Zifahamu Nchi nne zinazounga mkono kundi la Taliban

Mzee makoti

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
2,569
3,051

Marekani 'ikiikimbia' Taliban zifahamu nchi hizi nne zinazoendeleza uhusiano na kundi hilo​

e

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Huku Marekani na nchi nyingi za magharibi zikiharakisha kuwoandoa raia wake nchini Afghanistan baada ya kundi la Taliban kuuteka mji mkuu wa Kabul na kuchukua madaraka, kuna mataifa ambayo hayana wasi wasi wowote kuhusu kuendelea na uhusiano wao na watawala wapya wa Taliban .

Mataifa hayo yameonekana kutotikiswa na hofu ambayo Marekani na washirika wake wameonyesha baada ya Taliban kushika hatamu.

Miongoni mwa nchi hizo ni China ,Urusi ,Pakistan na Qatar. Mataifa hayo yamesema yataendelea na uhusiano wa kidiplomasia na Afghanistan na hata kulipa kundi hilo msaada linapoendelea na juhudi za kuunda serikali mpya nchini humo. Lakini kwanini nchi hizo zinaonekana kutokuwa na hofu kuhusu Taliban kuingia madarakani?

Urusi​

ur

Maelezo ya picha,

Urusi imekuwa mshirika mkubwa wa Taliban, ingawa mara kadhaa imekana kuisaidia kwa silaha kundi hilo
Baada ya kuangushwa kwa serikali ya Afghanistani, kampeni ya kimya kimya ya kulifikia kundi la Taliban kama imemlipa Rais wa Urusi Vladimir Putin. Kwenye maandishi kundi hilo limepigwa marufuku na Moscow, na mpaka sasa Serikali ya Urusi haijasema lolote kama italitambua kundi hilo kama serikali halali ya Afghanistan.

Lakini kauli ya wiki hii Waziri wa masuala ya kigeni wa Urusi alitangaza kwamba Urusi imeanza mawasiliano na Taliban ambayo imesema "imeanza kurejesha hali ya utulivu" jijini Kabul na maeneo mengine ya Afghanistan. Wakati Taliban wakiuvamia mji wa Kabul huku vikosi vya jeshi la Marekani vinavyomuunga mkono Raiss Ashraf Ghani vikiondoka, warusi waliweka wazi kwamba hawataondoa shughui zao za kidiplomasia nchini humo.

Katika taarifa yao wamesema, ni kwa sababu Taliban wamechukua nchi bila kukutana na upinzani wowote kutoka kwa vikosi vyilivyofundishwa na Marekani na washirika wake. Kidiplomasia, Urusi kama inaiunga mkono Taliban, iliweza kuruhusu mkutano huko Moscow uliohudhuriwa na Taliban, mjumbe wa baraza kuu la usalama la Afghanistan na shirika la kijamii, na kuipaisha Taliban kimataifa.

Katika taarifa zingine zinasema kuwa, Taliban imekuwa ikipokea silaha zake kutoka Urusi, ingawa mar azote Urusi imekuw aikikana kuwapa silaha wapiganaji wa kundi hilo.

China​

q

Maelezo ya picha,
China, ikiongozwa na waziri wake wa nje Wang Yi (kulia) iliwaalika wawakilishi wa Taliban kwa mazungumzoo huko Tianjin
Wakati Taliban ilipotawala kwa mara ya kwanza Afghanistan mwaka 1996, Chinailikataa kuutambua utawala huo na kufunga ofis zake za ubalozi kwa miaka kadhaa. Lakini kwa sasa Serikali ya China imekuwa nchi ya kwanza kuwakumbatia wanamgambo hao wa kiislamu.

Kigeugeu cha China kilionekana wiki mbili tu zilizopita, pale waziri wake wa kigeni Wang Yi alipoukaribisha ujumbe wa Taliban huko kaskazini mwa Tianjin, wakati huo wakiwa katika hatua za mwisho mwsho za kumuondosha madarakani Rais Ashraf Ghani, aliyetoroka nje ya nchi Jumapili ya wiki hii.

Wang akabariki kundi hilo kwa kusema "lina majukmu muhimu" ya kutawala Afghanistan kauli iliyozidi kuwapa nguvu Taliban na uhalali wa unachokifanya licha ya utawala wa kundi hilo kukosolewa na wengi ukitajwa kuendekeza ugaidi na kukandamiza wanawake.
China inahofia kuongezeka kwa uislamu wenye msimamo mklai miongoni mwa jamii ya wachina wachache wa Uyghur ambao wameonekana kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

China pia inataka kuendelea kujiimarisha kichumi kupitia jamii ya kimataifa , ikiwa na uchumi wa $14.7 trillion — ambao ni mara 17 zaidi ya uchumi wake wa mwaka 1996 — ukishamirishwa na biashara za ndani nan je ya taifa hilo.

Lakini kuongezeka kwa uyhasama kati ya Marekani na China, umefanya China kuendelea kujiimairsha yenyewe na kupunguza nguvu ya Marekani katika mataifa ambayo Marekani iliweka mizizi. Hilo ndilo linafanya kila fursa ikitokea Rais Xi Jinping wa China kuitumia kuwafurusha maadui zake, hasa Marekani wasiwakaribie wao na mipaka yake.

Haya ndiyo yanafanya China ionekana kama nchi kubwa itakayohodhi Afghanistan wakati huu Taliban ikijiandaa kutangaza taifa hilo kuwa taifa linalofuata misngiya kiislamu

Pakistan​

h

CHANZO CHA PICHA,USIP
Maelezo ya picha,

Balozi Asad Majeed Khan wa Pakistani
Waziri mkuu wa Pakistani Imran Khan, alisema jumatatatu ya wiki hii kwamba Afghanistan imevunja na kuondoa pingu za utumwa, baada ya serikali ya nchi hiyo kusambaratika. MMoja wa mabalozi wenye nguvu Pakistani Asad Majeed Khan aliwahi kueleza kwenye mkutano wa masuala ya amani wa USIP, Julai 7, 2021 kwamba. "kuwekeza kwenye amani Afghanistan ni namna pekee ya kupunguza ugaidi unaoendelea". Lakini kushika hatamu kwa kundi la Taliban chini Afghanistan kuna maana gani kwa majirani zao Pakistani?

Kifuupi, Marekani na raia wengi wa Afghanistan wanachukizwa na kitendo cha Pakistan kuisapoti Taliban, hali hiyo ikateresha uhusiano wa Marekani na Pakistan. Kinachoelezwa ni kwamba ushindi wa Pakistan ni maslahi ya kimkakati kwa Pakiostan, ingawa maafisa wa Pakistan wamekuwa wakikana kuwa na maslahi yoyote.Ngawa bado makundi ya kigaidi yapo, Pakistan inaamini, itakuwa salama zaidi Taliban wakiwa madarakani kwa sababu ya nguvu yao kijeshi na uswahiba wao.

Kwa mujibu wa ripoti ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa, kuna magaidi zaidi ya 6,000 wanaofanya kazi zao kutokea mpaka wa Afghanistan ambao wanaungwa ama wanahsirikiana na Taliban. Kwa kuwa Taliban wanaungwa mkono na Pakistan, huenda Pakistan inajihisi iko salama kiasi.

Inaelezwa pia wapiganaji wa Taliban katika kipindi chote cha miaka 20 wamekuwa wakipatiwa matibabu Pakistan, ambayo kibiashara pia imekuwa na soko katika nchi ya Afghanistan na imekuwa ikitoa huduma kwa taifa hilo.

Qatar​

Doha

Maelezo ya picha,
Asila Wardak (kushoto) kutoka baraza kuu la usalama la Afghanistan na Anarkali Honaryar, mwanasiasa wakiwa Doha kwenye mkutano wa kusaka amani wa Taliban na Marekani uliofanyika Doha, Julai 7, 2019

Qatar imekuwa taifa muhimu kwa amani ya Afghanistan na imekuwa ikiendesha mazungumzo ya amani kati ya serikali iliyofurushwa na na kundi la Taliban. IPia imekuwa nchi inayoiunga mkono Taliban wazi, ikielezwa kukisaidia kikundi hicho kiuxchumina kisiasa na kukipa hadhi ya kukitambua kimataifa.

Kwa Taliban kushika hatamu sasa Afghanistan, Qatar inaweza kuwa mnufaika wa kwanza baada ya Qatar kusimamia mzungumzo yaliyohusisha pia maafisa wa Marekani. Mazungumzo ambayo yamesaidia Marekani kuondoa vikosi vyake Afghanistan, kutolewa kwa wafungwa wa kisiasa na kivita katika magereza yaAfghanistan.

Baada ya Taliban kushika hatamu, kundi hilo linatarajiwa kupata msaada mkubwa wa kifedha kutoka Qatar ambayo nayo inatarajia kujiongezea nguvu katika maeneo ya Asia ya kati na maeneo mengine jirani kwa ajili ya shughuli zake za kiuchumi
 
Pakistani ndio wamekuwa wakiifadhili Taleban siku zote, sasa afunge ubalozi au ilipaswa kupanua ubalozi uliopo? Nina wasiwasi watu hawajamwelewa Mchina, huyu as long as kuna faida ya kiuchumi anayoipata , hata taifa husika likawa linaua raia wake, mchina hataongea chochote.
 
Hayo mataifa yanayojinasibu kwa kuutambua huo utawala wa kikatili wa Taliban yanajulikana wazi ni tawala za namna gani.

Huu utawala wa kiislamu kuna waislamu wengi tu ambao hawaupendi kabisa na tena ni wengi tu kwa dunia ya sasa na ndio maana waislamu wengi wamezamia nchi za magharibi na kamwe hawakimbilii kwenye nchi za kiimla kama China au Russia.

Nature ya mwanadamu yeyote kama alivyoumbwa na Mungu ni kiumbe kinachohitaji uhuru na hichi ndicho kitu ambacho utawala wowote wa kiislamu unapingana nao siku zote.

Mara kulazimisha wanaume wafuge ndevu, mara michezo haitakiwi, mara watoto wa kike wasisome, mara elimu ya magharibi haitakiwi, mara wote lazima wawe ni waislamu tena kwa lazima, mara watoto wa kike ni kufungiwa tu ndani kama kuku wa kisasa.

Yaani ni shida sana imani hii. Hawakubali kabisa kwamba karne ya saba ni tofauti kabisa na karne ya 21 na kwa maana yake ndio maana hata wananchi wao wanazikimbia hizo tawala zao za kiimla kwenda kwenye nchi zinazoamini ktk uhuru wa watu.
 
Nchi inaendeshwa kwa sheria za kiislamu, sheria isiyo na mwisho wala kupitwa na wakati. na sio mila. Mila ni ninyi huku.

Usome uislamu upate kuujuwa.
 
China yye Ana taka pesa tu na washirika ili aweze kuongeza ushawishi wa kisiasa duniani
 
Back
Top Bottom