Zifahamu faida za fenesi kwa afya yako

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Fenesi ni moja ya tunda ambalo mti wake ni mkubwa na wenye majani ya kijani kibichi. ndani ya tunda la fenesi huwa kuna mbegu .
Tunda hili hupatikana sana katika maeneo ya Asia na ni mojawapo ya matunda yenye virutubisho vingi kiafya.

Ndani ya fenesi kuna virutubisho kama vile vitamin A, C na B6 pamoja na madini ya potassium na calcium sambamba na madini ya chuma na magnesium.

Tunda hili ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi yaani 'fiber' ambazo ni muhimu kwa upande wa umeng'enyaji wa chakula na hivyo kumsaidia mhusika kuepukana na shida ya kukosa choo mara kwa mara.

Moja ya kazi nzuri ya fenesi ni pamoja na kuimarisha kinga za mwili, lakini pia tunda hili huongeza vitamin C mwilini ambayo piahusaidia kusaidia seli za damu kufanya kazi vizuri.

Kama utakuwa na ngozi mabayo si nzuri labda huenda itakuwa na mikunjo mikunjo basi ni vyema ukaanza kutumia fenesi leo kwani litakusaidia kuondosha hali ya mikunjo kwenye ngozi na kuondosha ukavu wa ngozi.

Kwa wale wenye shida ya upungufu wa damu yaani anemia tunda hili ni zuri pia kwao kutokana na kuwa na madini ya chuma 'iron' ambayokwa kiasi kikubwa husaidia uzalishaji wa seli nyekundu za damu mwilini.

Aidha, tunda hili la fenesi pia husaidia sana kwa wale wenye tatizo la presha ya kushuka hii ni kwa sababu ndani ya tunda hili kuna madini ya potassium ambayo hurekebisha kiwango sodium mwilini jambo ambalo huchangia kuongeza kwa kiwango cha msukumo wa damu mwilini,a lakini pia madini hayo ya potassium husaidia kuimarisha na kusimamia mishipa ya moyo

Matumizi ya tunda hili pia husaidia kuongeza uoni mzuri kutokana na kuwa na vitamin A anbayo ni muhimu sana kwa afya ya macho, lakini pia fenesi husaidia kuimarisha afya ya mifupa kutokana na kuwa na madini ya magnesium.

FB_IMG_1618634866843.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi hawapendi harufu yake na jinsi inavyoganda mkononi

Yule Mtu anayetoa vile vitunda na kuweka kwny vimfuko ana kazi kwelikweli.
 
Ulitaka lifakamiwi kwa wingi, sema tu linaongeza nguvu za kiume
Linaongeza nguvu za kiune mkuu, kula kutwa mara tatu halafu usiku unywe na tone la glicerine kidogo, kitu itasimama zaidi ya nchumari
 
Mimi sipendi kulimenya, huwa nanunua yale ambayo tayari yamemenywa na yako packed tayari.
Mwanzoni nilipata shida kuyala hasa kutokana na harufu yake.
Kulimenya hata mimi sipendi na sijawahi menya. Ukute limewekwa kwenye fridge lina kaubaridi flani aisee nakula bakuli zima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom