Ziara za Mh. Rais na foleni zinazokera watumiaji wengine wa barabara

namraroh

Senior Member
Sep 9, 2010
112
122
Hbr ya leo JF fans and members,
kwa kweli naona sasa tunapokwenda sipo kabisa.

Leo Mh. Rais yupo ziarani mkoa wa Pwani, hiyvo tumelazimika kukaa barabarani kwa zaidi ya saa moja kupisha apite. Sasa tunaenda wapi na kauli yake ya hapa kazi tu, Tanzania ya viwanda na kadhalika?

Napenda kuwashauri ndugu zangu wa usalama wabuni njia mbadala badala ya kukwamisha shughuli nyingine za kimaendeleo kwa muda wote huu, naamini kabisa Mh. rais hajui nini kinaendelea huku barabarani
 
Hiyo hali ilikuwepo tokea miaka na miaka elfu lela ulela.
Shukuru kwenye hiyo foleni ulipo hamjaamrishwa kushuka kwenye magari yenu na kukata matawi ya miti ili akipita mumshangilie!!!
 
IFIKE MUDA WAWE WANATUMIA HELICOPTER KUTOKA NJE YA MIJI MIKUBWA HALAFU MISAFARA IWE INAWASUBIRI NJE YA MIJI HUSIKA.
 
Hiyo hali ilikuwepo tokea miaka na miaka elfu lela ulela.
Shukuru kwenye hiyo foleni ulipo hamjaamrishwa kushuka kwenye magari yenu na kukata matawi ya miti ili akipita mumshangilie!!!
kadri siku zinavyokwenda tutafika huko ! tutashushwa na kuamriwa kushangilia misafara
 
Mkuu hata nchi zilizoendelea ambazo wana barabara nyingi na ni pana hayo mambo yanafanyika

Niliona ziara moja ya waziri mkuu wa uingereza bi Theresa magari yalisimamishwa yote hadi msafara wake ulipopita. Pia urusi, Kenya n.k.

Usalama wa Rais ni wa muhimu kuliko unapowahi wewe, kuna watu wanaweza kutumia mwanya huo wa magari kutosimamishwa kugonga gari la Rais
Nakubaliana na wewe kabisa, ila haja ya kuboresha utaratibu ni muhimu sana, haiwezekani masaaa mawili ufunge njia kuu eti kwamba rais anapita, kwanza siamini kwamba rais anafanya ziara barabarani hivyo muda wote huu katusimamisha
 
Sio lazima kusubiri unaweza kupita tu.. Wakikusimamisha waambie una haraka. Hawana noma hao jamaa.
 
Jana asubuhi wakati anaelekea mlandizi tulikaa sana pale njia inayotokea loliondo, ghafla nikaona kuna premio imechomoka hiyooo ikanyoosha nikasema wakimdaka huyu atajieleza.
 
Mkuu hata nchi zilizoendelea ambazo wana barabara nyingi na ni pana hayo mambo yanafanyika

Niliona ziara moja ya waziri mkuu wa uingereza bi Theresa magari yalisimamishwa yote hadi msafara wake ulipopita. Pia urusi, Kenya n.k.

Usalama wa Rais ni wa muhimu kuliko unapowahi wewe, kuna watu wanaweza kutumia mwanya huo wa magari kutosimamishwa kugonga gari la Rais
Sisi hatuna barabara nyingi
 
Back
Top Bottom