mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,050
- 4,903
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk Fidelice Mafumiko amesema kuwa anayetaka kupima vinasaba (DNA), iwapo ana wasiwasi na mtoto anapaswa kufuata taratibu, badala ya kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA).
Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 46 ya biashara Sabasaba, Dk Mafumiko alisema kuna hatua nyingi za kufuata ili kupata huduma hiyo ikiwamo kutoa taarifa kwa ofisa maendeleo ya jamii na wao ndiyo watapeleka maombi yao GCLA.
“Tukipata maombi kutoka katika mamlaka husika, tunayafanyia kazi. Gharama za kupima DNA ni rahisi sana kwa mtu mmoja ni Sh100,000” alisema Dk Mafumiko.