Zifuatazo ni dawa za kupambana na chunusi


shalet

shalet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Messages
2,944
Likes
2,045
Points
280
shalet

shalet

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2013
2,944 2,045 280
Habari wakuu naomba tutumie uzi huu kushaurina dawa mbalimbali zinazosaidia kupambana na tatizo la chunusi iwe umeshwahai kuitumia ikakusaidia au kuna mtu unamfahamu kaitumia ikamsaidia naanza kuandika dawa chache nilizotumia na zote zinapaatika pharmacy bila hata kuandikiwa a dkatari.
1. persol gel
2. epiderm cream
3. hydrocortisone cream - hii inakadiriwa kuwa na madhara kadhaa ukiitumia muda mrefu hivo ni vizuri kusoma kwanza maelkezo yake.
karibu wadau kama kuna dawa ya kuongezea hapo.
4. gentrisone cream
 
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
32,924
Likes
98,428
Points
280
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
32,924 98,428 280
Mimi ni katika wale wanaotumia maji na sabuni tu, uso ukiharibika ni katika harakati ya ile safari kwenda kulipia pango to the moon, ninaosha uso na sabuni na sipaki kitu chochote usiku.
 
princess ariana

princess ariana

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2016
Messages
4,864
Likes
6,859
Points
280
princess ariana

princess ariana

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2016
4,864 6,859 280
Mimi ni katika wale wanaotumia maji na sabuni tu, uso ukiharibika ni katika harakati ya ile safari kwenda kulipia pango to the moon, ninaosha uso na sabuni na sipaki kitu chochote usiku.
huwa inaleta chunusi?
je kama pia hujasex mda mrefu?
au kama hubleed vizuri?
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
84,160
Likes
126,860
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
84,160 126,860 280
Wengine wana ngozi nzuri za kurithi toka kwa wazazi, lakini wengine utawaonea huruma aisee jinsi chunusi zinavyowaharibu nyuso zao. Yaani unakuta mtu mpaka anajichukia.

Mimi ni katika wale wanaotumia maji na sabuni tu, uso ukiharibika ni katika harakati ya ile safari kwenda kulipia pango to the moon, ninaosha uso na sabuni na sipaki kitu chochote usiku.
 
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
32,924
Likes
98,428
Points
280
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
32,924 98,428 280
Wengine wana ngozi nzuri za kurithi toka kwa wazazi, lakini wengine utawaonea huruma aisee jinsi chunusi zinavyowaharibu nyuso zao. Yaani unakuta mtu mpaka anajichukia.
ninaona niwashukuru wazazi
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
84,160
Likes
126,860
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
84,160 126,860 280
Wengine lije jua ije mvua bado nyuso zao hazina hata kijichunusi utasikia watu wanamuuliza "unatumia nini" unakuta hatumii chochote kile.

ninaona niwashukuru wazazi
 
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Messages
18,160
Likes
1,614
Points
280
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2012
18,160 1,614 280
Dawa za asili ndio dawa hizo zingine biashara tu.
Tango
Limao
Liwa
N.k.

Aione MziziMkavu
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,029
Likes
5,492
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,029 5,492 280
JINSI YA KUONDOA CHUNSI KWA NJIA YA ASILIMagadi Soda:

Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge icho sehemu ilio athirika na chunusi. Kwa muda wa dakika 15-20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa maji yasiwe ya moto. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapo ona athari ya chunusi imepotea.

Matango:

Unaweza kutumia Tango kwa kuondoa chunusi na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.
mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kasha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Wacha ikae kwa muda wa dakika 15-20 kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu kwa siku.

Kitunguu Thaumu:

Unaweza kutumia kitunguu thaumu. Kuondoa chunusi. Matumizi ya Kitunguu thaumu, uleta matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na hata kuuwa bacteria sababu ina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili). Twanga kitungu thaumu, au unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi shikilia kwa dakika 5-10, na kisha safisha na maji baridi. Waweza kufanya ivyo asubuhi na jioni.

Mnana (Peppermint):

Unaweza kutumia majani ya Mnanaa kuondoa chunusi usoni.
Majani ya manna utumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa. Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.

Matumizi ya Limao:

Kata limao na kisha kwa kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwa maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha wacha pakauke, unaweza kurudia rudi kila baada ya masaa kadhaa. Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa, kwa sababu yameweka vihifadhi kemikali zingine kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao alisi.

Kutumia Asali:

Matumizi ya asali ni ya asili na ufanya ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.


Kutumia Papai:

Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na kisha iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.

Dawa Ya Meno:

Unaweza kushangaa, lakini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.
Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanyakazi vizuri.

Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au nganoiuliosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiwacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.
Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.

Matumizi ya Poda:

Unaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na na kuiwacha mpaka asubuhi.

Matumizi ya Mvuke:

Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo uku ukielekeza uso wao kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke k wa dakika 5-10. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.


Tahadhari:

Njia hizi za Asili, uchukuwa muda kidogo mpaka kuona matoke ya kuridhisha.
Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali ilio karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.
chanzo.Jikolangu
 

Forum statistics

Threads 1,275,230
Members 490,947
Posts 30,536,270