Zijue Tabia za Wanyama na uone unafanana Tabia na Mnyama gani

holy holm

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2017
Messages
2,217
Points
2,000

holy holm

JF-Expert Member
Joined May 6, 2017
2,217 2,000
Bata:Kujivuta vuta, kufanya kazi polepole na kuendekeza uvivu mapaka mambo ya kikundi yanazorota au kufa kabisa.

Bundi:Mtu anayefikiria ana akili kuliko wote kwenye kikundi- hutumia lugha ngumu kueleweka

Chura:Rudia rudia kitu kile kile mapaka anawachosha wenzake kundini

Kenge:Hatumii akili sawasawa, ujinga mwingi na kufanya maamuzi ya ovyo yenye kuwakatisha tamaa wenzake

Kiboko:Kulala lala na kupiga miayo, wakati wenzake wanachacharika, yeye ni kukaa tu hafanyi kazi.

Kifaru:Yeye hushambulia wengine kwenye kikundi bila sababu

Kinyonga:Kigeugeu, akiwa kwa mwanakikundi huyu anasema hili na akiwa kwa mwingine anasema tofauti

Kobe:Hujitoa akiudhiwa, hana uvumilivu kwenye changamoto zinazoikabili kikundi.

Kuku:Kuvuruga palipotengenezwa, kwenda tofauti na maono ya kikundi kwa kujali na kuzingatia mambo ya muda mfupi tu.

Mbuni:Huficha kichwa na hufikiri hakuna shida kwenye kikundi hata kama zipo shida nyingi

Nyati:Kujihami tu kwa sababu ya woga, hakosolewi, ukimgusa tu anaazisha vita vya maneno au kupigana

Nyoka:Anajificha huku akiuma bila kusema. Mchonganishi

Nyumbu:Woga na kutotumia akili kabisa.

Paka:Yeye anataka ahurumiwe tu na wenzake, hana mchango wowote kwenye kikundi.

Panya:Hachangii chochote yeye hujificha tu na kujitokeza wakati wa neema.

Popo: Hana msimamo, Kwa wanaokubali hoja yupo na kwa wanaopinga hoja yupo. Haeleweki.

Punda:Wagumu kubadilika hata umuelimishe kwa namna gani misimamo yake ni yale yale ya zamani.

Samaki:Hachangii hajibu, kazi kuteleza, kukwepa na kutoweka tu na huonekana hali ikitulia na kuwa shwari.

Simba: Hupigana kama hakubaliwi mawazo yake na wanakikundi.

Sungura:Hukimbia kama kuna dalili za hatari na kwenda kinyume na makubaliano ya kikundi

Tausi:Yeye huringisha na mambo mazuri aliyonayo ambayo wanakikundi wenzake hawana.

Tembo:Hufunga njia bila sababu watu wasipite. Huzuia mawazo, maamuzi ya kikundi yasifanikiwe bila sababu.

Tumbili:Mizaha mizaha tu wakati wote hayuko makini hata kwa mambo muhimu ya kikundi.
 

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Messages
8,365
Points
2,000

KENZY

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2015
8,365 2,000
Mwenye uzi akija sisemi mengi ila tahadhari tu kwa mweka mada uwe umejichanja chale za kujikinga na hirizi inayopumua usisahau... Maana asiefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu Hivyo msubiri mlimwengu aje.
 

Forum statistics

Threads 1,378,771
Members 525,185
Posts 33,724,037
Top