Zijue nchi 20 tajiri Afrika-Tanzania pia ikiwemo hongera

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
ZIJUE NCHI 20 TAJIRI AFRIKA.jpg

1.Afrika Kusini
Pato la Taifa ni dola bilioni 576.1
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 47,190

2. Misri
Pato la Taifa ni dola bilioni 534.1
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 14,877

3. Nigeria
Pato la Taifa ni dola bilioni 521.8
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 32,386

4. Algeria
Pato la Taifa ni dola bilioni 272.5
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 192,500

5. Morocco
Pato la Taifa ni dola bilioni 168.9
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 19,160

6. Angola
Pato la Taifa ni dola bilioni 123.1
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 37,940

7. Sudan
Pato la Taifa ni dola bilioni 112.552
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 202

8. Ethiopia
Pato la Taifa ni dola bilioni 109
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 3,382

9. Tunisia
Pato la Taifa ni dola bilioni 104
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 7,198

10. Ghana
Pato la Taifa ni dola bilioni 82.65
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 8,113

11. Libya
Pato la Taifa ni dola bilioni 76.52
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 120,900

12. Kenya
Pato la Taifa ni dola bilioni dola 53.40
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 5,541

13. Cameroon
Pato la Taifa ni dola bilioni dola 48.14
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 3,353

14. Tanzania

Pato la Taifa ni dola bilioni dola 41.33
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 4,758

15. Jamhuri ya kidemokrasia kongo
Pato la Taifa ni dola bilioni dola 32.69
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 5,239

16. Botswana
Pato la Taifa ni dola bilioni dola 29,707
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 7.993

17. Equatorial guinea
Pato la Taifa ni dola bilioni dola 26,147
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 4,027

18. Gaboni
Pato la Taifa ni dola bilioni dola 24,571
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 2,470

19. Mauritius
Pato la Taifa ni dola bilioni 19,270
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 3,919

20.Namibia
Pato la Taifa ni dola bilioni 25,743
Akiba ya fedha za kigeni ni dola milioni 2,267

WA-DANGANYIKA UCHUMI MUNAO MUNAUKALIA. TANZANI NI NCHI TAJIRI

KATIKA BARA LA AFRICA
 
Sidhani kama takwimu hizi ni current....Tanzania tupo 50 plus sasa hivi. Lakini utajiri haupimwi kwa kias cha GDP, na ndiyo maana utaona Botswana iko chini ya TZ lakini ukifika Botswana wananchi wana maisha mazuri zaidi. Pato la kila mtu Tanzania ni dola 1000 kwa mwaka tuko nyuma sana. Zambia wako juu ya Tanzania, japo kuna kila dalili hapo mbele tunaenda kuwa nchi tajiri sana hapa Afrika.
 
Unajua ukipima utajiri wa nchi kwa vigezo unavyotaka ww unaweza kujikuta ww ni tajiri sana. Hili liko hata katika level ya mwananchi mmoja mmoja, ukichukua mali mtu alizonazo kama viwanja, mashamba nyumba hata mifugo kwa wenzetu wafugaji ukaongeza na kiwango cha fedha ulizonazo kuweza kumudu mahitaji yako kwa miezi zaid ya sita, basi ww ni tajiri kwa mujibu wa definition uliyoleta mtoa mada.
Lakin je ni kweli? Hilo pato la taifa umetoa madeni tuliyonayo? Je umezingatia kuwa hiyo foreign reserve ni ya kucover miezi minne tu? ukiweza hayo mambo utaconclude kuwa sis bado ni masikin.
Me nadhan definition ya utajiri ni ziada uliyonayo ukitoa madeni pamoja na uwezo wa kujikimu kwa asilimia kubwa ya mahitaji bila kutegemea nguvu kutoka nje.
Kwa nin? Sababu nchi zilizoendelea zimejenga mazingira kwamba ni lazima uwe na fedha za kigeni ili upate mahitaji usiyoweza kuzalisha nchin mwako, ili kuhalalisha kutuuzia bidhaa zao hiyo kuendelea kuondoa umasikin wa watu wao, lakin ukweli ni kwamba hizo ni takwimu tu wao wanaweza kujihudumia kwa karibu kila kitu ukiacha rasilimali kama mafuta.
Sis hata ziada ya chakula kwetu ni tabu, mvua zisiponyesha kwa miezi sita mfululizo ni balaa
 
Kama hivyo ndivyo ni kwanini wanasema USA ndiyo nchi tajiri Duniani wakati kwa kutumia vipimo vyako hata top 10 hapa Duniani USA haingii?
 
Kama hivyo ndivyo ni kwanini wanasema USA ndiyo nchi tajiri Duniani wakati kwa kutumia vipimo vyako hata top 10 hapa Duniani USA haingii?
Kwa nin mkuu? Marekani inaweza kujitegemea kwa almost kila kitu, najua unataka kuongelea trade deficit, hizi nchi za watu weupe ni wajanja sana, wana akili nyingi tofauti na tunavyofikiri, hiyo wameitengeza kwa sababu mbali mbali ikiwemo kulinda madeni yao kwa nchi wanazozidai either direct or indirect. Yan kwa mfano kama mm ni tajiri na nakudai ww masikin kwa fedha nilizo kukopesha ufanyie mambo flani, ili nisipoteze sana ukishindwa kulipa basi natengeza mazingira na ww unidai hata kupitia rasilimali zako ambazo sio fedha. Hivi hujajiuliza kwa nin Japan mojawapo ya nchi zenye trade surplus kwa muda mrefu, lakin ndio nchi mojawapo yenye deni kubwa sana, wale sio wajinga hata kidogo.
 
Hiyo Angola juzi kati nimeiona kwenye nchi masikini leo tena ni tajiri,hawa wazungu wanatufanya mazezeta kweli yaani wanatugeuzageuza kadri watakavyo kwa kutuletea tafiti za uongo nasi tunazibeba na kudanganyana
Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo nayo je!Mi nadhani itumike human development index na sio gross domestic product.
 
Naombeni mnisomee namba hii-Dola million 120,900. Dola milioni laki moja na elfu ishirini na Mia tisa?? Hapana
 
Pato la taifa hapo limepimwa kwa kuangalia GDP yaana mapato toka sector zote. Sasa ukiangalia nchi zinazoongoza ni zile zinazozalisha mafuta na madini lkn sehemu kubwa ya wazalishaji ktk sector hizo ni wazungu kwa hiyo impact ya uzalishaji inakuwa nje lkn wananchi wa Africa wanabaki maskini mfano mzuri Nigeria ni wazalishaji wakubwa wa petroli lkn wananchi wananunua petrol kwa bei kubwa sana.
 
A country may have high GDP/PER CAPITAL INCONE but poor in Economic development. That is to say, GDP is not a good measure of Economic development as GDP don't include everything. Hahahaaaa hizo ni theory za UCHUMI jamani, acheni hasira. India INA GDP/PER CAPITAL INCOME kubwa sana lakini wananchi wake in masikini hatari.
 
Back
Top Bottom