Zijue tofauti kubwa za Misiba ya zamani na ya sasa hasa kwa upande wa Waombolezaji

Kumbe Tecno sometimes wanakuwaga na simu nzuri,vipi mkuu hii imesimama ngapi ??
Shot055.png
Lol, Jf leo imeamua kutuanika live bila chenga tunaotumia simu.
Nakereeka.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
hiyo ni athari moja tu maendeleo ya kiteknolojia

Sent from my F5 using JamiiForums mobile app

 
Kweli aisee,mm mwenyewe huwa nakereka mno na mijitu inayokimbilia kupost picha za marehemu kwenye mitandao ya kijamii.

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
 
Sema na wewe una Moyo, ukiiona unaenda kugoogle, lol.
Nisamehe bure mkuu,maana huwa napenda sana kumjua mtu kiundani sana,na mojawapo ya njia ninazozitumia ni kuangalia simu yake,maongezi yake au hata vitu anavyopenda kuchangia kwenye majukwaa.
 
Misiba ya zamani utawasikia ' Waombolezaji ' muda wote....
  1. Wakimlilia Marehemu huku wakitoa sana ' michango ' ya Pesa.
  2. Wakiwatia moyo Wafiwa
  3. Wakisaidia Kazi muhimu za pale Msibani
  4. Wakihakikisha mali za Marehemu pale Kwake haziibiwi
  5. Nyuso nyingi za Waombolezaji zikiwa na Simanzi kubwa
  6. Wanasali muda wote pamoja na kuimba kwa hisia ' Kali ' kabisa
  7. Hawajali kama Chakula kipo tayari na huwa hata hamu ya Kula hawana
Misiba ya sasa utawasikia ' Waombolezaji ' muda wote....
  1. Wakipiga majungu hasa ya kumuhusu ' Marehemu ' na Familia yake
  2. Wakipiga picha wawahi kuziweka katika Social Media zao
  3. Wanategea hata kusaidia tu Kazi za pale huku muda mwingi wakiwa ' busy ' na Kuchati
  4. Wakienda Chooni huwa hawakumbuki ' Kuflashi ' na badala yake wengi wao hutuachia ' Kumbukumbu ' zao za ' Kutukuka ' za ' Vinyesi ' vyao vyenye ' harufu ' kali.
  5. Utawaona wanapiga ' Miayo ' na wanaangalia Saa ili wajue Chakula kinakuja au hapana na ole wako ' wasile ' utajuta kuwafahamu / kuwajua ' kudadadeki '
  6. Wanawajadili Mdee, Malinzi na Hapi
  7. Wanashindanisha tu ' Magari ' yao na ' Simu ' zao lakini katika kile ' Kikapu ' cha ' michango ' hata Tsh 100/ hawajatumbukiza
Shikamooni!

Nawasilisha.
Mienendo ya watu misibani siku hizi inahuzunisha kuliko hata msiba wenyewe.
 
Mioyo ya binaadam imejaa unafiki sana,zamani ulikua ukifa unasifiwa sasa hivi ukifa hata ya uvunguni utayajua
 
Nisamehe bure mkuu,maana huwa napenda sana kumjua mtu kiundani sana,na mojawapo ya njia ninazozitumia ni kuangalia simu yake,maongezi yake au hata vitu anavyopenda kuchangia kwenye majukwaa.
Hahahahaha i got you, bro
 
Back
Top Bottom