa hivyo hivyo nyuma ya keyboard wakiingiza 50000 kila baada ya saa...tunatofautiana sana.
Totally wrong. Na waafrika wengi tunatumia huu msemo wa 'maskini ni yule mlemavu asiye na viungo' ili kujifariji lakini in a real sense maskini ni yule aliyezungumziwa kwenye post. Kuna walemavu wengi hawajakubali kuwa maskini na sasa ni matajiri wakubwa, alafu dume zima linasema maskini ni yule asiye na viungo alafu linaenda kumuomba kazi mlemavu tajiri.
 
Kweli kabisa aiseee
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,620
2,000
2. Mtu masikini huwachukia watu matajiri na waliofanikiwa.
Hii ni sababu ya wivu na hasira za ugumu wa maisha. Huamini wao ni masikini sababu ya watu matajiri kwamba matajiri wamechukua pesa zote.
Una maanisha magufuli ni mtu maskini au?
 
GoPPiii.

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
1,478
2,000
Totally wrong. Na waafrika wengi tunatumia huu msemo wa 'maskini ni yule mlemavu asiye na viungo' ili kujifariji lakini in a real sense maskini ni yule aliyezungumziwa kwenye post. Kuna walemavu wengi hawajakubali kuwa maskini na sasa ni matajiri wakubwa, alafu dume zima linasema maskini ni yule asiye na viungo alafu linaenda kumuomba kazi mlemavu tajiri.
Shukran kwa maelezo mazuri.
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
41,604
2,000
Mbona mimi masikini ila sina sifa hizo hapo juu? Napambana kweli kweli nijikwamue kwenye umaskini na marafiki zangu wengi matajiri!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom