MWANALUGALI
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 601
- 34
Namuomba Rais Jakaya Kikwete asitishe mara moja ziara anazofanya kwenye wizara mbalimbali kwa sababu hazina tija kwa Taifa na zinasababisha hasara kubwa na kupoteza muda wa kazi mwingi kwa wafanyakazi wa wizara anazokuwa anatembelea.
Siku nzima ya jana wafanyakazi wote wa Wizara ya Nishati na Madini hawakufanya chochote wakimsubiri rais aje na alipokuja hakuna kilichofanyika wakisubiri aondoke. Alipoondoka ilikuwa ni mijadala ( unajua watanzania kwa ushabiki wao) jinsi Waziri alivojikanyaga, mikwara ya rais, dowans nk.! fikiria manhours zilizopotea kwa rais kuja wizarani ambako hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia wala kutoka baada ya mkulu kuja.
Kama Kikwete anafikiri ni muhimu kukutana na watendaji wa wizara, anatakiwa awe anawaita ikulu na kuwapa kibano huko huko kuliko kuja ku disrupt kazi zetu za kila siku, vinginevyo inaonekana anatembelea kuja kuuza sura kama afanyavyo anapokwenda huko ughaibuni. Fikiria umati mkubwa uliokaa pale nje ya wizara ukisubiri kumuona, fikiria matatizo aliyosababisha kwa kuzuia magari kupita mtaa wa samora jana, na misongamano aliyoisababisha mjini!