Zijue aina 3 za kikwapa/vikwapa

Kubbra Hooda

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
209
500
Habari zenu wana jamvi.. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ieleweke wazi dhumuni la UZI huu si kutaka kuwakebehi watu wenye tatizo hili ila ni kupata maoni na ushauri jinsi ya kulitatua tatizo husika...

Kikwapa ni nn?Ni harufu mbaya ya jasho imtokayo mtu kwapani(Kamusi ya Kiswahili)ila kiuhalisia ni harufu yoyote mbaya itokayo sehemu yoyote ya mwili...

1:KIKWAPA KINACHOPATIKANA CHINI YA MAUNGIO YA MIKONO
Pengine hii ni aina iliyozoeleka kuliko zote maana mtu akiwa na harufu mbaya au kali utasikia wanasema ana kikwapa au kijasho

2:KIKWAPA CHA MDOMO
Hii hupelekea harufu kali kutoka kwenye mdomo yan hata upige mswaki au utafune big G bado hali ni ile ile. Wengi hupenda kusema ananuka mdomo la hasha mtu mwenye tatizo hili tunasema ana kiwapa cha mdomo hii inaweza kupelekea watu kukutenga au hata mahusiano kuvunjika kwa waliowahi kukutana na watu wenye shida hii mnaelewa nazungumzia nn

3:KIKWAPA CHA SEHEMU ZA SIRI/ NYETI
Hili pia ni tatizo ambalo lipo kwa jinsia zote mbili me na ke mtu mwenye tatizo hili hata ajitahidi kujisafisha na kubadili nguo zake za ndani bado hali hii huendelea kuwepo na wengi wetu badala ya kumwambia ukweli hasa akiwa ni mwenza wako tunaishia kuwakebehi au kuvunja mahusiano

Wanajamvi aina zote za vikwapa tajwa hapo juu huwa ni kero kwanza kwa mwenye tatizo mpaka kwa watu wanaomzunguka maana hakuna mtu anayeweza kuwa huru huku akijua anatoa harufu mbaya ktk mwili wake....
OMBI bila kuumiza hisia za yoyote naomba tujadili mbinu/dawa mbalimbali za kumaliza tatizo hili ...Nawasilisha


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom