Zijue Sifa na Majukumu ya Mkuu wa Mkoa kisheria hapa Tanzania

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Wakuu,

Leo ningependa kutoa darasa muhimu kuhusu sifa na vigezo vya mtu kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Tanzania.

IMG_6048.JPG


Tuanze kwa kutazama majedwali haya na ufafanuzi wake (kwa kiswahili) utafuata..

3780cf4d750376f37e296aa483457705.jpg


*Wizara ya TAMISEMI imehamishiwa Ofisi ya Rais.
_________

SEHEMU YA KWANZA: KUHUSU MKUU WA MKOA

- Ni sehemu ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

- Ofisi za Mkuu wa Mkoa zitakuwa kwenye Makao Makuu ya Mkoa husika

- Mkuu wa Mkoa atawajibika chini ya Waziri wa TAMISEMI

2. DHIMA YA KAZI HII

Kuhakikisha kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanapatikana kutokana na huduma bora za ushauri na uratibu ambazo zinajenga mazingira bora kwa Serikali za Mitaa na wadau kutoa huduma inayotarajiwa.

3. MAJUKUMU NA KAZI ZA MKUU WA MKOA

- Kuhakikisha uwepo wa Haki na Sheria kk mkoa

- Kuongoza na kusimamia operesheni za Maafa na Kufariji

- Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC), Mkuu wa Mkoa atawajibika kufanya jitihada za kuhakikisha kutimizwa kwa sera za serikali juu ya Mkoa husika.

- Kufanya yale yote yatakayosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mkoa kwa ushirikiano na serikali za mitaa.

4. ELIMU

Mkuu wa Mkoa itampasa awe na Elimu Ngazi ya Shahada(Degree) au inayoshabihiana na hiyo kutoka kwenye Taasisi ya Elimu inayotambulika.

5. UELEWA

Mkuu wa Mkoa atapaswa awe ni mwenye ufahamu kuhusu Utawala wa Sheria, Utawala bora, Kanuni za Haki Asilia (Natural Justice), Sera na taratibu zake, Uongozi na Utawala pamoja na masuala yote ya msingi ktk utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.

6. UJUZI

Kimsingi Mkuu wa Mkoa anapaswa kuwa na stadi zote za uongozi;

Ujuzi wa kujenga umoja, ujuzi wa kutatua changamoto, ujuzi wa kutoa ushauri nasaha, ujuzi wa maridhiano, ujuzi wa kuhimili msongo/mihemuko, sambamba na ujuzi kuhusu mahusiano ya umma na uwezo wa kuzungumza vizuri mbele za watu.

7. SIFA BINAFSI

Aonyeshe uwezo wa kutunza siri, kufanya maamuzi yenye tija, kufanya kazi pasipo mashinikizo, uelewa kuhusu mwenendo wa siasa na tamaduni za jamii, awe na heshima, mbunifu, mtenda haki, bila kusahau kuheshimu miiko ya kazi.

8. UZOEFU

Ni lazima Mkuu wa Mkoa awe ni mtu mwenye uzoefu kuhusu masuala ya utawala/siasa usiopungua Miaka 10.

9. MSHAHARA

Mkuu wa Mkoa atalipwa kiwango cha mshahara kwa taratibu zilizoainishwa na Ofisi ya Utumishi (kwa sasa salary scale yake ni LSS(P) 4).

Asanteni.
 
FB_IMG_1493573532596.jpg
FB_IMG_1493573549632.jpg
Kwamjibu wa Taratibu, kanuni na miongozo ya Jamhuri, Rais anaamriwa kumteua mkuu wa mkoa mwenye Degree.

Unaweza kujionae hapa, hizi ni taratibu za Tanzania sio za Ulaya wala China, mpeni taarifa Waziri dada yangu Mh Kairuki kwamba amekwaza na kudhihaki taifa.

Qualifications za Ukuu wa Mkoa hizi hapa chini... Pia wale ambao mmesikiliza mahojiano ya Waziri Mkuu mstaafu Mh Fredrick Sumaye na Idhaa ya Kiswahili ya DW mtakubaliana nae kwa namna alivyofafanua kwamba yeye akiwa waziri mkuu alishiriki kuweka utaratibu huu kuwa sheria, kwamba mkuu wa mkoa angalau awe na elimu ya ngazi ya degree, sio kama ambavyo taifa linadhalilishwa na Waziri Kairuki kwamba sharti ajue kusoma na kuandika tu!..

Na Yericko Nyerere
 
Back
Top Bottom