Zifahamu haki ya wenye nyumba na wapangaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zifahamu haki ya wenye nyumba na wapangaji

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jan 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Sheria kuhusiana na Mpangaji na Mwenye Nyumba nchini Tanzania zinaeleweka vizuri zaidi kwa kuiangalia kwanza Sheria iliyoweka misingi ya mahusiano ya masuala ya upangishaji (haki na wajibu wa mwenye nyumba na mpangaji wake) ambayo, japo

  imeshafutwa na kuwekwa sheria mpya badala yake, sheria hiyo ndiyo iliyoweka misingi muhimu katiak mahusiano haya hata leo.
  Ni vizuri basi tunavyoanza kuyafahamu mahusiano ya mwenye nyumba na mpangishaji wake kisheria tukiaangalia sheria hii na hasa pia kwa sababu hakujawa na mabadiliko makubwa sana katika masuala mengi muhimu ya haki na wajibu wa kila mmoja wao-yaani mpangishaji na mpagiji nyumba/chumba.

  Sheria hii ya mwaka 1984 iliyojulikana kama Rent Restriction Act (ama kwa tafsiti isiyo rasmi, 'Sheria ya Udhibiti wa Pango') kwa sasa imefutwa na kuchukuliwa na Sheria nyingine kama mbadala wake.
  Kabla ya mwaka 1984, masuala mengi ya nyumba na ardhi yalidhibitiwa na Sheria ya Ardhi yamwaka 1923 ambayo yenyewe nayo ilikuja kufutwa mwaka 1999 baada ya Bunge kupitisha Sheria mpya kabisa za ardhi, yaani Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999.

  Sheria ya Udhibiti wa Pango ya mwaka 1984 ilitaja bayana katika kifungu chake cha 2(1) kuwa ilihusika na nyumba za kupangisha za kuishi pamoja na zile za kibiashara, kubwa na ndogo na pia za binafsi na zile za umma. hata hivyo, mnamo mwaka 1992,

  mashirika na taasisi za umma yaliondolewa katika kuhusika na shetia hii ambayo kwa ukweli iliwekwa zaidi ili kulinda maslahi na haki za wapangaji, kipindi ambacho Tanzania bado ilikuwa ikifuata Ujamaa halisi na mnyonge kutetewa kwa kila namna.

  Mathalani, chini ya Sheria hii, iwapo mwenye nyumba (mpangishaji) alitaka kumfukuza mpangaji wake, basi ilibidi kwanza mpangishaji aende mahakamani kupata idhini ama baraka ya kufanya hivyo.

  Kwa mujibu wa Profesa Issa Shivji (2005) mpangishaji pia hakupaswa kumtimua mpangaji wake kwa sababu tu ya mpangaji kukosa kodi ya pango na kwamba pia mpangishaji hakupaswa kumtoza mpangaji
  kodi ya zaidi ya miezi miwili kabla.

  Sheria hii ya udhibiti wa Pango ambayo ingweza pia kuitwa Sheria ya Mpangaji na mwenye nyumba, ilikuwa imempa Waziri anayehusika na Ardhi na nyumba mamlaka makubwa mno likiwemo lile la kuwa na uwezo wa kusitisha matumizi ya vifungu fulani vya sheria hiyo au hata sheria yote kabisa (kama ilivyotungwa na Bunge) ili kwamba isimguse mtu au makundi fulani ama nyumba za aina fulani.

  Chini ya sheria hii kulikuwa na baraza la Utatuzi wa Migogoro ya wapangaji na wenye Nyumba ambalo lilikuwa na mamlaka makubwa na muhimu. Baraz hili lilikuwa limepewa mamlaka ya Kisheria kufanyakazi kama mahakama ili kwamba liweze kupokea malalamiko au kesi za migogoro ya pango na mikataba ya upangishaji nyumba ama kutoka kwa mpangishwaji au kutoka kwa mpangishwaji.

  Kwa mamlaka yake, Baraza hili liliweza kutoa amri ya zuio la kufukuzwa mpangaji au idhini ya mwenye nyumba kumtimua mpangaji wake na hata kufafanua kisheria mikataba ya upangishaji.

  Kifungu kimojawapo muhimu cha Sheria hii kilitamka bayana kuwa iwapo kulikuwa na mkataba kati ya mwenye nyumba na mpangaji wake na wakawa katika mgogoro katika mkataba huo, basi Baraza
  hili (mahakama ya Migogoro ya Nyumba) lilikuwa na uwezo wa kuja na amri yenye mkataba mbadala wenye haki kwa pande zote, ili mradi tu mkataba huu usikinzane na Sheria yenyewe ya Udhibiti wa Pango ya mwaka 1984.

  Baraza (Mahakama) la Nyumba ambao lilikuwa katika ngazi za chini, mikoa hadi taifa, lilikuwa na majukumu muhimu kama tulivyoona, na ili kuondoa utata wa mamlaka ya Baraza hilo sheria ilianisha wazi kupitia kifungu cha 11 majukumu kamili ya Baraza hili yakiwa, pamoja na yale yaliyotajwa, kuwa:

  (a) Kutoa uamuzi kama au la mahali au nyumba fulani iliyohusika na mgogoro ilikuwa inaguswa na sheria hii; (b) Kutaja kiwango cha kodi ya nyumba (pango) ambacho mpangishaji fulani alipaswa kukitoza kwa mpangaji wake pale mgogoro unapofika hapo; (c) Kusikiliza na kutolea uamuzi kuhusiana na suala lolote la ki-mgogoro wa kupinga kupandishwa ama kupunguzwa kodi ya

  nyumba; (d) kupanga uwiano wa ulipaji pango la nyumba itokeapo mgogoro unaohusisha wapangaji wanaopanga kwa kuchangia;
  (e) Kuamuru ulipaji fidia ama gharama ambazo mpangaji au mpangishwaji alifanya katika kutengeneza nyumba huku jambo hilo likiwa ni wajibu wa mhusika mwingine ama lilistahili kuchangiwa na jambo hilo likawa halijafanyika.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,485
  Likes Received: 4,759
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona hii ni kama historia?? tue sheria inayotumika sasa kwa ubayana
   
 3. u

  ureni JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ni kweli hata mie nimejaribu kuisoma kwa makini ni historia tu,hebu atufafanulie kwa vifungu au kwa yeyote anayejua atupe data.
   
Loading...