Zijue ajali kubwa zilizowahi kutokea Tanzania

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,144
15,143
Hizi ndio ajali kubwa 5 zilizowahi kutokea nchini mwetu na kugharimu maisha ya watu wengi katika historia ya nchi yetu.
Chanzo: BBC

Kwa sisi waamini tuendelee kumuomba Mungu atuepushe na ajali hizi zisijirudie tena

5: MV Skagit - 2012
images (3).jpeg

Ajali hii ilitokea miezi 10 tu baada ya kutokea kwa ajali ya MV Spice Islander. Ilikuwa Julai 18, 2012 majira ya alasiri meli hii ya MV SKAGIT ilipozama katika eneo la Chumbe, Zanzibar. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250, watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9.

Wananchi walikumbushwa machungu ya ajali ya MV Spice Islander kwa ajali ya meli ya Skagit iliyoua watu 81, wakiwemo Watanzania 75, Wakenya 3, Waholanzi 2 na Mrundi 1. Aidha, watu 212 walipotea na 154 walinusurika wakiwemo Waholanzi 5, Wajerumani 4, Wabelgiji 2, Wamarekani 2 na Waisraili 2. Kwa mujibu wa ripoti tumwe iliyoundwa kuchunguza ajali hiyo

Chanzo cha Meli hii iliyoundwa nchini Marekani mwaka 1989 na kampuni ya HALTER MARINE kuzama inaelezwa ilikuwa ni kutokana na hali mbaya ya hewa

4: Ajali ya Treni -Msagali - 2002
Dodoma
images.jpeg

Ajali ya treni iliyotkea Msagali Dodoma ni moja ya ajali kubwa za treni Tanzania

Kwenye upande wa ajali mbaya za treni kuwahi kutokea Tanzania hii ni miongoni mwao. Ajali ya treni ya abiria Namba A.12 ilitokea kilomita 388 kati ya stesheni za Igandu na Msagali Juni 24, 2002 saa 2.30 asubuhi.

‘Taifa limekumbwa na msiba mkubwa’ hii ilikuwa sehemu ya taarifa fupi kuhusu ajhali hiyo aliyowasilisha waziri wa uchukuzi wakati huo Profesa Mark Mwandosya, bungeni Dodoma.

Watu 281 walipoteza maisha, maiti 193 zilitambuliwa na kuchukuliwa huku maiti 88 zilizikwa na mamlaka za serikali kwenye mazishi ya halaiki katika makaburi ya Maili Mbili Kata ya Miyuji mjini Dodoma 27 Juni 2002 kutokana na kutotambuliwa.

Inaelezwa treni hi ilikosa nguvu ya kupandisha muinuko na breki kushindwa kufanya kazi kabla ya kuanza kurudi kwa kasi kinyumenyume na kwenda kuvaana na treni nyingine ya mizigo.

3: MV Nyerere - 2018
MV Nyerere
images (2).jpeg

Kivuko cha MV Nyerere kilikuwa na uwezo wa kubeba watu 101 lakini siku ya ajali ilielezwa kujaza watu karibu mara mbili ya uwezo wake

Septemba 2018 jumla ya watu 224 walifariki na watu wengine 41 wakiokolewa wakiwa hai katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

Ilikuwa moja ya ajali iliyoleta kumbukumbu ya ajali kubwa zaidi ya MV Bukoba. Iliyotokea katika ziwa hilo hilo.

Mhandisi wa kivuko hicho Alphonce Charahani alikuwa wa mwisho kuokolewa akiwa akiwa hai baada ya kukaa majini kwa saa 48.

Rais wa wakati huo hayati John Magufuli alipozungumza alieleza kuwa kivuko hicho cha MV Nyerere kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 101, lakini kwa takwimu za miili iliyopatikana na pamoja na manusura, ni wazi kwamba chombo hicho kilikuwa kimebeba abiria wengi kuliko uwezo wake.

2: MV Bukoba - 1996

images (1).jpeg

Hii ni ajali ya kihistoria, pengine ni moja ya ajali iliyoua watu wengi zaidi kwa wakati mmoja kuwahi kutokea Tanzania katika miongo ya hivi karibuni. Ilitokea Mei 21, 1996, na hata Serikali iliwahi kukiri kwamba ajali hiyo itaendelea kuwa miongoni mwa kumbukumbu mbaya kutokana na kuangamiza maisha ya mamia ya Watanzania wengi kwa wakati mmoja.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 800 walifariki katika ajali hiyo iliyotokea kilomita chache kutoka bandari ya Mwanza.

Ingawa ni miaka 26 sasa tangu kuzama kwa meli ya MV Bukoba, Bukoba ilipokuwa inakaribia bandari ya Mwanza umbali wa kilometa 56, aliyekuwepo na asiyekuwepo historia yake imeendelea kukaa vichwnai mwa wengi.

Meli hiyo iliyoundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 iliyokuwa tegemeo kubwa la kutoa huduma ya kubeba mizigo na abiria ndani ya Ziwa Victoria kati ya Bandari za Bukoba na Mwanza. Siku ya ajali inaelezwa kupakia zaidi ya abiria 2,000.

1: MV Spice Islander - 2011

Spice

Pengine kumbukumbu ya muda mrefu ya ajali ya MV Bukoba inapunguza machungu ya ajali ya MV Spice Islanders. Kuzama kwa meli ya MV Spice Islander hapo Septemba 10, 2011 katika eneo la Nungwi, Kaskazini mwa kisiwa cha Unguja, kulileta huzuni kubwa hasa visiwani humo kutokana na idadi kubwa ya watu kufariki.

Kwa mujibu wa ripoti rasmi ya jopo lililoundwa kuchunguza ajali hiyo chini ya Jaji Abdulhakim Ameir aliyeongoza jopo la watu 10, watu 1370 walipoteza Maisha.

Uchunguzi unaeleza ilibeba abiria karibu mara nne Zaidi ya uwezo wake. Ilikuwa na abiria 2,470 wakati uwezo wake ilikuwa watu 620.

Tume iliyoundwa inasema meli hiyo ilibainika kuwa na hitilafu iliyojulikana miezi miwili kabla ya kuzama kwake kutokana na ukaguzi uliofanywa na taasisi ya usalama wa bahari Sumatra, lakini bado meli hiyo ilipewa leseni.
 

Attachments

  • images (2).jpeg
    images (2).jpeg
    36.5 KB · Views: 36
Nimeshangaa leo ndo nagundua kumbe iliua watu zaidi ya buku aisee sikuwahi dhani ilikua kubwa kiasi cha kuizidi MV Bukoba
Haikuwa kubwa ila kama ulivyoandika hapo juu walipakia abiria mara nne kuzidi uwezo wake mixer mizigo.

Yupo jamaa yangu alikuwa na hardware Pemba yeye Twiga cement walimpelekea mzigo wake aliniambia ila sikumbuki vizuri ni kama ilikuwa ton 25 au ton 15 na siyo yeye tu aliyekuwa na mizigo ilikuwa mingi na ilikuwa ni likizo ya mwezi wa tisa kulikuwa na sherehe ya kidini mbeleni so familia nyingi zilibeba nyumba nzima hakubaki mtu wala hakuna aliyekubali kubaki bandarini zipo shuhuda kwamba chuma iling'oa nanga kutoka ktk gate abiria wengine wamening'ia kwa nje mfano wa gari za Mbagala za miaka ile na wote walikufa.
 
Haikuwa kubwa ila kama ulivyoandika hapo juu walipakia abiria mara nne kuzidi uwezo wake mixer mizigo.

Yupo jamaa yangu alikuwa na hardware Pemba yeye Twiga cement walimpelekea mzigo wake aliniambia ila sikumbuki vizuri ni kama ilikuwa ton 25 au ton 15 na siyo yeye tu aliyekuwa na mizigo ilikuwa mingi na ilikuwa ni likizo ya mwezi wa tisa na kulikuwa na sherehe ya kidini so familia nyingi zilibeba nyumba nzima na baadhi wote walikufa.
Aisee Mungu atuepushe na hizi ajali zisiendelee kutokea. Familia nyingi zilipotea kwenye hizi ajali zinazobeba watu wengi
 
Aisee Mungu atuepushe na hizi ajali zisiendelee kutokea. Familia nyingi zilipotea kwenye hizi ajali zinazobeba watu wengi
Pemba nzima ilizizima kama hajafa mjomba mtu kafa babu mtu au shangazi mtu zipo familia zilipoteza ndugu zaidi ya kumi,same na hiyo ya Mv Nyerere 2018 Ukerewe yote hakukuwa na nyumba ambayo haikuguswa kwa namna yoyote ile.

Ni kawaida ajali za visiwani na ziwani kuondoka na roho za watu wengi wa familia moja kutokana na muingiliano wao kuwa ule ule wa siku zote.
 
Bado vivuko vya magogoni pale feri. Watachinjika hata watu 2000 pale we subiri
Inasikitisha sana!!!

Nchi yenyewe tunajijua tunaenda kwa kudra za Mungu tu lakini uzembe tunaouzembea hakika ni wa ajabu Mungu aepushe mbali,huwa nikimsikia mtu anatambia mandhari nzuri ya Kigamboni na anapanda yale madude huwa naishia kutikisa kichwa tu nikimsikitikia
 
Wakati majinja imeangukiwa na contena ikauwa watu wengi enzi hizo ulikua hujazaliwa ni miongoni mwa ajali kubwa za barabarani
Nyie ndio mnaokurupukaga kwa uvivu wenu wa kusoma mada mnakimbilia kucomment....Bus linabeba watu wangapi? Nyie kizazi cha fb mnashida sana hamtakagi kujifunza yalotokea kabla hamjazaliwa ndio maana mnajua tu habari ndogondogo..mabasi ya majinja yameanza safari mwaka gani? Hii inadhihirisha upeo wako
 
Back
Top Bottom