Habari watumiaji wa jamii forum;
Nimekuwa nikifatilia kwa karibu sana mijadala mingi kuhusiana na uteuzi wa ndugu yetu Paul Makonda kuwa mkuu wa wilaya na baadae mkuu wa mkoa wa dar es salaam.
mimi binafsi kwanza napongeza kwa dhati kabisa uteuzi huo uliotukuka,Paul Makonda ni kijana mwenzetu hivi kwanini tunamchukia? Kwanini tunasema hafai?Je ninani anayefaa? kwanini kijana usimpongeze kijana mwenzako anaposimama, mimi ni miongoni mwa watu ninayependa utawala wa kizazi kipya, napenda vijana wachapakazi kama makonda, makonda ni mwanasiasa aliyeiva kisiasa hata hivyo makonda siyo malaika kwamba hatakosea, Vijana ebu naombeni tumsapoti makonda, huenda kati yetu kuna watu wanaweza zaidi ya makonda lakini hoja ni kwamba makonda ndiye aliye onekana hatuwezi kuteuliwa wote jamani! Onyesha uwezo wako na wewe uteuliwe? Hata vijana tukinuna haitasaidia kitu jaman, Tuonyeshe ushirikiano wetu kwake.
HISTORIA YA MAKONDA
Makonda amekuwa kijana wa mfano wa kuigwa, ni mchapakazi, sifa kuu za makonda si mwoga,
1. anaujasili wa kusimamia hoja na akaitetea, vijana wengi hawana sifa ya ujasili.
2. Anaheshimu na kuthamini wakubwa.
3. Ni mtu wa ibada, huenda ndiyo maana Mungu anamnyoshea.
4. Ni mtu ambaye hana hila na kinyongo kwa wengine,ni mtu anaependa wengine wafanikiwe.
5. Makonda hapendi dharau na manyanyaso- kwa sifa hii hapo ndipo watu huwa wanamfikilia vibaya, ila hakuna mtu yeyote anayejitambua akakubari kudharauliwa. Makonda hapo alipo ni Taasisi kamili kuna watu wanachanganya umri na Uongozi, mimi namtizama makonda kama kiongozi lakini kuna watu wanadharau sana, Wao Humtizama makonda kama bwana mdogo tu na anapowajibu kama mkubwa hapo ndipo wanaanza kumuona mbaya, mnafiki, mbeya,kiherehere n.k
6. Makonda siyo kigeugeu kama vijana wengine kama kina HAMPHREY, wanauwezo lakini hawana misimamo hawaminiki, Makonda anaaminika siyo kigeugeu.
Hayo ndiyo niyaonayo kwa makonda, na ninaimani sana na Paul makonda kwakweli; makonda ndiye kijana pekee aliyejitokeza kuonyesha anakerwa na mafisadi kuongoza nchi hii, ni kijana gani ambaye angeweza kuthubutu kumsema lowassa ndani ya CCM? Bofya hapa ujikumbushe
Hivi nani aliyewahi kujiuliza endapo LOWASSA angeshinda urai nchi hii kupitia UKAWA,Je makonda angekuwa na maisha gani?Makonda alijitoa kwa maslahi ya chama na taifa, sasa kwanini asineemeke kwa muhanga huo? Makonda mimi binafsi namkubali sana, sijui wengine mnatumia vigezo gani kumponda.Acheni ushabiki wa chuki binafsi, Kuna mtu aliniambia, yaani simpendi makonda, nikamuuliza hebu nitajie sababu japo tano tu kwanini humpendi makonda, Hakuwa na cha kunijibu zaidi ya kusema, basi tu simpendi, jamani Tusishabikie kila kitu kutoka kwenye baadhi ya magazeti, mengine yana ajenda zake bnafsi tusifuate mkumbo, Vijana tuoneshe upendo kwa mwenzetu huyu mteule, tumpongeze, na naamini yupo tayali kupokea ushauri wetu.Nina imani sana na Makonda kwakweli.

PONGEZI KWAKO MAKONDA MUNGU AKUBARIKI SANA