Zijue faida na mapungufu ya chanjo ya kansa ya shingo ya kizazi

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
KANSA ya kizazi husababishwa na virus vijulikanavyo Kama human papilloma.
Hivi virus huathiri viumbe vilivyo kwenye jamii ya wanyama na kila aina ya virusi vina aina maalum ya mnyama vinayemwathiri.
Virusi hivi huwa viko wazi na havipasui chembe vinapoingia ndani ya chembe

Yapo makundi makuu ya virus hawa wanasababisha kansa ya kizazi na kansa zingine kwa binadamu kama.kansa ya koo na kansa ya uke na uume

Makundi haya ni low risk human papilloma virus na high risk human papilloma virus
High risk hujumuisha aina kama 16, 18, 31, 33 na 45 na hawa ndio wanasababisha kansa ya shingo ya kizazi. Pia wapo low risk kama aina 6 na 11 ambao mara nyingi husababisha condylomas
Hawa wote huambukizwa kwa njia ya kujamiiana ikiwemo njia ya mdomo ambayo wanasayansi wengi huamini inaweza kusababisha kansa ya koo pia isabishwayo na hpv.
Pia husababisha ugonjwa au kuota kwa papilloma ambazo zikiwa kwenye ngozi tunaziita warts na zikiwa kwenye sehemu za siri tunaziita condylomas

Chanjo ikoje?
Chanjo iliyopo Gardasil inaweza kuzuia aina 6, 11, 16 na 18. Gardasil inaweza kutumiwa na wasichana na wanawake kuanzia 9- 26 na hutolewa kama dozi tatu ndani ya kipindi cha miezi sita. Tafiti za umuhimu wa chanjo kwa wanawake zaidi ya miaka 26 na wanaume zinaendelea
Mapungufu ya chanjo hii, haifanyi kazi kwa mwathirika wa virusi hivi, inafanya kazi kwa uthabiti ndani ya miaka mitano Na inatoa kinga kwa hizo aina nne nilizotaja ambazo ni 6, 11,16 na 18

Chanjo nyingine iliyotengenezwa na kampuni hii, GlaxoSmithKline (GSK). Jina la chanjo ni, Cervarix™, ni bivalent L1 VLP dhidi ya HPV aina 16 and 18, ingawa GSK wanadai inaweza kulinda dhidi ya aina 31 and 45 pia (Harper et al., 2004). Chanjo imeonyesha ulinzi imara ndani ya miaka 4.5 baada ya chanjo (Harper et al., 2006).
Cha msingi hapa kujua ni kwamba chanjo haina uwezo wa kulinda dhidi ya aina zote na kikubwa inachofanya ni kupunguza hatari.
Tukipata chanjo tusijisahu na kujiachia kwa kuwa na makoloni na michepuko ya kutosha.
Pia kumbuka huwezi kuvaa kondom mdomoni kwa hiyo hatari bado ipo.

Hawa ni naked virus maana yake wanaweza kupita njia ya chakula bila kuathiriwa na tindikali za njia ya chakula.
unaweza jua mtu ana hpv kwa kuangalia warts kwenye ngozi na sehemu za siri. Maana yake ni vyema kukagua na
Njia nyingine bora ya kuondoa hatari kwa mama zetu na dada zetu ni kupima kila baada ya miaka mitatu pap smear. Hii imeonyesha faida kutokana na tafiti nyingi zilizofanywa. Zipo hatari kadhaa za kipimo hiki lakini faida ni nyingi

Nawasilisha na unaruhusiwa kunikosoa ili watanzania wengi wanufaike na bandiko hiki kwa kupata habari sahihi na kweli
 
Uzi mzuri Sana mkuu,
Nadhani wanaume ni careers wa HPV.
Hivi mkuu mwanamke akishapata warts hakuna namna HPV unaweza kutibiwa au ndo bas tena?
Hiyo Vaçcine unayozungumzia nadhani hata Sanofi wanayo.....
 
Asane kwa complement mkuu
Mtu akipata whether mwanamke unaweza kutibu external kwa laser na caustic. Yaani njia kubwa na kuziondoa hizo warts
Kwa mwanaume na mwanamke pia inapokuwa kooni au kansa ya koo inayosababishwa na hpv njia ni operation tu

Uzi mzuri Sana mkuu,
Nadhani wanaume ni careers wa HPV.
Hivi mkuu mwanamke akishapata warts hakuna namna HPV unaweza kutibiwa au ndo bas tena?
Hiyo Vaçcine unayozungumzia nadhani hata Sanofi wanayo.....
 
Asane kwa complement mkuu
Mtu akipata whether mwanamke unaweza kutibu external kwa laser na caustic. Yaani njia kubwa na kuziondoa hizo warts
Kwa mwanaume na mwanamke pia inapokuwa kooni au kansa ya koo inayosababishwa na hpv njia ni operation tu
Ila Virus mwenyewe anabaki na anaendelea kuambukiza sio mkuu?
 
Kinga yake ni inayopatikana ni humoral. Hii inamaanisha virusi hawa wakiingia wataulizwa. Lakini ni wale waliokusidiwa kama nilivyotaja hapo juu. Wapo wengine wanao weza kuwepo ambao chanjo haina uwezo nao. Lakini ukipata kinga kusudiwa huwezi eneza au kupata ugonjwa ulikwisha chajwa
Ila Virus mwenyewe anabaki na anaendelea kuambukiza sio mkuu?
 
Back
Top Bottom