Zijue sababu za kwa nini tunazima simu ndege inapotaka kupaa na kutua

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
05b3d880-5eac-11e6-82a1-e6803dbb30ea_1280x720-660x400.jpg

Najua kama ni mtumiaji wa usafiri wa ndege utakuwa umekutana na taratibu za abiria kuzima simu wakati ndege inataka kupaa na kutua ila huenda ikawa hufahamu ni kwanini haswa unatakiwa kufanya hivyo, na inawezekana ulishajiuliza pia ina maana usipozima unaweza kusababisha ndege kupata ajali? jibu ni Hapana, isipokuwa unaweza kusababisha muingiliano wa mawasiliano kati ya rubani na waongozaji.

Vibrations au miungurumo ya simu na vifaa vingine vya electronics vinahusika kwa kiasi kikubwa kuvuruga mawasiliano mazuri kati ya rubani na wanaomuongoza, hivyo huwa tunashauriwa kuzima simu na vifaa vingine vya electronics wakati wa kupaa na kutua kwa ndege. Hiyo ni moja kati ya sababu kuu zilizotajwa kuhusiana na swali la ”Kwanini tuzime simu wakati ndege inaporuka na kutua”?
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi hakuna kitu kama hicho kwani unaruhusiwa kutumia
Airplane mode ukiweka haina shida
Tangu Android na iPhone zimeingia ni kawaida kutumia
Na kuna mda ukiwa angani kabisa unaruhusiwa kutumia bure kwa masaa 2 kama kutuma msg na e-mails kupitia Wi-Fi baada ya hapo unalipia
Hizi ni long haul flights
 
watu wanapenda sana ushahidi aisee!hata zamani ukimwambia MTU umekula pilau anakubishia sana ndio maana tuliamua kubakiza punje kadhaa mdomoni na kuhakikisha hazidondoki kwa gharama yoyote kwa sababu ya ushahidi N;B mm sio muhenga kiviiileee
Wakat mwingine unagoma kunawa mikono ili wenzio wanuse mikono yako na kuzibitisha kama umeminya pilau kweli.
 
Back
Top Bottom