Zidumu Fikra Sahihi za Mwenyekiti wa Chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zidumu Fikra Sahihi za Mwenyekiti wa Chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichankuli, May 21, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Wana JF mnaikumbuka salamu hii ya enzi za mwalimu?

  Kidumu Chama cha Mapinduzi,
  Idumu siasa ya Ujamaa na Kujitegemea,
  Zidumu Fikra Sahihi za Mwenyekiti wa CCM,

  Ningependa wana JF tujadiliane hivi ni kwa nini baada ya Marehemu Nyerere kuachia ngazi (mwenyewe akiita Kung'atuka) aliamua pia sehemu ya tatu ya salamu hii (zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM) kutotumika tena wakati bado mwenyekiti wa CCM aliendelea kuwepo?

  Je kuna uwezekano kuwa aliamini hakuna fikra sahihi toka kwa Mtasnzania mwingine zaidi ya za kwake?

  Je hii inaweza kuwa ndiyo hadi leo pamoja wengi wetu kukiri kuwa Muungano wa Tanfganyika na Zanziba unakasoro/kero nyingi lakini bado CCM hawako tayari kuzifanyia kazi na ikiwezekana kubadili muundo wa Muungano ili Watanganyika wakiwa sehemu ya pili ya muungano wasilazimike kulipa kodi ya umiliki wa ardhi wakati wenzao wazanzibari wanajikamatia ardhi kama hawana akili nzuri achilia mbali ubunge mara Mkuranga mara wapi huko Zenji?
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  "The greatest man is he who forms the taste of a nation; the next greatest is he who corrupts it"
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kichankuli,
  Nadhani kwanza Nyerere hakutaka kuabudiwa. Pia alishaona unafiki wa akina Kingunge ambao walikuwa wakiimba zidumu zidumu lakini kugeuka ameshakuwa bepari wa kupindukia.
   
 4. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Unafikiri ni kwa nini hakuacha fikra (sahihi?) za Mwenyekiti Mwinyi za Ruksa zisidumishwe na wanaCCeM?
   
 5. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mchonga meno alipenda sana kuogopwa,kuabudiwa na ketetemekewa na hakuzuia kwa wakati wowote kuacha huo msemo wa kipumbavu wa zidumu fikra za mwenyekiti.
   
 6. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Mkulu kumbuka vizuri, baada ya Mchonga kuachia Uenyekiti tu iyo salamu nayo haikutumika tena pamoja na kwamba haikutangazwa hadharani ni wazi yalitolewa maelekezo ya kutoitumia. Hoja yangu ni kuichambua salamu hiyo na kusitishwa kwake kutotumika maana bado wenyeviti tunaendelea kuwa nao
   
 7. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Salamu hiyo ilikuwa katika enzi za usoshalisti zilikuwa na madhumuni ya kuwadumaza watu kifikra ili kukandamiza fikra zozote zile za siasa mbadala.Alipoingia Mzee Ruksa salamu hizo hazikuwa na maana tena kutokana na hali ya kisiasa duniani kubadilika.Hakukuwapo haja tena ya kumwabdudu mtu mmoja kwani mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ulikuwa ndiyo unaanza kuchomoza.
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  ilikuwa sehemu ya unafiki wa Mwalimu Nyerere.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Now I get it..that is why the guys are so busy corrupting the state...wahusika wasindwe na walegee
   
 10. Mau

  Mau Senior Member

  #10
  May 22, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nyerere nae kachangia TZ kuwa mbovu kwani alikuwa na sera za kikandamizaji,enzi zake si ruhusa kuwa na biashara ukiwa mtumishi wa serikali
   
 11. T

  TONGINDI Senior Member

  #11
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Je na hii kauli mbiu ina tija kwa taifa au ni ufisadi mtupu pia? TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE
   
 12. r

  raffiki Senior Member

  #12
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka kauli mbiu hiyo ilikua na tija maana wenyeviti zamani walipatikana kwa fikra thabiti kwa maendeleo ya nchi na watu wake,nao walilitambua hilo..shv iwe wenyeviti wa kata iwe wa wapi ni ukiwa zuri tuu kutafuta umaarifuu kwa njia yeyote sasa hapo unadhani kauli mbiu zitasaidia nini.

  Nime post kauli mbiu yetu 2015 sio wanyonge ambayo ni <Wenye neema na watu wao,sie wanyonge na masikini na wazalendo wenzetu wa kweli Dr. Salim,Magufuli na Slaa..>nashangaa MOD wameidelete bhana mie naanza kupata mashaka na JF naona kuna figure zinapendelewa humu.
   
 13. T

  TONGINDI Senior Member

  #13
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata kwenye jf kuna uchakachuaji? sasa mawazo yetu tutayatolea wapi? dah bora niamie uhamishoni burundi!

  tz yanakaribia kunishinda.
   
 14. r

  raffiki Senior Member

  #14
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kaka uchakachuaji upo..mie nimeshausoma siku nyingi kuna thread za kusifia baadhi ya watu humu huwa zinafagiliwa sana na wakiguswa tuu au kuwekewa upinzani wanalindwa. Ni kweli wengi ma best wameshaliona hili hadi kufikia 2015 haka kamchezo kakikomaa watu wengi watasepaa rwand na burudi,isije ikawa mradi wa watu huu tena unajua tena bongo.
   
 15. O

  Ombeni Mbise Member

  #15
  Mar 20, 2013
  Joined: Nov 2, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwa najiuliza kila kukicha hawa jamaa wa CCM kusema ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WALIMANISHA NINI? Ukijaribu kuangalia Dunia yote ya Democrasia huwezi kuta eti watu wanakumbatia mawazo ya mtu mmoja na kuminya ya wengine eti zidumu fikra za mwenyekiti... Huu ni kunyima mawazo ya wengine na aina flani ya udi-kiteta wa siri na kuuwa fikran za wengine na kuaminisha kuwa fikra za mtu mmoja zinatosha kukidhi mahitaji ya watu...
  Hivi majuzi kuna kiongozi mkubwa wa ccm nilimuliza kwa njia ya simu hata yeye akasema haelewagi msemo huo una maaana gani. Kama chama hiki hadi leo kinatembea na msemo huu tunasema NO DEMOCRACY PRACTICE kwa hiki chama wanajamvi.
   
Loading...