Zidumu fikra sahihi za m'kiti ( kitanzi dhidi ya fikra huru )


Jayfour_King

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Messages
1,141
Likes
12
Points
0
Jayfour_King

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2009
1,141 12 0
Hi wana baraza ( JF ).
Mimi kwa sasa si mwanachama wa chama chochote ingawa ni shabiki chama chenye uthubutu wa kumwambia mfalme "mkuu umetoka uchi leo".

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu hotuba zote ambazo zimejiri bungeni tangu ya spika mteule (Anne Makinda) Waziri mkuu mteule ( MKPP) mwanasheria mkuu (Werema) Naibu spika ( J.Ndugai) na wanafiki wengine ndani ya CCM kuhusu spika wa bunge lililopita Mh. 6 kila mmoja kwa nafasi yake amekuwa akimsifia kwa kazi nzuri aliyoifanya.

Cha kushangaza hakuna hata mmoja ambaye amekuwa wazi na kutuambia mtu mwenye sifa zote hizo ambazo mimi pia (kwa mtazamo wangu) naamini alijitahidi sana kuwa fair na kuendesha bunge bila kuegemea sana upande wa chama chao.

Swali ni je hivi sababu hasa zilizomfanya aenguliwe kwenye nafasi hiyo ambayo kila mtu anasema kwamba alifanya vyema ninini? Kama wachambuzi na watanzania wa kawaida haitoshi kupewa sababu dhaifu kama 'kuwawezesha wanawake' kama ndio sababu za msingi za kumuengua Mh.6.

Hilo la wanawake limekuja kama kichaka na namna ya kumkwepa Mh.6 kwa kuwa hakuna mwanaume aliyepitishwa kugombea nafasi hiyo huu ni udhalimu,dhuluma,siasa za visasi na mwisho wa yote ni kutumia madaraka ya mwenyekiti wa chama vibaya.

Nimekuwa nikisikia kwamba muungwana ana siasa za visasi sikuwa naamini ila kwa hili naamini kujeruhiwa kwa maswahiba wake chini ya usimamizi wa Mh.6 naona hata muungwana naye pia hakupendezewa na akajichukulia nafasi hii kama namna ya kuonyesha kwamba ana makucha ya kushughulika na mtu yeyote so long as ni sisiem member.

Ninacho penda kuwaasa sisiem na hasa muungwana ni kwamba: Ule muda wa kusema zidumu fikra sahihi za mwenyekiti..........zimepitwa na wakati na uongozi imara utaletwa na demokrasia imara pia. Kwa vyovyote vile uteuzi wa spika umeongeza makundi na chuki miongoni mwa wanachama wa sisiem na hii ni hatari kwao.

Ingawa sisi tulio nje ya mifumo yao tunafurahia hili swali ni je wao wanalifahamu hilo?

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema pengine ni mpango wa mungu kumleta huyu muungwana ili aje avuruge mambo upande wao ili iwe nafasi nzuri kwa wapinzani wa kweli waweze kupata njia rahisi za kuikomboa nchi yetu kwa hawa wakoloni wa ndani.

Mungu ibariki Tanzania, pamoja tutashinda.
 
M

Mhombo.S.G

New Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
4
Likes
0
Points
0
M

Mhombo.S.G

New Member
Joined Jun 13, 2011
4 0 0
ki ukweli kwa anayeitwa spika wa Bunge Makinda ni nafasi nzuri kwa wapinzani kwakuwa,spika anaegemea zaidi kwenye chama na sio serikali,anatamani vyama ving vcngekuwepo cz huwa anachanganyikiwa kabisa kwa hofu na woga
 

Forum statistics

Threads 1,238,425
Members 475,954
Posts 29,319,891