Ziara za Kinana (Katibu Mkuu wa CCM) Mikoani

HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
69,120
93,847
Kutoka ukurasa wa Nape Nauye haya ndiyo aliyoandika.


Nimetoka kuongea na vyombo vya habari juu ya ziara za Katibu Mkuu na zinazotarajia kuanza, ni ziara za kusukuma utekelezaji wa Ilani.

Ziara zinategemea kuanza tarehe 21 Mkoani Mtwara, 22 Sumbawanga na 23 geita na 24 Arusha...!

Tunaanza Mtwara kushughulikia tatizo la soko la koro,kisha Sumbawanga kukagua miradi ya barabara,kisha Geita kushughulikia masuala ya migodi.

Na Mkoa wa nne ni Arusha ambako Katibu Mkuu atakagua Viwanda na kutatua tatizo la wawekezaji walioodhi viwanda bila kuvifanyia kazi...!



Pia Nape alisema hayaaaa kwenye account yake

THIS IS CCM..,WE DO WHAT WE WANT, WHEN WE WANT..,ALWAYS AT RIGHT TIME...!"

OUR TIME IS NOW....! Hii speed is beyond there imagination.,sijui kama watani wataweza mbio hizi.?!?"

JUMANNE, NOVEMBA 20, 2012 | NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

*Atangaza kutumia helkopita,
*Chadema nao wakimbilia Karagwe


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetangaza kuanza rasmi ziara ya kikazi mikoni ili kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Katika ziara hiyo, CCM imepanga kutumia helkopita ili kufikia maeneo yote ambayo imekusudia.

Ziara hiyo,imekuja siku moja baada ya Sekretarieti mpya kuchaguliwa wiki moja iliyopita mkoani Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema ziara hiyo itaongozwa na Katibu Mkuu, Abdurahman Kinana.

Alisema Kinana, ataongozana na wajumbe wa Sekretarieti na baadhi ya mawaziri ambao kila mmoja kwa nafasi yake, atawajibika kuwaeleza wananchi mikakati na mipango ya utekelezaji wa ilani na ahadi za CCM.

"Ziara hii, itaanza kesho katika mkoa wa Mtwara, hapo tutaangalia suala la bandari na korosho, ambapo chama kitakuwa na nafasi yake ya kueleza na mawaziri wanaohusika na bandari na korosho nao watawajibika kueleza wananchi.

"Novemba 22, tutakuwa Sumbawanga na tutajikita upande wa barabara na viwanja vya ndege… kazi itakuwa ile ile ya kukutana na wananchi na kuelezana ukweli,

"Siku inayofuata, tutakuwa Geita huko tutaangalia suala la madini na jinsi wananchi wanavyonufaika, waziri mwenye dhamana ataeleza hatua wanazochukua na mwisho wa ziara yetu itakuwa mkoani Arusha,tutajikita katika uwekezaji viwandani na ajira,"alisema.

Alisema baada ya kumaliza ziara hiyo, watarudi kujipanga tena ili kuandaa safari ya mikoa mingine.

Alisema suala la kujivua gamba bado litaendelea kufanyiwa kazi na kuhakikisha chama kinabaki na wanachama wasafi, wasiopenda na kutoa rushwa na wenye maadili mema.

Akizungumzia suala la kuwapo kwa propaganda za kudai CCM imechukua busara za Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa kutaka elimu ya sekondari kuwa bure na kupunguza kodi katika vifaa vya ujenzi, Nape alikana.

Alisema sula la elimu bure sio jambo geni, lilikuwapo tangu enzi za Hayati Mwalimu Nyerere.

CHADEMA

Wakati huo huo, Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), inatarajia kuanza katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila alisema M4C wanayoipeleka Karagwe ni mkakati wa chama hicho kuwajengea uwezo viongozi wake kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa.

Alisema kuna mabadiliko kidogo ya M4C iliyozoeleka ambayo hufanywa na viongozi wa kitaifa.

Alisema mkakati wa sasa, ni wa kisayansi umelenga kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya mikoa 32,kuanzia Novemba 22 hadi 23.

Baada ya hapo watapelekwa katika ‘shamba darasa' la wilaya nzima ya Karagwe yenye majimbo mawili na kata 32 ili kuwapima kama wameleewa sawasawa M4C.

"Huu ni mkakati mpya wa M4C, tutawakutanisha viongozi 64 wa mikoa yote ya kichama katika wilaya moja ya Karagwe, lengo ni kujenga uwezo wa viongozi wetu wa mikoa yote 32 ya kichama.

"Baada ya siku mbili, viongozi watagawanywa katika timu 10 katika kata 42 kwa muda wa siku mbili, kila moja ili wafanye kwa vitendo yale waliyofundishwa darasani, na baadaye tutawarudisha tena darasani kuona kama wameiva sawasawa.

 
wehu kweli nyie na hizo ziara zenu za unafiki,leo ndo mnashugulikia soko.wezi wakubwa.
 
mwambie akumbuke kuwaelezea jinsi alivyosingiziwa kuwa kampuni yake ndiyo inauwa tembo wetu kwa kutoa kibali cha kusafirisha pembe kwenda huko Asia ili wanachama waweze kumwelewa maana akiwa kimya watajua kuwa anahusika

CCM hoyeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Huyo msomali akifika Arusha awaeleze wananchi kuwa mashine za kufua nakukausha nguo alizopora kama msaada kwa ajili ya hopsital za jeshi na mount meru anazirejesha lini?.

Pia Muumulize maagizo ya Nape alipokuwa Songea kwenye Serikali yamefikia wapi?.Ngoja wale per diem tu hawana lolote wezi wakubwa ccm
 
Ziara za Katibu mkuu wa ccm kukagua viwanda na waziri wa viwanda anafanya kazi gani au ndo kutojua mipaka ya utendaji wa serikali na chama
Mr Rocky kama unakumbuka walisema CCM sasa inarudi kufanya kazi ya kuisimamia Serikali kwa hiyo wakiona utendaji usioridhisha watamwajibisha waziri husika kupitia vikao vya chama
 
Last edited by a moderator:
Arusha? Atapona mtu kweli hapo,bwana Nape na viwanja vya sahara mwanza mtakuwepo lini?
 
Kama chama kitaamua kuanza kuikumbusha serikali kutumikia wananchi walio wengi badala ya kutumika kama daraja la wachache kujineemesha basi itakuwa tofauti kubwa. Ngoja tuone mambo yatakavyoenda.
 
Sasa ni dhahiri CDM inakufa polepoleee SISIEM HOYEE WAMESHINDWA KUJENGA HOJA WAMESHAMIRI KWENYE UMBEYA
TULIWAMBIA SSM CHAMA KUBWA
 
Mtwara wanaenda Kushugurikia soko la Korosho kivipi? Si Bodi ya Korosho imeisha Tangaza Bei ya kununulia Korosho? Na si injulikana Mununuzi pekee ni Vyama vya Ushirika? Au wamepata Mnunuzi mwingine?

Arusha wanakuja kukagua Viwanda Vipi? cha Mataili? si wamekiuua CCM? vipi wamepata mwekezaji Mpya? Songea wanakagua Barabara wakiwa kama nani? Je Kinana amesomea Mambo ya Ujenzi? Je anataka aone kama kuna Nyufa Barabarani?

Hii nchi inamalizwa na Siasa, Mambo ya Kitalaamu inaingizwa Siasa,
 
mimi sio pro-chadema wala sio ccm mafisadi
ila niweke angalizo hili suala la korosho kulifanya kuwa ni ajenda ya kisiasa mnafanya dhulma kubwa sana,,na hata ile bodi ya korosho wale jamaa mudhhihir na anna abdalah hawana weledi wowote wa kazi zaidi ya kuendelea kuididimiza bodi ile
wakulima kila siku wanalalamika na kukata tamaa
hili nalo mnalifanya kuwa ni ajenda ya kisiasa??
 
Mtwara wanaenda Kushugurikia soko la Korosho kivipi? Si Bodi ya Korosho imeisha Tangaza Bei ya kununulia Korosho? Na si injulikana Mununuzi pekee ni Vyama vya Ushirika? Au wamepata Mnunuzi mwingine?

Arusha wanakuja kukagua Viwanda Vipi? cha Mataili? si wamekiuua CCM? vipi wamepata mwekezaji Mpya? Songea wanakagua Barabara wakiwa kama nani? Je Kinana amesomea Mambo ya Ujenzi? Je anataka aone kama kuna Nyufa Barabarani?

Hii nchi inamalizwa na Siasa, Mambo ya Kitalaamu inaingizwa Siasa,

Nikukumbushe tuu ndugu ya Chasha serikali ya CCM imerekebisha mambo mengi kupitia sauti au jukwaa la wapinzania na kwa kazi hiyo vyama vya upenzani vimetokea kupata wafuasi kwa kuwasemea matatizo yao. CCM sasa inakwenda kufanya hivyo hivyo "performance evaluation against yardstick" - ilani ya uchaguzi. Mimi siyo mali ya chama chochote nachangia tuu kuchangamsha jukwaa.
 
Last edited by a moderator:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom