Ziara za CDM - Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga na Zanzibar

kama mikoa hii ndiko kwenye ujinga na umaskini kwanini mmekimbia huko kaskazini kuja coast?
Au ujinga wetu ni kuwauzia maeneo mkajenga ili muweze kujisitiri na familia zenu? Wapwani kuwa wakarimu kuwakaribisha ndio mtutusi? Hivi mlitaka na sisi tuwe wabaguzi kama mlivyo kule kwenu kwamba ukiwa mgeni huuziwi eneo?
Hivi sisi wa pwani na wale mnao ua bibi zenu wenye macho mekundu ukidai ni wachawi na albino ili mpate utajiri nani ni mjinga? Kisha mmezoea pia kuwaita wa pwani ni washirikina bila kutoa ushahidi, kama ni great thinker, jiulize hivi, ulishawahi kusikia pwani wameua albino? Wameua vikongwe kwa imani za kishirikina?

nakumbushia tu msinipige mawe nikija pwani.
mapinduzi ya zanzibar yaliongozwa na tito okelo kutoka uganda.
na ukombozi wa kweli pwani utaletwa na akina tito okelo kutoka bara.
chadema vema.
 
Hii mikoa ni ngome yetu, CDM hawakubaliki kabisa na uzuri ni kuwa hata wao wanalifahamu hili na ndiyo maana huwa hawaendi kwenye ngome hizi, hata ufunguzi wa matawi katika vyuo vilivyo maeneo hayo ni ndoto, ha hii ni over 20% ya kura Tanzania, Tunaingia 2015 tukiwa na mtaji wa kura milioni 5 za wanachama pamoja na asilimia 20% ya mikoa hii, jipangeni kwa 2025.

Walienda kuwapa pole wahanga wa maandamano Arusha.
Wakaenda kuwapa pole wahanga wa North Mara

Jiulize ni kwa nini hawajaenda kuwapa pole wahanga waliobomolewa nyumba na mabanda yao Znz?

Na kwa nini wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana waliikwepa sana mikoa hii?.

Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga na Zanzibar ni maji marefu.

Acha upuuzi, safari inaendelea,CDM wamesema wanafika nchi nzima.

Lakini nasikitika ngome yenu inabaki kuwa maskini. Nipo Songea, kwa sasa hapa ni CHADEMA tuuuuu.
 
malaria sugu.

mwanangu una Id nyingi kweli.

hzi ngome unazisema ndiyo zinaongoza kwa umasikini na ujinga.

It is just a matter of time for all the people to run away from ccm, because is not standing for people and justice. Tatizo kuna watu wamengangania mtazamo wa udini na wanafikiri cdm ni ya dini fulani, they are deadly wrong. time will tell.:A S 103:
 
Mtaji wa CCM ni ujinga wa watanzania,ndio maana wana ngome ktk mikoa hiyo ambayo wanaongoza kwa ujinga na umaskini

Hivi umaskini kwa tafsiri yako ni ipi? kwani huko unakodhani wameendelea ndiko kunakoongoza magonjwa ya ukimwi na uchunaji wa ngozi za binaadamu mtindo mmoja! wachilia mbali wazee wenye machomekundu wanaouliwa ovyo! ningekushauri ufanye utafiti upya kuhusu nini maendeleo!
 
maeneo uliyoyataja nadhani bado watu wamelala na hawajuai kwa nini wanaishi... trust me kwa mwendo huu wa kununua blue band kwa kijiko au mkate kwa slices wataamka tu
 
nakumbushia tu msinipige mawe nikija pwani.
mapinduzi ya zanzibar yaliongozwa na tito okelo kutoka uganda.
na ukombozi wa kweli pwani utaletwa na akina tito okelo kutoka bara.
chadema vema.

Duh! Mambo mengine yamekaa kimizaha lakini ukiyatafakari kwa kina kuna ukweli ndani yake.

Kuna makala ya Mzee Mwanakijiji katika Tanzania Daima la Jumatano, 18th May 2011 akinukuu kitabu cha wale jamaa wadini wakidai kimsingi TANU, ambayo waasisi wake wengi ni wazee wa Dar es Salaam na maeneo ya Pwani, ni ya Waislamu.

Lakini tunaona TANU yenyewe, ilipata mwamko mpya baada ya kuingia Mwl. Nyerere kutoka bara. Jamani, hebu wasomi wetu fanyeni tafiti juu ya masuala haya.

La msingi si nani kaanzisha nini au kafanya nini; what matters is OUTPUT.
 
Back
Top Bottom