Kwa kiasi cha wiki tatu hivi zilizopita, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad alifanya ziara za majimbo katika wilaya zote kumi za Zanzibar akianzia kusini Unguja na kumalizia Micheweni Pemba. Katika ziara hizi za kichama kwa mara nyengine kumekuwa na taharuki na matumaini miongoni mwa wanachama hasa wa CUF na CCM.
Taarifa tulizopata ni kuwa Maalim alikuwa akijiita kuwa ni Rais na wafuasi wake walimshangilia na kumwita hivyo kila alipopita, alipata mapokezi makubwa hasa kisiwani Pemba.
Ziara hii imeleta taharuki na matumani kama nilivyosema kutokana na ujumbe wake wa wazi kwenye ziara hii. Mwishowe tutauliza masuali kwa ziara hii nzima na hali halisii ya nchi yetu Tanzania ilivyo kwa sasa.
Taarifa zinadokeza kwamba, Maalim alifika wakati kuwaambia wafuasi na wazanzibari kuwa muda mchache ujao atatangazwa kuwa Rais wa Zanzibar na alifika hadi kutaja neno "early march" akimaanisha mapema mwezi machi,2017. Kwa upande wa CUF na wafuasi wake walifurahia kauli hizi na kufufua matumaini ya kupata kile wanachodai haki yao ya Oktoba, 2015.
Kwa Upande wa CCM Zanzibar kulikuwa na taharuki kubwa kuanzia kwa wanachama wa kawaida hadi kwa wajumbe wa Baraza la wawakilishi waliokuwa wakiendelea na vikao vya Baraza huko Zanzibar. Taarifa zinaeleza mara kwa mara wajumbe walitaka msimamo wa Serikali(SMZ) kuhusu kauli za Maalim kujiita Rais na ahadi ya kutangazwa na huku wakihoji Maalim kufanya mikutano Zanzibar nzima tena wakati mwengine ya wazi bila kuchukuliwa hatua na madai ya kuvunja sheria. Inaelezwa mawaziri walipata shida kujibu.
Katikati ya taharuki hiyo, iliarifiwa Dr shein kukutana na wawakilishi wa CCM hapo Barazani tarehe 26 februari siku ya Jumapili iiyopita na kuarifiwa wawakilishi kuzuiwa hadi simu zao kwenye kikaoi hicho. Aidha kwenye mitandao ya kijamii kulienea taarifa za iliyodaiwa hutuba ya Dr Shein kwa wajumbe hao ikielezea ujio wa mabadiliko ya uongozi ingawa baadae ikulu ilikanusha hutuba hio.
Kwa ufupi, ziara hii ya Maalim na nongono zilizoko Zanzibar zinatia mashaka sana na zinawaweka wananachi na wafuasi wa vyama hasa vya CUf na CCM katika mazingira tatanishi.
Kwa upande mwengine wa vyombo vya habari , ziara hii ya maalim ilienea zaidi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kwenye redio, magazeti na televisheni ingawa ilikuwa ya zaidi ya wiki mbili.
Kwa mnasaba huu kuna nini Zanzibar na watu watarajie nini? Jee hii ni propaganda ? na kwa nini Maalim alifanya ziara hii bila bubudha yoyote ingawa mikutano ya kisiaa ya wazi imezuiwa na hii ya Maalim iliashiria kila dalili kuleta taharuki ya wazi kila alipopita? Kuna nini tujuvyeni basi.
Kishada