JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Saratani ya utumbo mpana ni aina mojawapo ya saratani ambayo inaathiri utumbo mpana na eneo la mwisho la utumbo mpana linaloitwa rectum.
Mwanzo wa saratani ya utumbo mpana ni vimbe ndogondogo zisizo saratani ambazo taratibu huanza kujitengeneza kwenye utumbo na baadaye kuanza kugeuka kuwa seli za saratani.
Kulingana na takwimu, tatizo la aina hii ya saratani linazidi kuongezeka kila kukicha huku asilimia 5 tu ya wagonjwa wakiwa wamerithi tatizo hilo.
Baadhi ya watu wenye saratani ya utumbo mpana hupata dalili za maumivu kwenye tumbo na tumbo kujaa gesi na kadiri tatizo linavyokuwa la muda mrefu zaidi ndivyo ukali wa maumivu unavyoongezeka zaidi.
Dalili kuu za saratani ya utumbo mpana ni:
Mabadiliko kwenye choo kama kuharisha na kupata choo kigumu ama kukosa choo kwa muda mrefu, dalili hizi zinaweza kuwa za muda mrefu
Kupata choo chenye damu ama choo cheusi na chenye nta
Mwili kuchoka sana kila mara
Kicheuchefu na kutapika mara kwa mara
Kukosa hamu ya kula na mwili kupungua uzito ghafla
Mwili kuishiwa damu (anemia)
Macho na ngozi kuwa na rangi ya manjano (jaundice)
Visababishi vya saratani hiyo ni kama vifuatavyo:-
Kuishi katika mazingira hatarishi na mtindo wa maisha.
Watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka ya 50 wapo kwenye hatari zaidi
Kula lishe mbovu hasa vyakula viliyosindikwa na kuchakatwa sana kiwandani,kama nyama za makopo, mafuta yaliyochemshwa sana kiwandani na kuwekewa hydrogen.
Uzito mkubwa na kitambi
Kuishi maisha ya kizembe pasipo na ratiba ya kufanya mazoezi na kushugulisha mwili
matumizi makubwa ya pombe hasa kwa watu wazima na wenye umri mkubwa
Uvutaji wa sigara na tumbaku
Wagonjwa waliowahi kuugua magonjwa ya mfumo wa chakula kwa kipindi cha nyuma
Watu wenye kisukari
Wanaofanya kazi kwenye maeneo yenye kemikali sababishi za saratani mfano kwenye mitambo ya mionzi na viwandani.
Hatua za kuzuia na Kupambana na Saratani ya Utumbo Mpana.
Kula zaidi vyakula vya kuondoa sumu na vyenye nyuzinyuzi au kambakamba kwa wingi. Vyakula hivyo ni kama Parachichi, nazi na tuwi la nazi,Viazi vitamu, Bamia, Karanga, Mafuta ya nazi na mizeituni, Tangawizi, Kokoa na uyoga.
Hakikisha unapunguza uzito.
Fanya mazoezi ya kutosha na kushugulisha mwili wako
Punguza matumizi ya pombe na sigara.
Hakikisha unatibu magonjwa ya mfumo wa chakula, kama kuharisha, na kukosa choo kwa muda mrefu.