Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
WENTSWORTH Resources, awali ikijulikana kama Artumas, ni kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa mafuta na gesi Afrika Mashariki. Kampuni hii imesajiliwa kwenye masoko ya hisa ya London na Oslo.
Kampuni inaendesha shughuli zake kwenye eneo la Mnazi Bay nchini Tanzania na kitalu cha Rovuma kilichoko nchini Msumbiji.
Hata hivyo, kampuni ya Wentsworth na washirika wake wanaendesha utafiti kwenye eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 12,700 kwenye bonde la Rovuma kusini mwa Tanzania na Kaskazini mwa Msumbiji.
Soma zaidi hapa => Zijue kampuni zilizowekeza katika mafuta na gesi Tanzania (11) – Wentworth Resources | Fikra Pevu