Zijue faida ya kutumia tunda la mkoma Manga

Bedui la bongo

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
297
306
1.Lina uwezo mkubwa wa kuzuia ugonjwa wa kansa

2. Linasaidia kukinga magonjwa ya moyo

Lina uwezo wa kuondoa Cholesterol mbaya ijulikanayo kama (LDL) na kuongeza Cholesterol nzuri ambayo haina madhara mwilini, ijulikanayo kama (HDL), hii husaidia kuondoa kasi ya kupata kansa.

Juisi ya komamanga inasaidia kwa kiasi kikubwa damu kutembea na afya ya mwili kwa ujumla.

3. Huupa afya mshipa wa moyo wa Arteries

4. Husaidia kurekebisha presha ikae sawa.

5. Husaidia kuimarisha mfumo wa meno kinywani, kwa wale wenye tatizo huwa linaondoka kwa kula sana tunda hilo.

6.Komamanga husaidia pia kutokomeza ugonjwa wa kuharisha, kwa mtu anayeharisha akitumia juisi yake anapata nafuu.

7. Husaidia kupunguza uzito na kukuweka sawa.

8. Huongeza hamu ya kula.

9. Husaidia usagaji wa chakula mwilini.

10. Hutibu ugonjwa wa kupungua kwa damu mwilini.



Sent using Jamii Forums mobile appiphone
 
Mkoma Manga ni adimu Tanzania kuyapata kwa bahati kubwa hayauzwi ovyo kama machungwa na maembe.
 
Mkuu hujatafuta tu yapo mengi

Sent using Jamii Forums mobile appiphone
IMG_20190106_001608.jpg

Dar hayaunzwi hovyo kukutana nayo sokoni bahati.
 
Eneo ninaloishi mimi yamejaa sana yanaishia kuharibiwa na watoto tu na ule uchachu (radha yake mbaya) linafanya likose wafuasi.
.
Ahsante kwa kutujuza faida zake nianze kuilinda japo simjui muhusika wake.

Mkoma manga mchachu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom