Ziara za BAVICHA zazaa matunda:Vijana duniani waililia Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ziara za BAVICHA zazaa matunda:Vijana duniani waililia Tanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Oct 19, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  TAMKO LA IYDU KUPINGA UKANDAMIZWAJI WA CHADEMA, MAUAJI YA WAFUASI WAKE NA WAANDISHI WA HABARI NCHINI TANZANIA

  Published: 18 October 2012
  [​IMG]
  Wakati Chama cha kisoshalisti CCM nchini Tanzania kikiwa kinapoteza mvuto , Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA) ambacho vijana wake (BAVICHA) ni mwanachama wa Umoja wa Vijana wa Kidemokrasia Duniani (IYDU) kimeendelea kuwa nguvu ya kuhamasisha na kuwaunganisha wananchi wa Tanzania katika ngazi za chini kupitia kampeni yake ya Vugu Vugu la Mabadiliko (M4C)Programu ya M4C ilizinduliwa na kuanza rasmi mwezi Mei 2012 na imekuwa tishio kwa Chama tawala cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake inayohaha kuendelea kuwa na mamlaka ya kisiasa nchini Tanzania.

  Katika jitihada za kuidhibiti programu ya M4C, serikali ya CCM imekuwa ikitumia jeshi la polisi, usalama wa taifa na vyombo vingine vya serikali kama ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kuinyamazisha CHADEMAMatukio ya utekaji nyara na mateso makali kwa wale wote wanajitokeza hadharani kuipinga serikali ya CCM na kuhamasisha watanzania wengine kudai haki zao za msingi yamekuwa yakiongezeka.

  Mfano halisi wa utekaji nyara na utesaji ni ule wa Dkt Stephen Ulimboka uliotokea mwezi Juni 2012 baada ya kuwaunganisha madaktari wenzake wa Tanzania kugoma kuishinikiza serikali kuboresha huduma ya afya Tanzania.

  Tukio la utekwaji wa Dkt Ulimboka lilifuatiwa na ufungiwaji wa gazeti la MWANAHALISI lililochapisha habari za kuhusisha utekwaji huo na idara ya usalama wa taifa ya Tanzania.Katika mazingira mengine, jeshi la polisi Tanzania limekuwa likivunja katiba na sheria za nchi hiyo kwa kuizuia Chadema kufanya mikutano yake ya hadhara na shughuli nyingine za siasa bila kutoa sababu za msingi zinazoeleweka huku likiachia Chama Cha Mapinduzi kufanya shughuli hizo hizo bila usumbufu wowote.

  Wakati CHADEMA ikifanya maandamano ya amani na mikutano yake ya hadhara, Jeshi la polisi limekuwa likitumia nguvu kubwa zisizohitajika na wakati mwingine za kinyama kwa raia na wafuasi wa chama hiki bila sababu za msingi.

  Katika jitihada zake za kuzuia maandamano ya amani na kisha mkutano wa hadhara katika Manispaa ya Morogoro mnamo tarehe 27/08/2012, jeshi la polisi nchini Tanzania lilitumia mabomu ya machozi na risasi za moto dhidi ya raia na wafuasi wa CHADEMA wasiokuwa na silaha hatimaye kupelekea kuuwawa kwa kijana mmoja na wengine kujeruhiwa vibaya.

  Tarehe 02/09/2012 wakati CHADEMA ikiwa kwenye mikutano yake ya ndani na kufungua ofisi za matawi yake mapya mkoani Iringa, mamia ya askari walikusanyika kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA kwa kutumia mabomu na risasi za moto hivyo kupelekea kumlipua na kumuua Daudi Mwangosi, mwandishi wa habari wa kituao cha Televisheni cha Channel 10 aliyekuwa akiripoti shughuli za CHADEMA huku idadi ya wafuasi wa chama hicho wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

  Matukio haya ni mfululizo wa matukio mengine ya mauaji ya kisiasa yaliyotokea mapema mwaka huu (2012) ni pamoja na matukiyo yaliyohusisha; mauaji ya mwanachama wa CHADEMA Mbwana Masudi kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Igunga mwezi Septemba mwaka 2011, uchinjwaji wa kiongozi wa kata wa CHADEMA , Msafiri Mbwambo mara tu baada ya uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru Mashariki mwezi wa April 2012 na mauaji ya raia watatu mnamo tarehe 05/01/2011 jijini Arusha kwenye maandamano ya amani yaliyolenga kupinga uchaguzi usio wa kidemokrasia wa Meya wa jiji hilo.

  Katika hatua nyingine, msajili wa vyama vya siasa Tanzania ametangaza kutishia kuifuta CHADEMA katika usajili kwa madai kuwa ndio msingi wa vurugu zote hizoKutokana na hali inavyo endelea nchini Tanzania;IYDU inaitaka serikali ya Tanzania kuheshimu uwepo wa vyama vya siasa vya upinzani na haki yao ya kukutana na kuandamana kwa amani.

  IYDU inaitaka serikali ya Tanzania kuheshimu haki ya vyama vya siasa vya upinzani kuendesha mikutano yake ya ndani.IYDU inataka serikali ya Tanzania kuheshimu Uhuru wa mawazo na haki za kupata na kutoa habariIYDU inawataka Jeshi la polisi nchini Tanzania kutumia njia za amani badala ya nguvu zisizo na tija katika kulinda na kuimarisha amani na utulivu.

  IYDU inaitaka serikali ya Tanzania kuhakikisha wale wote wanaohusika na mauaji wanachukuliwa hatua na kwamba vyombo huru vifanye uchunguzi wa mauji haya.IYDU inahimiza jumuiya ya kimataifa kuishinikiza serikali ya Tanzania kuhakikisha CHADEMA haibughudhiwi katika kufanya shughuli zake kikatiba.[​IMG]
   
 2. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Imechapishwa wapi na chombo gani cha habari?
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mbona hueleweki mkuu?
   
 4. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2015
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,523
  Likes Received: 25,351
  Trophy Points: 280
  kumbe ni kweli BAVICHA imevuma dunia yote !
   
Loading...