Zifahamu haki na wajibu wako kama mlipakodi kwenye mkataba wako na Mamlaka ya Mapato (TRA)

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mkataba huu unaainisha bayana haki na wajibu wa mlipakodi kama ilivyoelezwa kwenye sheria za kodi kwa lengo la kudumisha na kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya TRA na mlipakodi.

Wajibu wa TRA


TRA katika kutekeleza wajibu wake wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali inazingatia yafuatayo:-

6.1 Kutoa makadirio sahihi ya kodi kwa mujibu wa sheria.
6.2 Kukusanya kodi kwa mujibu wa sheria za kodi, kanuni na taratibu zilizopo.
6.3 Kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu kwa walipakodi na wadau wengine.
6.4 Kushughulikia maulizo ya walipakodi na wadau wengine ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao. 7
6.5 Kushughulikia malalamiko ya walipakodi na wadau kwa nia ya kupata ufafanuzi/ ufumbuzi na kuiwezesha TRA kubaini mapungufu katika huduma inazotoa. Maoni ya walipakodi na wadau yatachangia kuboresha huduma.
6.6Kuajiri na kuwaendeleza watumishi wake ili wawe na uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja na wadau wengine.

6.7 Kuelimisha walipakodi na wadau kuhusu haki na wajibu wao.
6.8 Kuhakikisha upatikanaji wa fomu za kodi na taarifa sahihi kwa wakati na kwa lugha nyepesi. 6.9 Kurahisisha mawasiliano kati ya walipakodi na wadau wengine.
6.10 Kushirikiana na walipakodi na wadau wengine kwa misingi ya kujali heshima, utu na kuwa na mtazamo wa kumjali mteja.
6.11 Kushirikiana na Bodi ya Rufani za kodi/ Baraza la Kodi na Mahakama katika kuhakikisha uzingatiaji wa muda katika mahudhurio Mahakamani na utoaji wa vielelezo ili kutatua migogoro ya kodi. Pia TRA itaheshimu maamuzi yatakayotolewa na mahakama.

6.12 Kutoa ushauri kwa Serikali na taasisi zake kuhusu masuala ya sera, sheria za kodi na utekelezaji wake.
6.13 Kutoa mafunzo ya kitaaluma kwa walipakodi na wadau kuhusu masuala ya kodi.
6.14 Kutoa mrejesho wa taarifa zitakazotolewa na walipakodi pamoja na umma zinazohusu ukwepaji wa kodi. Pale itakapothibitika kuwa kulikuwa na ukwepaji wa kodi na kodi hiyo kukusanywa, mtoa taarifa atazawadiwa asilimia 3 ya makusanyo husika lakini kiwango hicho hakitazidi TZS milioni 20.

7.0 Wajibu wa Mlipakodi

Mlipakodi anawajibika kwa mambo yafuatayo:-

7.1 Usajili Mlipakodi anayestahili kusajiliwa kwa ajili ya kulipa kodi ana wajibu wa kujisajili kisheria.

7.2 Uwasilishaji wa Ritani za Kodi Mlipakodi aliyesajiliwa kwa mujibu wa sheria za kodi ana wajibu wa kuwasilisha ritani za kodi na kulipa kodi iliyokadiriwa kwa muda unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

7.3 Usahihi wa Ritani, Nyaraka za Forodha na Madai ya Marejesho Mlipakodi anayewasilisha ritani, nyaraka za forodha au madai ya marejesho anawajibika kuhakikisha kwamba nyaraka hizo ni sahihi.

7.4 Malipo ya kodi kwa wakati Mlipakodi ana wajibu wa kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka kulipa adhabu au/na riba kama ilivyoainishwa katika sheria.

7.5 Utoaji na Kudai Stakabadhi/Ankara za kodi za kielektroniki • Mlipakodi (Muuzaji) ana wajibu wa kutoa stakabadhi za mauzo/ankara za kodi za kielektroniki • Mnunuzi ana wajibu wa kudai stakabadhi za manunuzi/ ankara za kodi za kielektroniki kwa kila bidhaa/ huduma iliyotolewa.

7.6 Ushirikiano na Maafisa wa TRA Kila Mlipakodi ana wajibu wa kutoa ushirikiano kwa maafisa wa TRA: • Kwa kutoa taarifa na nyaraka zinazohusiana na masuala ya kodi au taarifa nyinginezo pale anapotakiwa kufanya hivyo. • Kuwapa nafasi ya kutimiza wajibu wao kisheria pasipo kuwaingilia, kuwatisha, kuwatukana, kuwadharau au kuwashawishi kwa namna yoyote ile.

Haki za Mlipakodi

TRA itazingatia na kuheshimu haki za Mlipakodi katika kuhakikisha vyovyote kuwa anatimiza wajibu wake wa kulipa kod bila vikwazo 11 Haki hizo ni pamoja na

8.1 Utendaji Usio na Upendeleo Mlipakodi anastahili kupata haki sawa katika utekelezaji wa sheria za kodi ili aweze kulipa kodi kwa kiasi kinachotakiwa.

8.2 Faragha na Usiri Taarifa binafsi au zile za kibiashara zitakazotolewa katika ofisi za TRA zitafanyiwa kazi kwa usiri na kwa faragha isipokuwa tu pale sheria inapoelekeza vinginevyo.

8.3 Dhana ya Uaminifu Mlipakodi ana haki ya kudhaniwa kuwa ni mwaminifu isipokuwa pale tu mwenendo wake utakapothibitishwa vinginevyo.

8.4 Kupinga Makadirio ya Kodi Mlipakodi ana haki ya kupinga makadirio ya kodi au uamuzi wowote uliofanywa na TRA kwa mujibu wa sheria.

8.5 Vivutio na Misamaha kwa mujibu wa Sheria za Kodi Mlipakodi ana haki ya kupanga masuala yake ya kodi ili kuweza kupata vivutio/msamaha wowote utokanao na sheria za kodi kwa kuzingatia vipengele na taratibu zilizopo.

Kwa maelezo ya ziada pakua faili la PDF hapo chini
 

Attachments

  • MKATABA WA HUDUMA NA MLIPAKODI.pdf
    374.7 KB · Views: 37
Back
Top Bottom