Zijue athari za kufanya Ngono kinyume na maumbile

Innovator97

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
273
372
Ukiachilia mbali mambo ya imani, leo tuone athari za jambo hili japo kwa ufupi. Sehemu ya haja kubwa huwa na misuli miwili inayofanana na pete, kwa Kiingereza huitwa sphincters, labda kwa Kiswahili kisicho rasmi sana tunaweza kuiita misuli vitanzi.

Miongoni mwa sehemu za mwili zilizo na mishipa mingi ya fahamu ukiondoa kisimi cha uke ni sehemu ya haja kubwa. Mishipa hii ya fahamu hufanya kazi ya kuzisaidia tissue zilizo katika eneo hili ziweze kutofautia kati ya choo kilaini, kigumu pamoja na gesi zinazotolewa.

Kazi nyingine muhimu ya mishipa hii ni kutengeneza utaratibu sahihi wa namna gani haja hii muhimu kabisa ya mwili inatekelezwa na mshusika bila changamoto zozote.

Wingi huu wa mishipa ya fahamu ndiyo hushawishi baadhi ya watu kufanya tendo hili la ajabu kabisa kiutamaduni na kiimani. Turudi kwenye misuli vitanzi ama sphincters, misuli hii huwa ipo miwili yaani mmoja nje na mwingine ndani.

Athari kuu za kushiriki tendo la ndoa kupitia sehemu hii husababishwa na kulegea kwa misuli tajwa na kuathirika kwa mishipa ya fahamu.

Ukiachilia mbali usambazwaji wa magonjwa mbalimbali, athari zingine mbili kubwa ni kukosa udhibiti wa choo (fecal incotinence) na ugumu katika kuacha jambo hili (uraibu).Ikitokea misuli hii umeiharibu sana, choo kitakuwa kinatoka muda wowote bila taarifa yako bila kujali umejiandaa au la.

Ukishazoea kufanya zoezi hili utapata uraibu ambao utakupa wakati mgumu sana kuacha kutokana na wingi wa mishipa ya fahamu ambayo huwa tayari imezoeshwa kufanya kazi isiyo yake.

Kwa wanawake huenda mbali zaidi kwa kuleta fedheha kubwa hasa wakati wa kujifungua mtoto ikiwa Mungu atakusaidia kupata ujauzito (kutoka kwa kinyesi bila mpangilio).

Wenye tabia hii waache na Mungu awasaidie.
 
Miongoni mwa sehemu za mwili zilizo na mishipa mingi ya fahamu ukiondoa kisimi cha uke ni sehemu ya haja kubwa.

Mtoa mada anatuelimisha kuwa hiko kiduara kipo very sensitive.
 
Maneno tu. Usifanye sababu wamkosea Mungu wako na sio sababu kuwa sijui utajinyea
 
Kwa wale watiaji wao vipi? Maana kama kwao haina madhara na kwa vile huwa wanalipa hela kununua Malaya si wataendelea tu hawa kwa kuwa hawaathiriki na hao wanaoathirika hawana issue nao. Ebu wahofishe na wao juu ya madhara wanayoweza pata. Hakuna uwezekano kweli wakuziba kwa urethra kwa kupump kinyesi kwa miaka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom