Ziara ya waziri wa China East Africa yaipa Tanzania viwanda 200

Naton Jr

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
7,867
19,258
Waziri wa mambo ya nje wa china Wang Yi amewasili Tanzania kwa ziara ya siku Moja, ikiwa ni utekelezaji wa mazungumzo juu ya mpango wa maendeleo ya viwanda kati ya Tanzania na China.
Huku viwanda takriban 200 vikitarajiwa kujengwa kufikia mwaka 2020.

Munira Hussein amezungumza na Afisa habari wa wizara ya mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mindi Kasiga juu ya ziara hiyo.

Chanzo: BBC
 
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi azuru Tanzania - BBC Swahili

Zito Kabwe na ndugu zake wa chadema wakisikia hii habari wanaweza kufa kihoro kwa chuki, na kwa kuongezea pia mvua zimeanza kunyesha hivyo hakuna baa la njaa!
 
Inaonekana Tanzania inaenda kuwa taifa lenye viwanda vingi East Africa and Central baada ya miaka 3, bandari ya Bagamoyo nayo yatajwa.
 
Nchi ya viwanda tulo ahidiwa kwwnye campaign ndi hiyooooo
 
Ni kweli kabisa pia habari zinasema wataihuisha TAZARA na Kujenga reli ya kati. Ni jambo la kihistoria na wala China hajawahi kufanya hivi katika taifa lolote.

[Udumu udugu wetu kati ya Tanzania na China.]
Duuu sio mchezo hii haiijawahiii kutokea popote pale ndani ya uumbaji
 
Tanzania na China tumetoka mbali Sana enzi za the legendary JK Nyerere na Mao Zedong katika mradi wa TAZARA wachina wengi walipoteza maisha Tanzania sababu yetu hivyo jambo lolote ambapo yupo Tanzanian na Chinese paheshimu sana.
Hongera kama itatendeka japo Waswahili ni wale wale.
 
Nafikiri nayo Bagamoyo itahusika na mamia haya ya viwanda
tmp_8446-12507515_1042049659192361_4477648731092421548_n.png2118123600.jpg
Ni Pamoja na Bagamoyo Port???? Na Kigoma Dubai ya Africa????
 
Udugu kati ya nchi hizo mbili na wa muda murefu sana. China iliweza kuingia Umoja wa Mataifa na baadae kubwa na kura ya Veto kutikana na juhudi kubwa zilizofanywa Salim Ahmed Salim alipokua UN kwa kadri ya maagizo ya J K Nyerere. Ndio maana China hawatosahau historia hiyo.
 
Back
Top Bottom