Zijue baadhi ya sababu: Kwanini hupaswi kumuoa mwanamke askari

Good Father

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
10,275
18,351
Wakuu habari za muda huu.
Nitumie fursa hii kuwapa darasa vijana wenzangu wanaotarajia kua na wachumba au pengine wana wachumba tayari na wanapanga kufunga pingu za maisha.

Huu ndio ukweli kuhusu plan zenu kuwaoa askari wa kike, japo naweza kuwakwaza au kuharibu mipango ya baadhi ya watu lakini ukweli lazima usemwe na hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kwamba hayapo(Mwl. Nyerere).

Niende kwenye baadhi ya sababu ninazoweza kusema hupaswi kumuoa askari wa kike endapo unataka kua na ndoa imara na yenye furaha.

1. Hulka ya askari wa kike ni watu jeuri sana (hilo mnalifahamu sina cha kusema sana).

2. Askari wa kike wengi ni wahuni, kwao kugawa penzi sio tatizo maana wana ujasiri wa mafunzo mpaka ujasiri wa kufanya matendo ya hovyo. Kingine ni vema ukajua kazi ya uaskari ni kazi yenye mazingira magumu na kwa kawaida wanawake hawapendi ugumu kwenye maisha, sasa kinachofuata ni kuliwa na wenye mamlaka ili kupunguza ugumu wa mazingira ya kazi, hapa hutamkuta anapangwa zamu za ajabu ajabu, hutamkuta anakaa mazingira ya ajabu kama kijijini sana, kituo cha ajabu ajabu, utamkuta ofisini, kazi simple simple.

Ukiona hivyo mara nyingi ndo basi tena, ukiona manyoya ujue kaliwa.


3. Endapo utamuoa na ikatokea siku mmekosana basi jua kabisa kesi yenu itahamia kazini na huko kazini kesi yenu itashughulikiwa kwa kutegemea rank zenu na sio kwamba nyie ni mume na mke(endapo wewe na mkeo mtakua wote ni askari).
Sasa kibaya zaidi mkeo awe na rank kubwa kukuzidi nakwambia utashughulikiwa vilivyo, kesi ya kumpiga makofi mkeo itageuka na kuitwa kesi ya wewe kumpiga kiongozi wako wa kijeshi,nakwambia utajuta ndipo utakapotambua mpapai haufai kwa mbao.

4. Kwa nature ya kazi yao ni vigumu kutekeleza majukumu yao kama wanandoa maana ratiba zao hazieleweki, akiitwa kazini saa tano usiku huwezi kukataa maana kaitwa na boss,sasa je wewe una uhakika gani kwamba huo wito ni wa kikazi(halali).

Sikatai, wapo askari wa kike wastaarabu sana tu na wameolewa,ila ukifuatilia asilimia za waliowengi ni matatizo matupu.

Najua sio kila mtu atakubaliana na hili, nami nakaribisha mawazo tofauti maana sio dhambi ila ukweli ninaoufahamu ndio huo hapo juu, wengine matomaso siku yakiwakuta watakumbuka huu uzi, nawahakikishia iko siku baadhi yenu mtasema "Good father" aliwahi kuandika uzi flani tukaupuuza.

Sisemi watu msioe askari,ninachosema hapa ni kuwapa alert mjue kama mnaelekea huko mjiandae vipi kukabiliana na changamoto, kingine akili za kuambiwa changanya na za kwako, ikumbukwe maneno yangu sio sheria.

Naishia hapa najua kuna wenzangu mnajua sababu nyingine mnaweza kuongezea.

NB:Sijataja jeshi lolote wala chombo chochote kutoka nchi yoyote.
Ieleweke kwamba uzi huu ni universal.

Nawasilisha.
 
1. Wewe hakuna unachokijua, uzi wako umekaa kifitnafitna baada ya kutoswa na askari.

2. Uandishi wako wa kudonyoadonyoa pia na umebase upande mmoja wa kuponda umesahau zipo familia za kiaskari nzuri zaid ya raia na maisha yanaenda.

3. Mwalimu Nyerere mtu mzito sana kwenye hili taifa kuliko hata baba yako, lakini umeshindwa kumnukuu vizuri, umechanganyachanganya na ufyoro wako hapo juu kisha unasema (Mwal Nyerere).

Ushauri: Zingatia hivyo vitu hapo juu kisha urekebishe uzi wako
 
Upo sahihi, hii jinsia ya kikee kwenye sector ya ulinz ni matatizo alaf ukutee mwanamke Mwenyewe bombaa ndy kabisaa

Akisema mkuu njoo nyumbani utasikoa ndiyo sir.
Hiyo ni inferiority complex...ukishaanza kujiona unatakiwa kuwa powerful kwenye jambo moja ili uweze kum win mwanamke basi ujue hutaishia kwa askari tu utatoa proposal hata wanawake wenye uelewa mkubwa wasiolewe na kama ukipata kundi la wajinga wanaokushabikia utaenda mbali zaidi... mama yangu ni mwanamke lazima tuwaheshimu na kusimama kwenye majukumu yetu ipasavyo!
 
Hayo ni mapungufu, ila faida zake zipo pia, gari lako haliguswi na trafik tena uwe unampeleka kazini na kumfata jioni utaona raha yake kila trafik anakuita shem,

sio kila askari anakaa doria wapo wahasibu masekretari na maofisa ambao hawaendi doria, hakikisha unamwendeleza kimasomo apate nafasi nzuri kazini

umalaya ni hulka ya mtu wapo masista wanapigwa jiti kama kawaida, sidhani kama vina uhusiano na ajira, anaweza kuwa mama wa home akakuaga anaenda kulala msibani akaishia kuliwa asusa

askari ni wavumilivu kimaisha anaweza ishi mazingira yeyote na muda wowote, ukimwambia dili zimekata tukapange chumba na sebule buguruni hana tatizo,

askari matumizi yao kidogo muda mwingi wanakuwa na nguo za kazi na hawaruhusiwi kujiremba na mekapu za ajabuajabu, yangu ni hayo tu, karibu kwenye mjadala
 
nilikuwa na mke mjeshi alisumbua san mkuu. mpaka nimeachan nae, ilikuwa mbinde kweli! nivile nilikuwa na uwezo kipesa.
Maandiko matakatifu yapo wazi kabisa kwamba mume hatomuacha mkewe ila kwa uasherati,sasa ikiwa hukumkuta kwenye zinaa na kwamba unasimama vizuri kwenye nafasi yako katika nyumba basi ujue sababu uliyoitaja ya mke kuwa mtata nawe utakuwa una mchango wa kumfanya awe venye alikuwa..Pole ila zipo ndoa nyingi tu zenye discipline tunazijua...mlioshindwa msitafute pakuegemea!
 
Huu utafiti wako si utafiti kamili umebase zaidi kwenye mambo ya kufikirika na ya kuhisi ingekuwa tasnifu yako ya elimu ya juu na ukakutana na mhadhiri anayejielewa ungerudia mwaka wa masomo na uje na tittle nyingine!
Silazimishi mtu kukubali hili andiko, you can take it and you can leave it.

Wanaolewa ninachosema wataelewa na wengine yalishawakuta.

We leta drama zako za madesa ukadhani utajua kil kitu, ni vema ukatambua kila mtu ana lake analojua sasa nami hili andiko langu nalielewa vema.
Kama wewe ni professor basi endelea kufundisha au subiri teuzi.

Mkuu alisema mavyeo yako mengi msiwe na wasi wasi.
 
Back
Top Bottom