Zijue sababu za kinywa kutoa harufu mbaya

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
20210201_141424_0000.png
Kinywa kutoa harufu mbaya huweza kuwa kero kwako binafsi au kwa watu wanaokuzunguka.

Visababishi vya harufu mbaya kinywani ni kama vifuatavyo:-

Aina ya vyakula

Vyakula jamii ya vitunguu, tangawizi, na viungo vingi vinavyotumika kwenye chakula endapo vitameng'enywa na bakteria katika kinywa huleta harufu mbaya ya kinywa.

Kutosafisha kinywa

Kama husafishi kinywa kwa dawa ya meno na kusukutua mdomo haswa baada ya kula wakati wa jioni, utapata harufu mbaya mdomoni kutokana na vyakula hivyo vinavyobaki kinywani kuozeshwa na bateria pamoja na vimeng'enya.

Vyakula mara nyingi vikibaki kinywani hutengeneza ukuta kuzunguka meno na ulimi na kuta hizi ni chakula kizuri kwa bakteria waliopo mdodomoni. Bakteria wanapokula kuta hii husababisha kuzalisha kwa tindikali na harufu mbaya mdomoni

Mdomo kukauka

Mate husaidia kuosha mdomo dhidi ya mabaki ya chakua na harufu, endapo mtu ana midomo iliyokauka, kwa kukosa unyevu wake atapata harufu mbaya.

Midomo kukauka hutokea sana wakati wa usiku kama asili ya maumbile ya binadamu na hivyo mtu kuamka na harufu mbaya kinywani wakati wa asubuhi. Tatizo la harufu mbaya kinywaji huzidi endapo mtu amelala kinywa kikiwa wazi.

Aina ya dawa mtu anazotumia

Baadhi ya dawa huwa na kemikali ambazo zikivunywa kinywani au tumboni husababisha mtu kuwa na harufu mbaya kinywani. Na baadhi ya dawa pia hukausha mate.

Maambukizi kwenye kinywa

Mtu akiwa na maambukizi kinywani huweza kutoa harufu mbaya. Maambukizi haya yanaweza kuwa kwenye vidonda vinavyotokana na upasuaji, kutolewa jino, kuoza kwa meno au magonjwa mengine ya koo na pua kama tonsil n,k

Saratani, magonjwa ya kimetaboliki na tatizo la kiungulia huweza kusabaisha kinywa kutoa harufu kali sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom