HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 69,344
- 94,505
Kutoka ukurasa wa Nape Nauye haya ndiyo aliyoandika.
Nimetoka kuongea na vyombo vya habari juu ya ziara za Katibu Mkuu na zinazotarajia kuanza, ni ziara za kusukuma utekelezaji wa Ilani.
Ziara zinategemea kuanza tarehe 21 Mkoani Mtwara, 22 Sumbawanga na 23 geita na 24 Arusha...!
Tunaanza Mtwara kushughulikia tatizo la soko la koro,kisha Sumbawanga kukagua miradi ya barabara,kisha Geita kushughulikia masuala ya migodi.
Na Mkoa wa nne ni Arusha ambako Katibu Mkuu atakagua Viwanda na kutatua tatizo la wawekezaji walioodhi viwanda bila kuvifanyia kazi...!
Pia Nape alisema hayaaaa kwenye account yake
THIS IS CCM..,WE DO WHAT WE WANT, WHEN WE WANT..,ALWAYS AT RIGHT TIME...!"
OUR TIME IS NOW....! Hii speed is beyond there imagination.,sijui kama watani wataweza mbio hizi.?!?"
Nimetoka kuongea na vyombo vya habari juu ya ziara za Katibu Mkuu na zinazotarajia kuanza, ni ziara za kusukuma utekelezaji wa Ilani.
Ziara zinategemea kuanza tarehe 21 Mkoani Mtwara, 22 Sumbawanga na 23 geita na 24 Arusha...!
Tunaanza Mtwara kushughulikia tatizo la soko la koro,kisha Sumbawanga kukagua miradi ya barabara,kisha Geita kushughulikia masuala ya migodi.
Na Mkoa wa nne ni Arusha ambako Katibu Mkuu atakagua Viwanda na kutatua tatizo la wawekezaji walioodhi viwanda bila kuvifanyia kazi...!
Pia Nape alisema hayaaaa kwenye account yake
THIS IS CCM..,WE DO WHAT WE WANT, WHEN WE WANT..,ALWAYS AT RIGHT TIME...!"
OUR TIME IS NOW....! Hii speed is beyond there imagination.,sijui kama watani wataweza mbio hizi.?!?"
JUMANNE, NOVEMBA 20, 2012 | NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM
*Atangaza kutumia helkopita,
*Chadema nao wakimbilia Karagwe
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetangaza kuanza rasmi ziara ya kikazi mikoni ili kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Katika ziara hiyo, CCM imepanga kutumia helkopita ili kufikia maeneo yote ambayo imekusudia.
Ziara hiyo,imekuja siku moja baada ya Sekretarieti mpya kuchaguliwa wiki moja iliyopita mkoani Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema ziara hiyo itaongozwa na Katibu Mkuu, Abdurahman Kinana.
Alisema Kinana, ataongozana na wajumbe wa Sekretarieti na baadhi ya mawaziri ambao kila mmoja kwa nafasi yake, atawajibika kuwaeleza wananchi mikakati na mipango ya utekelezaji wa ilani na ahadi za CCM.
"Ziara hii, itaanza kesho katika mkoa wa Mtwara, hapo tutaangalia suala la bandari na korosho, ambapo chama kitakuwa na nafasi yake ya kueleza na mawaziri wanaohusika na bandari na korosho nao watawajibika kueleza wananchi.
"Novemba 22, tutakuwa Sumbawanga na tutajikita upande wa barabara na viwanja vya ndege… kazi itakuwa ile ile ya kukutana na wananchi na kuelezana ukweli,
"Siku inayofuata, tutakuwa Geita huko tutaangalia suala la madini na jinsi wananchi wanavyonufaika, waziri mwenye dhamana ataeleza hatua wanazochukua na mwisho wa ziara yetu itakuwa mkoani Arusha,tutajikita katika uwekezaji viwandani na ajira,"alisema.
Alisema baada ya kumaliza ziara hiyo, watarudi kujipanga tena ili kuandaa safari ya mikoa mingine.
Alisema suala la kujivua gamba bado litaendelea kufanyiwa kazi na kuhakikisha chama kinabaki na wanachama wasafi, wasiopenda na kutoa rushwa na wenye maadili mema.
Akizungumzia suala la kuwapo kwa propaganda za kudai CCM imechukua busara za Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa kutaka elimu ya sekondari kuwa bure na kupunguza kodi katika vifaa vya ujenzi, Nape alikana.
Alisema sula la elimu bure sio jambo geni, lilikuwapo tangu enzi za Hayati Mwalimu Nyerere.
CHADEMA
Wakati huo huo, Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), inatarajia kuanza katika Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila alisema M4C wanayoipeleka Karagwe ni mkakati wa chama hicho kuwajengea uwezo viongozi wake kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa.
Alisema kuna mabadiliko kidogo ya M4C iliyozoeleka ambayo hufanywa na viongozi wa kitaifa.
Alisema mkakati wa sasa, ni wa kisayansi umelenga kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya mikoa 32,kuanzia Novemba 22 hadi 23.
Baada ya hapo watapelekwa katika ‘shamba darasa' la wilaya nzima ya Karagwe yenye majimbo mawili na kata 32 ili kuwapima kama wameleewa sawasawa M4C.
"Huu ni mkakati mpya wa M4C, tutawakutanisha viongozi 64 wa mikoa yote ya kichama katika wilaya moja ya Karagwe, lengo ni kujenga uwezo wa viongozi wetu wa mikoa yote 32 ya kichama.
"Baada ya siku mbili, viongozi watagawanywa katika timu 10 katika kata 42 kwa muda wa siku mbili, kila moja ili wafanye kwa vitendo yale waliyofundishwa darasani, na baadaye tutawarudisha tena darasani kuona kama wameiva sawasawa.