Zifahamu faida 5 za kununiana na mpenzi wako ndani ya mahusiano ya ndoa au uchumba

Chrix_Tz

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
880
1,098
1.HUSAIDIA KUPUNGUZA MIGOGORO

Hali hii hupunguza kabisa migogoro ya hapa na pale, kwani hiki ni kipindi ambacho mtakuwa mbalimbali jambo ambalo huepusha maudhi ya kibinadamu.

Mfano, yawezakana katika kipindi mlichonuniana na mpenzi wako, uliingia ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake kutoka kwa mtu aliyekosea namba. Kwa kuwa hauko naye karibu jambo hili halitakuumiza maana hutaelewa nini kimeendelea tofauti na kama ungelikuwa naye karibu.

2.KUBAINI TABIA X ZA MWENZAKO
Hiki ni kipindi ambacho sasa kitakusaidia wewe kubaini tabia na mienendo mibaya ya mwenzi wako. Hii ni kwa kuwa utakuwa mbali naye hivyo naye hujiona kuwa yuko huru kufanya jambo lolote analoona kuwa linafaa bila kujali uwepo wako kwani kila mtu hana ‘time’ na mwenzake.

Kama ni mlevi kupindukia, mchafu, muongo na tabia nyingine mbaya za kufanana na hizi basi ataanza kuzionesha katika kipindi ambacho mmenuniana.

3.KUPATA MUDA WA KUTAFAKARI ZAIDI
Hapa naomba nieleweke vizuri kabisa kwamba, ninapoongelea suala la kutafakari zaidi katika kipindi ambacho wewe hauna maelewano mazuri na mwenzi wako, namaanisha kuwa utapata muda mzuri zaidi wa kutafakari penzi lenu kwa ujumla.

4.KUFAHAMU AINA YA MARAFIKI ZAKE
Si kila rafiki wa mwenza wako ana nia nzuri na uhusiano wenu au anafurahia penzi lenu. Mathalani, labda wewe ni msichana na pengine miongoni mwa rafiki zake kuna mmoja au wawili ambao hutamani sana kupata penzi lako.
Sasa katika kipindi ambacho utakuwa umenuniana na mpenzi wako basi itakuwa ni nafasi nzuri kwao kuitumia kunyunyizia sumu ya kumponda huku wakikutamkia maneno ya kukushawishi, hivyo utakuwa umeelewa ni aina gani ya marafiki alionao mwenzi wako.

5.KUBAINI AINA YA PENZI ALILONALO KWAKO
Katika kipindi hiki, utaweza kuelewa ni aina gani ya penzi alilonalo huyo mtu wako juu yako. Kwa mpenzi aliye na hisia za dhati kabisa kwako, katika kipindi hiki atakuwa ni mtu wa kutafuta njia ya kupata suluhu ya tatizo lenu.



X-mas na Mwaka Mpya Iyoooo
 
Ubunifu ni kitu kimoja cha msingi sana katika maisha.

Unaweza kukutana na uzi mrefu kuanzia dar hadi moro, umepangiliwa kwa aya, unasoma aya moja baada ya nyingine pasi na kuchoka mpaka mwisho na haupotezi maana.

Na vilevile kuna vinyuzi vingine ni vifupi, havina mpangilio mzuri yaani ukisoma aya moja ama utangulizi tu unajikuta kichwa kinauma, unapiga miayo, kinachofuata ni kuamua kuutupilia mbali maana hauna maana.

Nimejitahidi nimesoma aya ya kwanza tu nika-lose interest kwa kweli.
 
Umejitahidi kupangilia vema mkuu comment yako ila baada ya kuisoma nikagundua hii ni tabia ya mtu mweusi kwahiyo sishangai sana aina hii ya comment kwangu ni chai na bagia ..... karibu tena kimeni
Ubunifu ni kitu kimoja cha msingi sana katika maisha.

Unaweza kukutana na uzi mrefu kuanzia dar hadi moro, umepangiliwa kwa aya, unasoma aya moja baada ya nyingine pasi na kuchoka mpaka mwisho na haupotezi maana.

Na vilevile kuna vinyuzi vingine ni vifupi, havina mpangilio mzuri yaani ukisoma aya moja ama utangulizi tu unajikuta kichwa kinauma, unapiga miayo, kinachofuata ni kuamua kuutupilia mbali maana hauna maana.

Nimejitahidi nimesoma aya ya kwanza tu nika-lose interest kwa kweli.
 
Kwa ubunifu kama huu au vipi wa kucopy na kupaste ama upi mkuu




Nipo hapa maeneo ya buza kwa mama kibonge, habari ni kwamba jamaa mmoja ambae hajafahamika jina lake wala la mpenzi wake, amemchoma kisu mpenzi wake hadi kufa.

Jamaa baada ya kumchoma mpenzi wake huyo, na yeye amejichoma kwa lengo la kujiua lakini mpaka naandika hapa alikuwa bado hajafa.

Tukio hili limetokea kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo East London hapa buza kwa mama kibonge.

Wenyeji wa hapa wanadai kuwa haijapita hata miezi mitatu tangu dada mmoja kunyongwa na mpenzi wake hadi kufa kwenye nyumba hii hii ya kulala wageni chanzo kikisemekana ni wivu wa kimapenzi.

Vijana tujaribu kutafuta namna bora ya kutatua changamoto zinazotukabili bila kuleta athari kama hivi.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom