Zijue aina ya Serikali zinavyoongozwa duniani

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
ZIJUE AINA ZA SERIKALI ZINAZOONGOZWA DUNIANI.

Kuna aina mbalimbali za serikali duniani miongoni mwa serikali hizo ni serikali za kidemokrasia(Democracy), Kidikteta(Dictatorship), Kifalme/Kimalikia (Monarchy), Kidini (Theocracy), Kidungu/Kijamaa(Totalitarian), Jamhuri (Republic) na Serikali za kihasimu(Anarchy).

SERIKALI YA KIDEMOKRASIA(DEMOCRACY).
Aina hii ya serikali ina mlolongo mrefu na imebebwa na historia ya matukio ya kihistoria kama vile vita, ukoloni. Vilevile katika serikali ya kidemokrasia watu wake (raia) huwa ndio waamuzi wa mwisho katika mustakabali wa taifa/nchi.Ikiwa pamoja na kuchagua kiongozi wa taifa (Mkuu wa nchi),wawakilishi mbalimbali, kuandaa na kuwezesha kwa katiba ya nchi. Raia wa nchi huwa huru katika kufanya mambo mbalimbali ikiwa pamoja na shughuli za kisiasa,kiuchumi, n.k

KIDIKTETA (DICTATORSHIP)
Hii ni serikali ambayo mtu mmoja huongoza kwa kutumia nguvu na kila raia/mwananchi lazima afate sera,taratibu na miongozo ya yule anayeongoza. Pia katika utawala wa aina hii kila jambo linaloamuliwa na anayeongoza hufanyika bila kupingwa. Aina hii ya uongozi ndio mbaya zaidi duniani ikifanana na ya kimachafuko (Anarchy).Mifano ya tawala za kidikteta ni pamoja nchi hizi ambazo ziliwahi kutawaliwa na watu tofauti katika nyakati tofauti Ujerumani chini ya Adolf Hitler, Zaire ya Mabuto Seseko,Uganda ya Idd Amin Dada n.k

KIFALME/KIMALIKIA(MONARCH)
Serikali hii huwa na kiongozi mkuu wa nchi ambaye hutumika kama kielelezo cha nchi, pia huwa na kiongozi mkuu wa serikali ambaye ndiye husimamia/kuratibu shughuli zote za serikali. Mara nyingi katika serikali hizi mkuu wa nchi huwa si Mtendaji wa serikali kwa maana ya kiutendaji bali husalia kama kielelezo cha mkuu wa nchi. Mkuu wa nchi katika mataifa haya huwa ni mfalme/malikia na kiongozi mkuu wa serikali huwa ni waziri mkuu. Mifano ya nchi zinazoongozwa kwa utawala wa aina hii ni Uingereza, Sweden, Spain n.k

KIDINI(THEOCRACY)
Katika serikali ya aini hii uongozi wake huwa juu ya taasisi za kidini ambazo hubeba mamlaka ya kiutendaji/kiutawala juu ya mfalme wa nchi. Mara nyingi serikali hizi huwa katika tawala za mataifa ya kiislamu.

KIDUNGU/KIJAMAA (TOTALITARIAN)
Aina hii ya serikali huendeshwa na mikundi kimoja chenye watu wa ama undugu au urafiki ambao hujipa mamlaka ya kuendesha mawazo ya watu wengi kwa miongo kazaa.Aina hii inafanana kama ya kidikteta isipokuwa hii huendeshwa zaidi ya mtu mmoja katika kuendesha mawazo ya watu wengi hutumia propaganda za umma wa raia maisha binafsi kupitia sanaa, sayansi na elimu. Mifano ya nchi hizo ni muungano ule uliokuwa wa Kisoviet na Vietnam.

JAMHURI (REPUBLIC)
Serikali za aina hii hufanana sana na serikali za kidemokrasia ambayo watu wake/raia wana katiba ya kuchagua viongozi kwa njia ya kidemokrasia. Lakini kitu kinachotofautisha na serikali hii na ile ya kidemokrasia ni kuwa serikali hii hutokana na muungano wa ama nchi mbili au himaya mbili na zaidi ili kutengeneza/kuunda taifa moja. Mifano wa nchi hizo pamoja na Tanzania, Marekani n.k

SERIKALI YA KUHASIMIANA(ANARCHY)
Katika nakala yangu hii fupi.Hii ni aina ya mwisho katika serikali ambazo nimejaribu kizieleza kwa ufupi. Serikali hii huwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe bila kuwa na serikali inayofanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu (bila kuwa na uongozi wa kikatiba) na uongozi wa kimuundo kama nchi. Mifano halisi kwa sasa naweza kuizungumzia Libya na Syria kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zimeingia kwenye mtafaruko wa kiungozi.

Note.
Serikali za kijamhuri(Republic) na kidemokrasia (Democracy) Mara nyingi zinaweza kutumika kwa pamoja katika nchi moja, lakini hutegemea na aina ya uongozi uliopo katika nchi husika. Kwa mfano Tanzania huitwa nchi ya kidemokrasia vilevile ni nchi ya kijamhuri kutokana na kuungana kwa nchi mbili (Tanganyika & Zanzibar).
 
Nchi yangu demrasia tupa kule muungano nao tupa kule upuhuzi mtupu
 
Ni katika kuelimishana tuu, Jamhuri sio muungano, bali ni autonomy, mamlaka yote ya kujitawala.

Nchi yetu ilipata uhuru tarehe 9 Dec, 1961 kutoka mkoloni Mwingereza, hivyo Mwalimu JK Nyerere akawa Waziri Mkuu wa kwanza, ila haukuwa Jamhuri, yaani republic, Mkuu wa nchi aliendelea kuwa Malikia wa Uingereza, kama ilivyo kwao Mkuu wa serikali ni Waziri Mkuu lakini mkuu wa nchi ni Malikia.

Tarehe 9 Dec, 1962, Mwl Nyerere akajiuzulu uwaziri mkuu, na kuitangaza Tanganyika kuwa Jamhuri, chini ya President, hivyo rais Nyerere ndio akawa rais wa kwanza wa Tanganyika, hivyo hata sherehe za uhuru, ni sherehe za uhuru na jamuhuri.

Tulipo ungana tukawa union, hivyo tuliitwa United Republic of Tanganyika and Zanzibar baadae Tanzania. Muungano ni union na sio republic.

P
 
Ni katika kuelimishana tuu, Jamhuri sio muungano, bali ni autonomy, mamlaka yote ya kujitawala.

Nchi yetu ilipata uhuru tarehe 9 Dec, 1961 kutoka mkoloni Mwingereza, hivyo Mwalimu JK Nyerere akawa Waziri Mkuu wa kwanza, ila haukuwa Jamhuri, yaani republic, Mkuu wa nchi aliendelea kuwa Malikia wa Uingereza, kama ilivyo kwao Mkuu wa serikali ni Waziri Mkuu lakini mkuu wa nchi ni Malikia.

Tarehe 9 Dec, 1962, Mwl Nyerere akajiuzulu uwaziri mkuu, na kuitangaza Tanganyika kuwa Jamhuri, chini ya President, hivyo rais Nyerere ndio akawa rais wa kwanza wa Tanganyika, hivyo hata sherehe za uhuru, ni sherehe za uhuru na jamuhuri.

Tulipo ungana tukawa union, hivyo tuliitwa United Republic of Tanganyika and Zanzibar baadae Tanzania. Muungano ni union na sio republic.

P
Asante kwa eliamu huwa nakuaaminia kwa upembuzi.
 
Nitachangia kikwaresmakwaresma....''Kwakuwa bwana aliyejuu Ni mwenye kuogofya na ndiye mfalme mkuu wa Dunia yote" mwisho wa kunukuu
 
Back
Top Bottom