Zijue mbinu 5 za kumtongoza msichana yeyote mrembo hadi akubali

MKALI W MAMBO

Senior Member
Aug 9, 2018
190
135
Habari za jumatano poleni kwa kugombea Usafiri wa Daladala Asubuhi ya leo.

Je, unamtamani msichana mrembo ambae kwa sasa ni kama marafiki? au unavutiwa na yule demu unayemuona kila siku mtaani na unashidwa kujizuia sema hujui uanzaje? Haijalishi kama unamjua au hamjuani, ila inapokuja kwenye kumtongoza mwanamke unachotakiwa kujua ni uelewa wa vitu kadhaa kuhusu jinsi kutamani kunavyokua na jinsi ya kufanyia kazi ili ufanikiwe .

Kumtongoza demu na vitu unavyotakiwa kujua

Kwanza kabisa kama unataka kumtongoza msichana au kumfanya tu akupende tu, inabidi uwe mtu poa ambae anaweza kuvuta macho ya wasichana.

Kama hautaweza kua mtu anayeweza kumvutia msichana kirahisi, utakua bado unauwezo wa kumtongoza mwanamke unayempenda lakini itakua ngumu kuwezesha yeye akukubali .

Kiufupi fatisha njia hizi 11 rahisi na kiukweli kabisa utakua vizuri katika kutongoza na hata kwa mambo mengine yatakayofuata baada ya hapo.

Tumia njia hizi moja baada ya nyingine na ijapokua utacheza karata zako vizuri basi lazima umpate mrembo yoyote unayemtaka hata kama kuna watu wengine kibao wanamfukuzia .

1 . Kua karibu nae

Siku zote , kama unataka kumtokea msichana njia muhimu kabisa ni kuweza kumjua kwa undani .Usikurupuke kurupuke tu ukaanza kutongoza , msichana ataogopa au atakuona mtu rahisi kua nae na mwisho wa siku utaishia kumboa tu .

Ongea nae na upate kumjua vizuri. Mtumie message na usiwe na mzuka, mfanye awe kama rafiki kwanza. Usimtokee kwanza sema pia usisubiri sana maana ataanza kukuchukulia poa .

2 . Kua mtu unayependeka

Hii ni hatua muhimu sana. Na huu ndio wakati utagundua kama anahisia na wewe kweli au anakuchezea akili . Pia unapoongea nae mara kwa mara jaribu kugundua vitu anavyovipenda. Jaribu kuweka ukaribu nae kwenye kitu ambacho wote mnakipenda.

3 . Usilale Usiku

Ndio maana mitandao mingi ya simu ikawapa ofa za usiku watu kama nyie muongee usiku kucha . Usiku ndio muda sahihi wa kuweza kutoa ya moyoni na kueleza hisia zako kwa msichana. Anza kwa kuweka maongezi ya kawaida na kadiri unavyoendelea weka vionjo fulani vitakavyomfanya aanze kuingia line bila kugundua kama unamtokea.

4 . Ishi Maisha mawili

Unapoongea nae usiku, mwaga sera zako na funguka kuhusu mambo ya mapenzi sema mkikutana ana kwa ana mchana usiongelee mambo ya mapenzi kabisa labda aanze yeye na hivyo kumaanisha ashaingia line na anapenda maongezi hayo.

Pia epuka kuongelea kuhusu mambo yenu ya kimapenzi mnapokua na marafiki wengine bali fanyeni hivyo mkiwa wawili . Kwa kufanya hivyo unamfanya aamini kuna uhusiano motomoto wa siri unapikika kati yenu.

5 . Usimfanye ajue unampenda

Wanaume wengi ufanyaga kosa hili kubwa. Wanawaambia wanawake wanawapenda au wanahisia za kimapenzi kwao . Ni kweli unampenda , anajua hivyo tayari. Au hajui? Unampigia simu kila saa, mnataniani kimapenzi na anaona uhusiano wenu kabisa.

Kwahiyo japokua anahisi unampenda, usije kuonyesha hivyo kwani anahitaji kusikia kutoka kwako ili ajihakikishia hisia zake. Chukulia poa na usifunguke kuhusu hisia zako kwake, kitendawili alichonacho ndicho kitamfanya azidi kukunata na kutaka kujua mwisho wa mambo .

Ni hayo tu...Asubuhi njema
 
Dah! kuongea naye usiku kucha!!!! Aisee katika vitu ambavyo huwa siwezi ni kuongea na mtu yeyote yule kwa mda mrefu yaani mwisho ni nusu saa tu mbali na hapo kichwa hugonga sana mkuu!

Harafu mbona hujaweka njia ya kuwa na pesa au bado zinaendelea!!
 
Hizi mbinu zilifaa enzi za Joji Pojy zile.
Kipindi shiva jero jero na tigo extreme pack kabla ya ujio wa internet za simu nchini.

Sahivi watu wanatongozana whatsapp kwa emoji tu mchezo kwisha!

Chupi zimekuwa cheap mitandaoni, unahitaji MB100 tu na hela ya kula na guest tu kupata demu!

Ukiwa na kazi na usafiri tu kitaa mademu wanajitongozesha wenyewe!
 
Labda kwa watoto wanao anza mapenzi mimi natumia mbinu hii
1.nampa pesa
2.nampa pesa
3.nampa pesa
2.nampa pesa
nampa pesa
2.nampa pesa

Nasijawahi kumkosa mwanamke yeyote
 
Hii ni nadharia tu na inafuatana na wanawake unakutana nao. Pesa sio na upendo, ila ni catalyst tu. In this case, Catalyst (money) speeds up the reaction of love but itself weakens as reaction continues. So, to keep the reaction going, one has to keep adding the catalyst(money). This violates the MOU Of love. Ni mtazamo wangu tu.
Labda kwa watoto wanao anza mapenzi mimi
Natumia mbinu hii
1.nampa pesa
2.nampa pesa
3.nampa pesa
2.nampa pesa
nampa pesa
2.nampa pesa

Nasijawahi kumkosa mwanamke yeyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikiza niwaambie mwanamke yeyote anaejielewa anaenda kwa Mwanamme mwenye status.

Women love dangerous, smart young men (pigania sana upate status flan reasonable)

Hela sio kiviiile ingawa ni mbolea kwenye mapenzi ku accomodate/facilitate show za 6 by 6

Ila kuna watu wanang’oa madem wakali na hawajawahi tumia hata cent.

Status ya mwanamme ndio inamfanya akubalike au akataliwe.
 
Mimi nakupa mbinu 7 za kumpata sholi mkali zilizo fanyiwa research kabisa
1.Mpe hela

2.Mpe hela

3. Hujanielewa, nasema mpe hela

4.Wewe mpe hela tu

5. Usichoke kumpa hela

6. Brother, mpe hela

7. Namalizia kwa kusema, mpe hela unampata kabla ya saa nne asubuhi.
 
Hii namba 3 kwanza sijaielewa mana mademu wengi hawataki uwapigie usiku sababu ana vidume wengi inawezekana mida hiyo kaenda kulala kwa Jafar, hapo si ndo ataona unamzingua kabisa.
 
Mpaka sahivi nimegadhabika! Yani nisilale!!! Huyo mwanamke wa kunifanya nisilale nihangaike nae ati kuwasiliana tu hili siwezi kilivumilia labda kama sina usingizi,wanawake wa Leo nikujisumbua bure tu... Nimegadhabika mkuu hilo la kutokulala futa.
 
Ukimtongoza akikataa muache tafuta mwingine mapenzi haya lazimishwi ipo siku na yeye atapanga foleni kusubiri Upepo wa kisulisuli na atajikuta hata huo upepo amesha uchelewa tayari.
 
hayo yooote ya nini Nambie Ukweli unachotaka ndoa au muonjano baaasiiiii!! jibu utapata! ukikataliwa sepa mbele huko! tena fastr tu na sahau!
 
Wanawake wa leo ni watu wa hovyoo....ukiyafuata hayo juu mwanamke ataishia kukuumiza kumoyo...tafuta pesa ujipange na ujijenge kwa ajili ya maisha yako ya baadae.....
 
hayo yooote ya nini Nambie Ukweli unachotaka ndoa au muonjano baaasiiiii!! jibu utapata! ukikataliwa sepa mbele huko! tena fastr tu na sahau!
Ndoa bila kuonja, hivi inawezekana kweli siku hizi? Enzi za mababu sawa....
 
Back
Top Bottom