Ziara za wabunge ughaibuni wakati bandarini kulikuwa hovyo

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Wakati wa awamu ya nne ilikuwa kila kukicha lazima iwepo habari ya wabunge kwenda nje kujifunza masuala ya uendeshaji wa serikali kupitia uwezo na uzoefu wa mataifa ya nje.
Ukitazama TBC saa mbili usiku utaiona habari ya wabunge wa kamati fulani ambao wamekwenda Singapore kwa ajili ya kujifunza mambo fulani. Ukitazama ITV utakuna na wabunge ambao ni wajumbe wa kamati ya miundombinu wakiwa katika ziara ya kujifunza usimamiaji na uendeshaji wa miundo mbinu, wakiwa nchini Afrika ya kusini. Yaani awamu yote ya nne karibu kila kukicha kulikuwa na habari zinazohusu wajumbe wa kamati za bunge wanaokwenda nje ya nchi kwa ajili ya kukuza uzoefu wao katika masuala yanayohusiana na kamati yao.

Lakini awamu ya tano imewadhihirishia wananchi kwamba pale bandarini peke yake kuna madudu mengi sana yalikuwa yanaendelea na yamechangia katika kudumaza uchumi mzima wa nchi hii. Najiuliza, inakuwaje kamati za bunge ya miundo mbinu iende kujifunza utendaji wa kazi katika nchi za nje, wakati bandari yetu inashindwa kufanya mambo ya msingi kabisa, kama vile kusimamia ulinzi ipasavyo?. Mabomba ya mafuta hayasimamiwi kama vile ni mali ya Taifa, mageti ya bandari hayana usimamizi mzuri, halafu kuna watu wanaokwenda nje ya nchi kwa kutumia kodi ya wananchi eti kwenda kujifunza masuala ya miundo mbinu?.

Ndoo ya maji inavuja, maji yanamwagika hovyo njiani, mwenye ndoo badala ya kuitazama ndoo yake vizuri ili ikibidi izibwe ili isiendelee kumwaga maji njiani, yeye anakimbilia kwa jirani eti kuangalia ni jinsi gani ndoo yake haivujishi maji!. Nauombea kwa Mwenyezi Mungu uongozi wa serikali ya awamu ya tano usije kupoteza lengo ambalo ndilo limeuweka madarakani.

Nawaombea kwa Mungu viongozi wa juu kabisa wa nchi hii, waweze kuvishinda vishawishi vyote vya rushwa na mitego yote yenye lengo la kuwaingiza kwenye ufikiriaji wa mambo na utendaji wenye hulka za kifisadi. Mungu ni mkubwa na ni mwema, naamini siku zote atawaongoza viongozi wa awamu ya tano.
 
Back
Top Bottom