Elections 2010 Zijue Sumu Zinazoiua CCM Taratiibuuuuu!

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
127
Sote Tumeshuudia Rafu za Uchaguzi ambao umemalizika kwa kumpatia bwana Mkubwa Ushindi wa Mezani Kama walivyokuwa wamepanga wao.

Lakini wasikae wakajidanganya na wajione wao ni clever sana kuliko watanzania wengine wanaohubiri haki na chaguzi huru.

Sasa basi genge la hawa wezi wa CCM litegemee matatizo yafuatayo yanayokwenda kukizamisha Chama:-

  1. Lile kundi lililonyang'anywa ushindi kipindi kile cha mchakato wa Kura za maoni ndani ya CCM bado linahasira za kichini chini, na wanaungana na wapinzani kufurahia ushindi uliowabwanga wale wakongwe e.g. Lawrence Masha, Philip Marmo, Mramba n.k. Kundi hili litaendelea kuwepo licha ya jitihada zinazochukuliwa na viongozi wa juu kukinusuru Chama. Hii ni added advantage kwa Upinzani.
  2. Pesa iliyotumika kwenye mchakato mzima wa kampeni za CCM inatakiwa irejeshwe sehemu/ kwa watu husika. Hapa sasa ndo penye mtihani mkubwa na watanzania wategemee kusikia mengi baada ya dikteta Kuanza awamu nyingine ya uongozi wake. Ni dhahiri kuna gaps ambazo hazitaweza kuzibwa, na sababu ni kwamba kipindi cha kampeni CCM hawakutegemea kupata upinzani mkubwa kama ilivyojidhihirisha, Sasa basi katika kuhaha ili kujinusuru na fedheha ya kushindwa NGUVU YA PESA ikapewa Kipaumbele. Ukijiuliza vyanzo vya hizo pesa ni vipi?, na je walifanya uamuzi sahihi na kwa wakati sahihi kabla ya kuidhinisha hayo matumizi ya pesa? Jibu unalo wewe msomaji. Kama ofisi ya CAG itafanya kazi yake vizuri basi tutegemee kashfa nyingine nzito zaidi zitakazowakumba hawa madikteta wetu wa CCM.
  3. Si watendaji wote wa serikali wanaoridhishwa na utendaji wa serikali ya kikwete, watu wamekata tamaa. Na hili limejidhihirisha baada ya kupiga kura. Watu wachache sana wamejitokeza kupiga kura ukifananisha na idadi ya watu waliojiandikisha, researchers hii ni topic nzuri kwenu, Swali ni kwanini watu wengi hawajitokezi kuchagua viongozi wao?. Hivi serikali iliyoko madarakani haijiulizi swali, kwanini kipindi cha karibuni kumekuwa na leakage ya sensitive information? Baadhi ya nyaraka za vikao vya siri zimewekwa hadharani siku za hivi karibuni na hii tabia tutaendelea kuiona hata katika serikali ya awamu yake ya pili. Na safari hii huenda ikaja kwa kasi ya ajabu sana, nasema hivo kwa sababu kuna watendaji ambao hawaridhishwi na utendaji kazi wa serikali lakini hawataki kujionesha hadharani " OGOPA KUPAMBANA NA ADUI YAKO AMBAYE UNAMTUMIA KUFANIKISHA MAMBO YAKO BILA KUJUA"

MWISHO KABISA NAHITIMISHA KWA KUKUPA SLOGAN YA "INSIDE OUT" NIKIWA NA MAANA ANGUKO LA CCM LIMEANZIA NDANI YA CHAMA KUTOKANA NA AINA YA WATU WALIOKO NGAZI ZA JUU KUKOSA HEKIMA NA BUSARA. KILICHOWAJAA NI TAMAA YA PESA NA KUSAHAU MASLAHI YA TAIFA!
 
Kuna ile posti inayosema, 'Ushindi wa Kikwete ni shubiri kwa ccm' iliongelea jambo kama hili. Nimejaribu ku search bila mafanikio.
 
Sisi m hawawezi kubadilika maana wanahakika ya ushindi wa mezani milele.

Kwanza Pole kwa maswahibu,
ushindi wa mezani unakikomo chake,kama ule uliotokea kule Mwanza nyamagama na ilemela.
tusikate tamaa mapema tuendeleze mapambano mpaka dunia ielewe umuhimu wa raia kupiga kura na wao watoe pesa kwa ajili ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom